Wacheza dili wa ndege ‘mpya’ ATCL hawa hapa

Wacheza dili wa ndege ‘mpya’ ATCL hawa hapa

BASIASI

JF-Expert Member
Joined
Sep 20, 2010
Posts
9,732
Reaction score
5,011
Wacheza dili wa ndege ‘mpya' ATCL hawa hapa



VIGOGO wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), waliofanya dili la kukodisha ndege chakavu aina ya CRJ 200 na kutangaza kwamba wameinunua, wamebainika.

Vigogo hao wamebainika katika mwendelezo wa uchunguzi uliofanywa na Tanzania Daima kwa kutumia vyanzo vyake vya kuaminika kutoka ndani ya shirika hilo.

Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili umebainisha kwamba ndege hiyo ambayo ni mzigo kwa taifa, ilikodishwa na uongozi wa ATCL ukiwahusisha viongozi wakuu ambao ni Mkurugenzi Mkuu wa ATCL Kapteni Milton Lazaro.

Mkurugenzi Mwendeshaji Kapteni Richard Shaidi na Mwenyekiti wa Bodi ya ATCL, Salum Msoma.

Tanzania Daima ilipomtafuta Kapteni Lazaro alijibu kwa ukali akisema: "Kama mnataka kuendelea kuandika andikeni kwa sababu tayari mshaandika wakati mwanzo niliwaambia subirini na hamkufanya hivyo.

Alipoulizwa kuhusu ukweli wa ndege hiyo alisema: "Nashangaa mnaniuliza nini wakati mmeshaandika kwamba ndege hiyo ni mbovu. Kwa sasa nipo kwenye kikao, hivyo siwezi kuzungumzia suala hilo, ninyi endeleeni kuandika.

Pamoja na kwamba gazeti hili lilidokezwa kwamba Mkurugenzi Mwendeshaji wa ATCL, Kapteni Shaidi ana uwezo wa kuingia katika bodi kutokana na cheo chake, lakini alikana kuwa miongoni mwa viongozi wanaoingia kwenye bodi hiyo.

Aliongeza kuwa: "Si sahihi kwamba mimi naingia kwenye bodi, na hivyo siwezi kuzungumzia chochote kuhusu suala hilo.

Majina ya wakuu hao waliohusika yamebainika wiki moja baada ya gazeti hili kuandika ukweli kuhusu upotoshaji uliofanywa na shirika hilo la umma kwa kuwaeleza wananchi kwamba ndege hiyo aina ya CRJ 200 ni mpya na imenunuliwa nchini Canada.

Uchunguzi wa gazeti hili ulibaini kwamba ndege hiyo ni chakavu na ni mzigo kwa taifa kutokana na uendeshaji wake kutumia kiasi kikubwa cha fedha.
Ulibaini kwamba ndege hiyo imekuwa ikitumia kiasi cha dola 4,500 za Marekani ambazo ni sawa na sh milioni 7.2 kwa saa inapokuwa angani na inapotua kiwanjani hugharimu kiasi cha dola sawa na sh 320,000.

Ndege hiyo ambayo imekodiwa kwa muda wa wiki tisa imeigharimu ATCL kuwalipia marubani wake watano kutoka Kenya malipo ya dola 500 za Marekani ambayo ni sawa na sh 800,000 kwa siku kwa ajili ya malazi ya hoteli ya hadhi ya nyota tano.

Gharama nyingine za marubani hao ni pamoja na usafiri kiasi cha dola 200 za Marekani sawa na sh milioni 1.6 kwa wote watano.

Tanzania Daima limegundua kwamba baada ya kukodiwa kwa ndege hiyo, gharama za kuitoa Kenya na kufikisha nchini zilikuwa dola 6,000 za Marekani ambazo ni sawa na sh milioni 9.6 na itakapomaliza muda wake wa wiki tisa itatakiwa kurudishwa Kenya kwa kiasi hicho hicho cha fedha.

Ndege hiyo imebainika kukodishwa nchini Kenya katika Shirika la Ndege la Fly 540 ambalo kabla ya shirika hilo kutetereka kiuchumi ndege zake zilikuwa zikifanya safari zake hapa nchini.

