Hazard CFC
JF-Expert Member
- Apr 7, 2015
- 16,620
- 38,653
MWACHE MCHAGGA AITWE MCHAGGA
Jamaa mmoja toka kiboriloni alienda Benki na kuomba mkopo wa shilingi 200,000 ili asafiri kwenda Dar. Ofisa mikopo akamwambia lazima ajaze fomu fulani na awe na kitu cha kuweka dhamana. Mdau akajaza fomu kisha akakabidhi funguo za benzi yake aliyokuja nayo pamoja na nyaraka za umiliki wake kwa meneja. Ofisa mikopo akaiingiza gari kwenye yadi ya benki na kumpa mchagga laki mbili yake. Kilichomshangaza meneja wa benki ni kuwa benzi ile ina thamani ya 255,000,000 na kuwa iweje mwenye gari kama hii amekosa 200,000. Baada ya wiki 2 mchagga akarudi na kurejesha mkopo wote pamoja na riba ya shilingi 15,000. Afisa mikopo akafurahi lakini akamuuliza, inawezekanaje una gari la thamani hivi na ukaangaika kupata mkopo wa shilingi laki 2? Mchagga akamjibu, Ni wapi hapa Moshi utapata mahali salama kupaki gari yako kwa wiki mbili kwa kodi ya shilingi 15,000 tu?