Wachezaji fumbueni macho

Choga Cosmasy

Member
Feb 8, 2017
18
32
Na
Cosmasy Choga

Ukiwa shuleni utajifunza mambo ya lensi mbinuko na mbonyeo na kila moja hufanya kazi yake mbinuko kufanya uone mbali wakati mbonyeo kufanya uone Karibu,anyway Soka nalo ni kama sayansi vile unapaswa kuyajua hayo kabla ya na baada ya.

Vipaji vingi vya soka vinaibuka na kufanikiwa kutamba lakini wengi wameshindwa kupata mafanikio makubwa tofauti na ilivyotarajiwa hapo awali,Wengi huanza kuvuma katika umri wa miaka 17 lakini saba baadae wamepotea yaani 24,unaweza kujiuliza alianza shule akaishia la pili lakini mbona anaelewa vizuri utacheka tu ni kwamba ameshindwa kutumia ile sayansi ya lens mbinuko akameza madini ya lens mbonyeo ni kosa.

Tuone wapo wachezaji kama Chuji,Ngassa,Bahanuzi,Henry,Ab
dulhalim,There,Bahanuzi,Nizar na wengine kama hawa,kama ingekuwa safari basi hawa waliaza kabla ya Samatta lakini kuvaa miwani ya kuona Karibu kulipoza Soka lao,kama lens mbinuko wangeitendea haki haya ya Ulimwengu tungezungumza kuazia 2005 huko na Leo yangekuwa marudio tu na kusema huyu kavunja rekodi.

Ni lini mtasema tunavunja rekodi za mess,ronaldo,Robihno na nyingine?,ama miwani yetu ni hapa hapa mchezaji umefika hadi nje ya Africa, mchezaji umeenda hadi marekani lakini bado fahari yako ukaja kujivunia kutua azam fc ni aibu hiyo,umepaa hadi Vancouver huko fahari yako imekuja kuzimia mwadui,mbeya city ni ajabu.

Hili ni ombi kwenu mliosalia pasueni miwani ya lens mbonyeo na mtumie miwani ya lens mbinuko,mwagieni maji nyayo za Frank domayo mkakanyage unyayo wa Ulimwengu historia zenu zije ziwe historia inayovunjwa maana nimechoka kusikia ulaya ndio wamezoea kuvunja rekodi za waliotangulia.

Lakini lens hii viongozi wa timu mtumie karne hii sio ya kupoteza mabilioni ya pesa ni karne ya kuingia katika club tajiri duniani kuwa na academics ni utajiri,kumiliki viwanja ni utajiri pia fahari si kununua wachezaji bila kuuza mchezaji bali ni kutumia wachezaji mliowakuza na kufanya biashara,ujanja si kudanganya ujanja ni kufanya uongo wa vitendo chanya ni aibu kuona miaka 21-80 unamiliki uwanja wenye kuhifadhi kambale,dagaa na vyura ama Kobe.

Nahitimisha kwa kusema Ipi faida ya rasilimali watu wa vilub hadi sasa????,unapiga hesabu ya mashabiki 50millions lakini bado unakuwa tegemezi,unapiga hesabu ya member 35 million lakini hujui niamke vipi.

e10e1550edea250fe6b0a4ccf4f25322.jpg
 
Back
Top Bottom