Vyanzo vyetu kutoka ndani ya ATCL vimeeleza kuwa kama shirika hilo lingekuwa na nia ya kupunguza gharama ya uendeshaji, lingenunua ndege aina ya DASH-8 inayotumiwa na shirika hilo ikiwa na uwezo wa kubeba watu 50 kama ilivyo kwa CRJ 200 ambayo imekuwa na uwezo wa kubeba mizigo mingi zaidi ya CRJ.

Ndege aina ya DASH -8 pamoja na kufanya kazi sawa na CRJ 200, lakini gharama za uendeshaji wake ni nafuu kwa sababu marubani na wahandisi wake wanatokea nchini.

Kwa upande wa gharama za uendeshaji, Dash-8 inapokuwa angani hutumia dola 2,500 za Marekani ambazo ni sawa na sh milioni nne kwa saa,vinayotofautiana kwa zaidi ya sh milioni 3.6, na pindi inapotua kiwanjani hugharimu kiasi dola 200 sawa na sh 320,000.

Tanzania Daima limegundua kwamba sababu za ndege hiyo inayonasibiwa kuwa mpya kuendeshwa na marubani, wahandisi kutoka Kenya imetokana na usajili wake kufanyikia nchini humo na si Tanzania kama ATCL ilivyojinasibu awali.

Uingizaji wa ndege hiyo ya CRJ 200 unafananishwa na ule wa Boeing 727 ambayo ilinunuliwa Lebanon na hatimaye imefia Kilimanjaro na kuwa kiota cha ndege.


Chanzo: Tanzania Daima
 
Sasa kama ushahidi wote huo upo mamlaka zinazohusika zinangoja msaada wa watu wa marekani kuwafungulia mashtaka? Au ndo yale ya ushahidi ni dhaifu ya dpp? Hebu hao takukuru wanoe vichwa kwani dpp mpya namwaminia siyo kama yule billionaire aliyepewa ulaji mwingine.
Kama kina mramba wameshtakiwa hao makepteni wana kinga gani?
 
Hii habari mbona imekaa kimaslahi zaidi.., its as if kuna mtu alikuwa nataka inunuliwe Dash ili yeye apige hela, badala yake imekodishwa hito CRJ 200 ndio roho inamuuma..
 
Kuna kila sababu ifike wakati kuwadungua risasi watu wa aina hii, tumechoka na ufisadi Tanzania, maana watunzi wa sheria wanatunga sheria zinazowalinda watunga sheria wenyewe, mafisadi na jamaa zao kwa maslahi yao

Tufikiri, tutafakari na kisha tuchukue hatua
 
4th January 2011


Wikileaks has revealed diplomatic cables complaining of favouritism and suspicion of corruption in the manner Air Tanzania Company Limited (ATCL) went about shopping for jetliners for its ageing fleet four years ago.According to the cables, carried in the New York Times of Sunday, January 2 this year the US Embassy in Dar es Salaam fighting for Boeing then said: "As Air Tanzania shops for new airplanes for its ageing fleet, we remain troubled by separate press reports, quoting Air Tanzania leadership and most recently the Minister of Infrastructure that a decision has been made in favour of Airbus." This decision would have been made without any serious negotiations with Boeing. We have actively engaged at the highest reaches of this government, and for the moment halted the rush to Airbus and opened a window that Boeing intends to exploit."


The newspaper report titled: "Diplomats Help Push Sales of Jetliners on the Global Market. Tanzania and the Fight to Stop Airbus Sale," said Boeing executives, at times, were pressed by foreign government officials and airline executives to hire "agents" or other intermediaries to help deliver a sale.According to the diplomatic notes, Air Tanzania seemed to be seriously evaluating the leasing and sale options offered by Boeing, "but we do not believe we are out of the woods, in view of early efforts to pressure Boeing to hire an "agent," and subsequent rumours that China is tying aid to purchase of Airbuses in order to give business to the joint manufacturing facility being built in China," the US embassy said.


It said in June 2007, Boeing had submitted a request for advocacy through the Department of Commerce's International Trade Administration, and Ambassador Retzer, the Deputy Chief of Mission (DCM) and Economic Counsellor (EconCouns) met with Rob Faye, Regional Director of Sales for Boeing Commercial Airplanes, on several occasions.
It said Boeing's early dealings with top officials of the airline beginning in June suggested (to Post) that the company's fear of outside influence or corruption might be legitimate.


