Radio Producer
JF-Expert Member
- Feb 4, 2011
- 728
- 320
Waheshimiwa.
Mnaonaje mkianzisha radio ili kuisaidia jamii yenu kwa kupata taarifa kwa urahisi? Mh! najua mnaweza kuzitumia radio zenu kwa kampeni pia hapo sasa:- angalia gharama zote kwa hapa chini:-
Heshima mbele Wakuu!!!
Leo nimeamua niweke maelezo ya kutosha juu ya kuanzisha radio kwa hapa Tanzania, bila kuwa na lugha ya kibiashara badala yake niweke ukweli wote ili mtu aone kabisa mwanzo au mwisho gharama zake zikoje.
Kwanza kabisa kuna makundi matatu ya radio:-
1. Commercial Radio. (Za kibiashara)
2. Public Radio (Radio za watu wenye lengo/dhumuni maalum, kama vile makanisa, mashirika, asasi n.k)
3. Community Radio (Radio za jamii, zinazowekwa kwa manufaa ya jamii, mara nyingi hazitengenezi faida japo imo ndani kwa ndani)
Unaweza kuamua wewe binafsi juu ya radio gani ungependa kuanzisha, inategemeana na wito wako. Gharama juu ya kila kundi la radio zinaweza kutofautiana kulingana na ubora, mfano radio ya jamii inaweza kuwa ya kawaida sana vifaa vya kawaida, lakini ya biashara inahitaji uwe na vifaa vizuri ili uweze kuingia kwenye ushindani. Nisiende mbali sana na lengo wacha nijielekeze kwenye pointi husika:-
Haya ni mambo muhimu kwanza ya kuzingatia unapotaka kufungua au kuanzisha kituo cha radio:-
1. Fanya uchunguzi wa masoko (Ni wapi radio yako uweke, mfano mkoani, wilayani, je kuna ushindani gani kwenye maeneo hayo, je maeneo unayoweka radio yanaweza kuvuta wadhamini wakubwa kama makampuni ya simu na wakaja kudhamini?)
2. Ukishapata eneo. Andika Pusiness Plan+Feasibility Study kwa ajili ya mradi wako. Katika Feasibility Study unatakiwa kuwasiliana na TCRA ili upewe fomu za kuombea leseni ambazo ndizo zinavipengele vizuri vya Feasibility Study utakavyovijana na baada ya hapo unaweza kusubmit hiyo moja kwa moja kama application. Moja na vipengele muhimu katika Feasibility Study ni:-
A: Specific ya vifaa vya radio yako vyote.
B: Memorundum/katiba ya kampuni yako na leseni yake ya usajili.
C: Structure ya uongozi ya radio unayotaka kuianzisha.
D: Financial Statement ya miaka 5 (hii ni muhimu zaidi)
E: Line up ya vipindi vya radio unayotaka kuanzisha.
E: Policy zote za radio.
N.k
3. Kuomba leseni TCRA.
4. Ununuaji wa Vifaa. (Kuna vifa vingine ni mpaka uwasiliane na TCRA ili upewe specification mf. kama STL)
5. Utengenezaji wa Studio.
6. Installations ya vifaa vya studio na transmission site.
7. Mafunzo
8. subiri TCRA wakupe leseni kisha uanze kurusha matangazo ya majaribio ya mieizi 3-6.
Gharama halisi za Radio inayoweza kusikika kuanzia KM 100-150.
1. Transmitter ya Watts 1500 Tshs 12,051,960/=
2. Antena Zake 2dipole Tshs 5,869,200/=
3. STL (Studio to Transmitter Link) Tshs 9,648,000/=
4. Vifaa vyote vya studio 2. (full set) Tshs 25,808,400/=
5. Freight Fee Tshs 3,296,400/=
6. Usajili TCRA Tshs 5,000,000/= na gharama zote zingine zitakazohitajika.
7. Kutengeneza studio Tshs 4,000,000/= (milango, accoustic materialsn.k)
8. Kuendesha mafunzo Tshs 4,000,000/= (kila kitu)
9. Kuandika Feasibility Study Tshs 3,000,000/=
10. Installations ya vifaa vyote na consultancy fee Tshs 7,000,000/=
Jumla Kuu ya vifaa bila local custom charge+mafunzo+TCRA Tshs 79, 673, 960/=
Gharama za uendeshaji kwa mwezi:-
1. Mshahara wa Meneja Tshs 700,000/= kwa kuanzia unamlipia nyumba.
2. Mshahara wafanyakazi 5@250,000/= Tshs 1,250,000/=
3. umeme Tshs 150,000/=
4. Maji 20,000/=
5. Mawasiliano na Internet 100,000/=
6. Usafiri/Mafuta Tshs 200,000/=
7. Stationaries Tshs 100,000/=
8. Pango la nyumba Tshs 250,000/=
9. Ziada Tshs 300,000/=
Jumla Tshs 3,270,000/= makadirio ya wastani.
hivyo jumla kuu ukitaka kuanzisha na kuendesha radio station kwa mwezi 1, inayoenda umbali wa Km 100-150
ni Tshs 82, 943, 960/= bila VAT+customs charge wakati wa kuingiza vifaa nchini.
Faida(Kipato) ya biashara ya Radio.
Utafaidikaje sasa na investiment hii kubwa:
1. Matangazo madogomadogo na muda wa hewani kwa wanaohitaji unaweza kukuingizia mpaka Tshs 10,000,000/= kwa mwezi hasa kama upo mkoani, hapa tayari utakuwa umepata gharama za kuendeshea radio.
2. ukipata wadhamni wakubwa kama makampuni ya simu, mfano ukapata makampuni matatu, kila kampuni kwa mwezi ikakulipa Tshs 3,000,000X3=9,000,000/=
3. Kuna mashirika huwa yanaendesha vipindi na matangazo kwa mwezi minimum Tshs 5,000,000/=
So kama radio yako imepata wadhamini wa hatua zote tatu hizo unaweza kupata mpaka Tshs 24,000,000/= kwa mwezi haya ni makadirio tu, uhalisia unaweza kupunguza au kuongeza mapato haya.
Na mwisho unaweza kuwa unaomba grant kupitia radio yako.
Jaman niishie hapa kwa kusema kwamba, mtu anaweza kukuambia kuanzisha radio kwa Tshs 20,000,000/= kila kitu lakini ukweli zitaongezeka tu ukiweka na gharama zingine, eidha gharama hizi zinaweza kupungua ukiamua kuweka radio ndogo zaidi. niishie hapa, kwa chochote au lolote ni PM kwa details zaidi.