The August
JF-Expert Member
- Oct 9, 2018
- 1,079
- 2,027
Hello JF!
Leo ningependa kushare nanyi na tutafakari pamoja juu ya utamaduni huu umaarufu wa jamii ya watu wa kaskazini mwa Tanzania hasa mkoa wa Kilimanjaro. Wakazi wa eneo hili Kila ufikapo mwisho wa mwaka huongozana kurudi majumbani kwao uchagani. Wengi tumezoea kusema wanakwenda kuhesabiwa. Mimi sio mchaga , hivyo kama wanaenda kuhesabiwa au la, siwezi lisemea hilo.
Mwaka 2015 niliongozana na rafiki yangu mmoja kwenda huko. Kwa kweli utamaduni ule ulinivutia sana na kuufanya niutazame katika mtazamo chanya wa kiuchumi na kijamii.
Sina hakika kama kuna kabila lingine lenye utamaduni huu nchini, lakini kadri siku zinavyokwenda inanipa fikra kuwa labda utamaduni huu ndiyo chanzo hasa cha watu hawa kuenea kwenye ofisi nyingi nyeti, ndio sababu kutawala na kuenea kila eneo ilipo shughuli za kiuchumi, au ndio sababu ni ajabu kukuta diwani mchaga, kule usukumani lakini si kinyume chake.
Utamaduni huu nimeuona unafaida kubwa kiuchumi na kijamii kama ifuatavyo.
1. Ndugu kufahamiana.
Pindi watu wakutabapo katika kusanyiko la nyumbani ndipo hapa kumjua shangazi, mjomba, kaka, babamdogo. Hapa ndipo unajua shangazi yuko idara fulani mkoani Tabora, au ni meneja masoko wa kampunj fulani kule mtwara, au ni mkuu wa shule fulani kule Mbeya kama si meneja wa bank tawi la bariadi, au pia ni mkurugenzi wa shirika ama halmashauri fulani. Kwa muktadhaa huu kijana mwemye CV yake mkononi ni rahisi kushikwa mkono na kuwekwa kitengo fulani au mwenye kampuni kupewa tender ya ujenzi katika halmashauri.
2. Kujuana changamoto ziwakabilizo wanachama wa familia.
Waswahili husema ng'ombe akivunjika mguu hukimbilia zizini. Ndio kusanyikika hili husaidia kila mtu wa familia kueleza shida yake, amekwama wapi, biashara yake imekwama wapi. Hapa ndipo watu wanaweza shikana mikono na baraka kuanzia hapa.
3. Hamasa ya kutafuta pesa.
Katika kusanyiko hili, watu wanakuja na magari, watu wanakuja na familia zao. Hili linatoa hamasa kubwa ya mtu kupambana akijua kuwa Next december nisionekane fala.
4. Kuboreka kwa makazi ya nyumbani.
Jamii nyingi za ni kawaida mtu akishalowea mjini na kuoa hupotelea huko, siku ya msiba ukifika tunakuta nyumbanj kuko hohe hahe..katika mfumo huu wa wachaga, familia ikikusanyika inaona mapungufu yaliyopo nyumbani. Hivyo wanafamilia wanaweka nadhiri na commitment ya kufanya ukarabati. Ndio maana si ajabu vijiji kule kukuta vina hali nzuri ya maisha.
Hivyo kwa utamaduni huu wa wenzetu tunaweza jifunza sana jinsi gani jamii au familia inaweza ikaendela. Familia zetu ni vyema kujenga utamaduni huu wa kuwa na kipindi fulani cha mwaka kukutana nyumbani. Faida zakd ni kubwa mno...
We think globally and act locally.