The report said in subsequent meetings with Faye, the DCM raised the issue of Air Tanzania's dealings with Boeing and Airbus in conversations with a close advisor to President Jakaya Kikwete.According to the report the DCM specifically noted Air Tanzania Managing Director and CEO, David Mattaka's unusual "suggestion" that Faye should contact a wealthy South Asian hotelier, who subsequently suggested to Faye that he would need his services to open the right doors in government. Faye flatly refused, responding that Boeing does not use "agents" in Tanzania or elsewhere.


The report released as comment that "Agents" and steep "commissions" have been at the heart of several corruption scandals here (Tanzania), including a BAE radar deal in which the GOT paid a 31 percent commission to a Tanzanian agent, much of which ended up in Swiss bank accounts, according to a UK Parliamentary investigation. Despite the fact that the UK shared this evidence with Tanzania's corruption board, no evident action has been taken.The presidential advisor later got back to the DCM, telling him that President Kikwete was "incensed" upon learning that senior Air Tanzania officials might be intending to profit personally from the deal.


The report said Ambassador Green raised MCC (Millenium Challenge Corporation) Compact, the importance of transparency to the investment climate, and a level playing field for Boeing in his presentation of credentials to President Kikwete on September 12.Earlier the DCM had called on the Infrastructure Minister and spoken with a close advisor to the President underscoring the same points. "We will continue to press hard not only on behalf of Boeing, but the importance of transparency and a level playing field to the positive investment climate Kikwete is working to create," said the report.


It said further that on August 9, Boeing's Faye met with Maua Daftari, Deputy Minister of Infrastructure, and Dr. Bartholomew Rufunjo, Director of Transport and communications in the Ministry of Infrastructure (the Ministry that makes all financial decisions regarding Air Tanzania). Faye reported his meetings with both Daftari and Rufunjo were promising.
Both officials mentioned more than once the importance of a fair and level acquisition process for Air Tanzania's development. David Mattaka, CEO of Air Tanzania, went out of his way to tell Faye on August 10 that Air Tanzania did not use agents.


Mattaka repeated this statement during a meeting between Faye and the Air Tanzania board of directors. Faye reported that it was apparent that there had been some communication with the Ministry, presumably from State House, to ensure there would be no "go-betweens" in Air Tanzania's dealings with Boeing. On the sidelines, Mattaka reportedly mentioned to Faye that he thought the pressure was originating with the US Embassy.It said Ambassador Retzer forcefully raised the issue of combating corruption in his last public speech before leaving on August 31.


On September 2, forty-eight hours after Retzer departed the country, the Tanzanian press reported for the second time that Air Tanzania was in the process of procuring eight Airbus planes, and extensively quoted Tanzanian Minister of Infrastructure, Andrew Chenge."We did not view the timing of the second announcement -- on the heels of Retzer's departure and before Ambassador Green had arrived and been credentialed -- as a coincidence," said the cable.The report said on September 7, the DCM and EconOff met with Minister Chenge, raising President Kikwete's trip to the United States and his plan to take a large business delegation.


Kikwete would be marketing Tanzania as a prime location to trade and invest. It was important, therefore, that a major US corporation like Boeing compete on a level playing field with Airbus, so its message to the US business community would echo Kikwete's message.The DCM said Boeing and the Embassy had been confused by recent press reports regarding Air Tanzania's acquisition of new aircraft, and asked Chenge to clarify the status of negotiations.Chenge said contrary to his purported statements to the Tanzanian press, no final decision had been made on whether Air Tanzania would acquire Airbus or Boeing airplanes.


However, the issue of financing was also a primary concern due to a lack of government funding for the new aircraft. He stated that he could say "with certainty" that no decision has been made, but his Ministry was "very cautious on how to proceed because (they) don't have the money." He said he understood Boeing could help open doors to financing possibilities, but "certain deadlines" needed to be met.The report said the DCM stressed that regardless of the outcome, the Embassy wanted to see that Air Tanzania is engaged in fair and transparent negotiations. He pointed out that Tanzania would benefit from giving Boeing the chance to underbid Airbus.

