Wabunge Wetu wa Ajabu!, Wanaachaje Bunge Lijipendekeze Kwa Serikali!, Wanajua Wajibu Wao?. Check 'n' Balance Itoke Wapi?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,498
113,604
Wanabodi,

Wakati taifa likiwa bado limepigwa na butwaa ya kilichomtokea Mhe. Tundu Lisu, najiunga na kumtakia uponyaji wa haraka, japo nakiri mimi ni miongoni mwa wale wanao leave all options open including "friendly fire", kama ilivyo issue ya kupotea kwa Ben Saanane, could be "an inside job", as a member of the 4th estate, tunawajibu wa kuzungumzia mustakabali wa taifa letu.

Angalizo
Naomba kuanza na angalizo: Ukosoaji wowote, utaofanywa kwa kinachofanywa na serikali yetu, na mihimili yake ya dola, kuwa we are doing a wrong thing, na kama unatolewa in good faith, kwa nia ya kujenga na sio kubomoa, na ukosoaji huo ukatoa ushauri wa the right thing to do, huitwa " a constructive criticism" ambao ni ukosoaji mzuri, ni very healthy katika ujenzi wa taifa lolote la kidemokrasia linaloheshimu uhuru wa kujieleza, (freedom of expression) na kuheshimu haki za binaadamu (human rights) kwa kuheshimu katiba na kufuata utawala wa sheria (the rule of law).

Serikali yoyote yenye nia ya dhati ujenzi wa taifa lake kwa kufuata misingi ya katiba nzuri na kuheshimu misingi ya haki binaadamu na utawala wa sheria!, inakuwa makini sana na hoja zozote zinazohusu katiba, sheria, taratibu na kanuni. Zikitokea kelele zozote zinazohusu ukiukwaji wa katiba, sheria, taratibu na kanuni, au uminyaji wa demokrasia, serikali makini zote, huzichukulia hoja hizi very serious kwa uzito unaostahili, serikali yoyote inayopuuzia hoja za ukiukwaji wa haki zilizotolewa na katiba, then serikali hiyo sio serikali sikivu, ni serikali ya ki imla, au ni ya kidikiteta!, na rais yoyote anayekiuka katiba aliyoapa kuilinda, huyo ni rais dikiteta. Vivyo hivyo Bunge linalokiuka kanuni zake, na kushindwa kuisimamia serikali, hilo ni Bunge Butu!.

Mihimili Mitatu ya Dola, Serikali, Bunge na Mahakama
Serikali nyingi za mataifa, zinazo heshimu katiba, na kufuata mfumo wa kidemokrasia na utawala wa sheria, zina mihimili mitatu ya dola ambayo ni Serikali, Bunge na Mahakama. Mihimili hii inatakiwa kuwa sawa kwa kufanya kazi kwa uhuru na kujitegemea bila kuingiliwa na Mhimili mwingine (independent) na wakati huo huo kila mhimili ukiwa ni mlinzi na mdhibiti wa mhimili mwenzake, (check and balance) ili mihimili mmoja usizidishe mamlaka yake na kuingilia mihimili mingine.

Kazi, Majukumu na Wajibu wa Mihimili ya Dola
Kwa wasiojua kuhusu kazi, wajibu na majukumu ya mihimili mitatu ya dola, watakipongeza kitendo cha taarifa ya kamati teuli ya bunge kuwasilishwa kwa rais, badala ya kuwasilishwa bungeni, wabunge wakatoa mawazo yao, kisha bunge likatoa azimio la bunge ambalo ndilo lingewasilishwa serikali kwa Waziri Mkuu, kisha Waziri Mkuu, akamkabidhi rais, azimio la Bunge, na sio mapendekezo ya Kamati Teule ya Bunge!.

Bunge Letu ni Bunge la Ajabu!, Wabunge Wetu ni Wabunge wa Ajabu
Kiukweli kabisa, wabunge wetu ni watu wa ajabu sana!, inawezekana ni watu wasiojielewa majukumu yao ni nini mule bungeni!. Wamewezaje kumuacha Spika, tena akiwa na Naibu Spika mbobezi wa sheria, kuliacha Bunge letu tukufu, kwenda kujipendekeza kwa mhimili wa the executive!, what has rais ambaye ndiye Mkuu wa The Executive, has to do na mapendekezo ya kamati teule ya Bunge?. Badala ya rais kupelekewa Azimio la Bunge, amepelekewa mapendekezo ya Kamati Teule!, Hii kama sio ajabu ya mwaka ni nini?.

Hayo yote yakifanyika, huku tunao wabunge makini, wamenyamaza, wanasheria manguli, nao wamenyaza, kama Bunge linafanywa ni idara ya serikali, Mkuu wa The Legislature, anakwenda kupiga magoti kujinyenyekeza kwa Mkuu wa The Executive, then nani atamsimamia nani na nani atamdhibiti nani kwa maana ya kufanya checks and balance?!.

Rais Magufuli Anapokea Taarifa ya Kamati Teule ya Bunge Kama Nani?.
Kwa mujibu wa Katiba yetu, japo rais wa JMT ni sehemu ya Bunge kwa kuliunda, kulivunja, kulihutubia, kusaini miswada kuwa sheria na kuteua Mtendaji Mkuu (Katibu wa Bunge), lakini rais sii mbunge na hahusiki na utendaji wa day to day activities za Bunge, hivyo alivyopelekewa ripoti ya Kamati Teule ya Bunge, kabla haijadadiliwa bungeni na kujumuisha maoni ya wabunge, amepelekewa kama nani?!.