The DCM ended the meeting by mentioning the upcoming vote on the Millennium Challenge Corporation (MCC) Compact for Tanzania, and the importance of transparency to sustaining any Compact that eventually would be signed. On the way out, Chenge's staffer reportedly told the DCM that he was aware that Chenge had "misspoken" and been "misquoted" in the press, and that his office had already received several calls for clarification.Minister for Transportation Omar Nundu told this paper yesterday that he was not aware of the report."I am not aware of the reports. I do not know," said Nundu.This paper called Andrew Chenge for the comment but his phone could not be received. Mattaka who has since moved from ATCL was not reachable as his phone was switched off.



SOURCE: THE GUARDIAN
 
Kuna kila sababu ifike wakati kuwadungua risasi watu wa aina hii, tumechoka na ufisadi Tanzania, maana watunzi wa sheria wanatunga sheria zinazowalinda watunga sheria wenyewe, mafisadi na jamaa zao kwa maslahi yao

Tufikiri, tutafakari na kisha tuchukue hatua

Ipo siku tu...tutavuana nguo kwakuwa wale walioko kwenye viti vyakuzunguka hatuoni km sisi tuliokaa kwenye benchi za mbao km tuna akiri.napata uchungu sana kuona watu makampuni ya UMMA yamekuwa ya viongoz na familia zao, nimewahi kuomba kaz pale km km airline economist km mwenye tahaluma hiyo, hata hivyo nafasi hiyo kwa kubebwa alikaa mwenye diploma ya sociology .kisa mtoto wa boss. Ipo siku tutaanza kuviziana barabarani tunalambana maana km rwanda, kwani mapapa yamezidi kukumbatiwa .Mi najiuliza mtu km CHENGE ,bado anafanya nn kwenye mfumo.kigunge woote hao toa nje, leo wimbo wa tz hatuna wataalam sijuh wanatoa wapi ujasiri wa kuuimba tena kwa fitina wakijua danganya toto.leo tz wako professional kila idara.inauma sana lawama hizi na adhabu hii imtafune J.Kikwete siku akikutana na Mungu.
 
Wacheza dili wa ndege ‘mpya’ ATCL hawa hapa



VIGOGO wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), waliofanya dili la kukodisha ndege chakavu aina ya CRJ 200 na kutangaza kwamba wameinunua, wamebainika.

Vigogo hao wamebainika katika mwendelezo wa uchunguzi uliofanywa na Tanzania Daima kwa kutumia vyanzo vyake vya kuaminika kutoka ndani ya shirika hilo.

Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili umebainisha kwamba ndege hiyo ambayo ni mzigo kwa taifa, ilikodishwa na uongozi wa ATCL ukiwahusisha viongozi wakuu ambao ni Mkurugenzi Mkuu wa ATCL Kapteni Milton Lazaro.

Mkurugenzi Mwendeshaji Kapteni Richard Shaidi na Mwenyekiti wa Bodi ya ATCL, Salum Msoma.

Tanzania Daima ilipomtafuta Kapteni Lazaro alijibu kwa ukali akisema: “Kama mnataka kuendelea kuandika andikeni kwa sababu tayari mshaandika wakati mwanzo niliwaambia subirini na hamkufanya hivyo.

Alipoulizwa kuhusu ukweli wa ndege hiyo alisema: “Nashangaa mnaniuliza nini wakati mmeshaandika kwamba ndege hiyo ni mbovu. Kwa sasa nipo kwenye kikao, hivyo siwezi kuzungumzia suala hilo, ninyi endeleeni kuandika.

Pamoja na kwamba gazeti hili lilidokezwa kwamba Mkurugenzi Mwendeshaji wa ATCL, Kapteni Shaidi ana uwezo wa kuingia katika bodi kutokana na cheo chake, lakini alikana kuwa miongoni mwa viongozi wanaoingia kwenye bodi hiyo.

Aliongeza kuwa: “Si sahihi kwamba mimi naingia kwenye bodi, na hivyo siwezi kuzungumzia chochote kuhusu suala hilo.

Majina ya wakuu hao waliohusika yamebainika wiki moja baada ya gazeti hili kuandika ukweli kuhusu upotoshaji uliofanywa na shirika hilo la umma kwa kuwaeleza wananchi kwamba ndege hiyo aina ya CRJ 200 ni mpya na imenunuliwa nchini Canada.

Uchunguzi wa gazeti hili ulibaini kwamba ndege hiyo ni chakavu na ni mzigo kwa taifa kutokana na uendeshaji wake kutumia kiasi kikubwa cha fedha.
Ulibaini kwamba ndege hiyo imekuwa ikitumia kiasi cha dola 4,500 za Marekani ambazo ni sawa na sh milioni 7.2 kwa saa inapokuwa angani na inapotua kiwanjani hugharimu kiasi cha dola sawa na sh 320,000.

Ndege hiyo ambayo imekodiwa kwa muda wa wiki tisa imeigharimu ATCL kuwalipia marubani wake watano kutoka Kenya malipo ya dola 500 za Marekani ambayo ni sawa na sh 800,000 kwa siku kwa ajili ya malazi ya hoteli ya hadhi ya nyota tano.

Gharama nyingine za marubani hao ni pamoja na usafiri kiasi cha dola 200 za Marekani sawa na sh milioni 1.6 kwa wote watano.

Tanzania Daima limegundua kwamba baada ya kukodiwa kwa ndege hiyo, gharama za kuitoa Kenya na kufikisha nchini zilikuwa dola 6,000 za Marekani ambazo ni sawa na sh milioni 9.6 na itakapomaliza muda wake wa wiki tisa itatakiwa kurudishwa Kenya kwa kiasi hicho hicho cha fedha.

Ndege hiyo imebainika kukodishwa nchini Kenya katika Shirika la Ndege la Fly 540 ambalo kabla ya shirika hilo kutetereka kiuchumi ndege zake zilikuwa zikifanya safari zake hapa nchini.

Vyanzo vyetu kutoka ndani ya ATCL vimeeleza kuwa kama shirika hilo lingekuwa na nia ya kupunguza gharama ya uendeshaji, lingenunua ndege aina ya DASH-8 inayotumiwa na shirika hilo ikiwa na uwezo wa kubeba watu 50 kama ilivyo kwa CRJ 200 ambayo imekuwa na uwezo wa kubeba mizigo mingi zaidi ya CRJ.

Ndege aina ya DASH -8 pamoja na kufanya kazi sawa na CRJ 200, lakini gharama za uendeshaji wake ni nafuu kwa sababu marubani na wahandisi wake wanatokea nchini.

Kwa upande wa gharama za uendeshaji, Dash-8 inapokuwa angani hutumia dola 2,500 za Marekani ambazo ni sawa na sh milioni nne kwa saa,vinayotofautiana kwa zaidi ya sh milioni 3.6, na pindi inapotua kiwanjani hugharimu kiasi dola 200 sawa na sh 320,000.

Tanzania Daima limegundua kwamba sababu za ndege hiyo inayonasibiwa kuwa mpya kuendeshwa na marubani, wahandisi kutoka Kenya imetokana na usajili wake kufanyikia nchini humo na si Tanzania kama ATCL ilivyojinasibu awali.

Uingizaji wa ndege hiyo ya CRJ 200 unafananishwa na ule wa Boeing 727 ambayo ilinunuliwa Lebanon na hatimaye imefia Kilimanjaro na kuwa kiota cha ndege.


Chanzo: Tanzania Daima

Kama kawaida bongo ni shamba la bibi kila anayepata upenyo anavutia kwake.
 
Dah! Bongo yetu. Sasa wako wapi waliokuwa wanamshutumu shirima kuanguka kwa atc kwenye pósti ya precision air kuuza ndege zake. Ndio maana nimekataa kata kata kujiongezea elim ingawa inapatikana bure hapa nikiona eti wasom kama chenge na dizain iyo ndio wanategemewa nchin. Ntakomaa kubeba boksi nadiploma yangu. Mijitu inaiba wazi wazi bila huruma kodi za wavuja jasho. Kwanini mapinduzi ya aman yasitokee bila vita tubadilishe utawala? ?? Nyambaff zetu
 
Watanzania tunaishi kwa kudra za mungu tu! Ndio manna nota lipokuwa homu nikiiugua cendi hospitali nilikuwa napona kimungumungu tu. Hospitali za walala hoi kaa mm ni bora u hende kwa mganga wa kienyej
 
Naona wanamalizia kuliua kabisa hili shirika.. Hawa wakurugenzi na Shirima hawana tofauti.. Wote ni wahujuma
 
Mimi hofu yangu ni kuwa isije kuwa jeneza linalopaa.
 
Back
Top Bottom