Tumshukuru sana rais Magufuli kutamka hadharani kuwa ameyapokea mapendekezo yote ya kamati na atayatekeleza kwa asilimia 100%, utekelezaji huu ni kupitia discretionary powers za rais wa JMT aliyopewa na katiba yetu kuwa anaweza kuamua kutekeleza ushauri wowote, au kuamua kutotekeleza ushauri wowote anaopewa na yoyote at his discretion, at his plesures, na angeamua hawezi kutekeleza jambo lolote, lakini lingekuwa ni Azimio la Bunge, then ni kama amri ya mahakama, utekelezaji wa maazimio ya Bunge, sio at Presidents pleasures, but it is a compulsory obligation, na asipotekeleza, bunge linaweza kukutana na kumuwajibisha rais!.
The Doctrine of Separation of Powers, Checks And Balance
Kwa muda mrefu sana hapa nchini kwetu, tumekuwa na tatizo kwenye kitu kinachoitwa "The Doctrine of "Separation of Powers" and "Checks and Balances" kati ya mihimili hii mitatu ya dola, "The Legislature, The Executive and The Judiciary, ambavyo vyombo hivi vyote vitatu vinapaswa kuwa "huru bila kuingiliwa" "independence of its decisions" ili kila kimoja kiwe na nguvu zake chenyewe " powers" ambazo zimetenganishwa na kingine, "separations" ila pia vimepewa mamlaka ya kitu kinachoitwa "checks and balances" kama a watchdog of one another ili mihimili hii isivuke mamlaka yake, au ikitaka kuleta madhara, izuiliwe na one onother!.

Mamlaka za vyombo hivi vitatu, "Powers" za Bunge, Serikali na Mahakama, hazipaswi kuingiliwa na chombo kingine chochote, kumaanisha maamuzi ya serikali ni ya serikali yanatakiwa kuheshimiwa na Bunge na Mahakama, maamuzi ya Bunge yanapaswa kuheshimiwa na Serikali na Mahakama na Maamuzi ya Mahakama, yanapaswa kuheshimiwa na Bunge na Serikali, lakini kila siku, tunashuhudia jinsi maamuzi ya vyombo hivi, yanavyoingiliwa na vyombo vingine na hata katika yale majukumu yake ya msingi ya kila muhimili!, yaani Bunge kazi yake ni kutunga sheria, Mahakama kazi yake ni Kutafsiri sheria, na Serikali kazi ni ketekeleza sheria!.

Kuingiliana kwa Majukumu ya Bunge, Serikali na Mahakama
Kumekuwepo kuingiliana katika majukumu haya ya msingi, hali inayoleta migangano ya kuingiliana kwa muda mrefu, mfano kazi ya kutunga sheria ni kazi ya Bunge, lakini Mahakama katika baadhi ya maamuzi yake, hujikuta imetunga sheria kupitia maamuzi au huku zake mbalimbali ambazo hu set kitu kinachoitwa "precedents" na serikali katika utekelezaji wa majukumu yake, hujikuta imetunga sheria kupitia "executive orders" mbalimbali zinazotolewa kupitia "waraka" na kutangazwa kwenye gazeti la serikali, "Government Gazette" hivyo kuwa sheria!, ambako huku ni kuingilia majukumu ya kibunge kutunga sheria, serikali nayo inatunga sheria, mahakama nayo ni mtunga sheria, na serikali za mitaa nazo ni mtunga sheria ndogo, "by laws"!. Hivyo kila chombo ni mtunga sheria na sii bunge pekee!.

Kazi ya mahakama ni kutafsiri sheria na dispensing of justice, yaani kutoa haki, lakini kuna vyombo kibao vya kiserikali, vinatoa hukumu na adhabu mfano baadhi ya Mabaraza, (Quasi Judicial Bodies) na baadhi ya Wakala za serikali, TCRA, Sumatra, Ewura, SSRA, etc, zimepewa mamlaka ya kimahakama, au mabaraza, hutoa maamuzi na hukumu, mfano Ewura aliwahi kuvifungia na kuipiga fine vituo vya mafuta kwa kisingizio cha kuuza mafuta machafu, wamiliki wakaenda mahakamani, kwa hoja kuwa mwenye mafuta machafu ni supplier na sio wao, mahakama ikatupilia mbali uamuzi wa Ewura, na kuvifungulia, Bunge la Samuel Sitta likaingilia kati kuwa mahakama inaingilia uhuru wa Ewura na kuidhalilisha mbele ya jamii.

Kwenye jukumu la kutafsiri sheria, Mahakama ilitamka wazi baadhi ya sheria zinazotungwa na bunge ni "bad laws" na kutoa amri zifutwe kwenye vitabu vya sheria, "scraped out from the books of law" mfano haki ya mgombea huru, serikali ikangilia kati, na kufanya mabadiliko ya katiba na kukichomeka kipengele cha "mgombea lazima adhaminiwe na chama cha siasa", hivyo kuingilia uhuru wa mahakama, mahakama bado ikatamka kipengele hicho ni "unconstitutional" wanasheria nguli wakaitwa kama marafiki wa mahakama "amicus curiae" kuishauri mahakama kama ina uwezo wa kufuta kipengele cha katiba, wakakubaliana kuwa Mahakama, haina uwezo huo bali ni bunge ndilo pekee lenye uwezo wa kubadili kipengele cha katiba!, hii issue iliwasha moto mkubwa sana wa majadiliano kuhusu uhuru wa mahakama na haki kinga na madaraka ya bunge!.

Checks and Balance
Pamoja na kuwekwa kwa mipaka yote ya kutoingiliana, mihimili hii ya dola, imepewa mamlaka ya "checks and balance" kuingilia na kuuzuia mhimili mmoja usivuke mipaka ya mamlaka na madaraka yake kuleta madhara kwa taifa, hivyo vimepewa mamlaka ya kuingilia kati "intervention" pale inapoona mhimili fulani unajipa madaraka kuliko hata uwezo wake!.

Uwezo wa Bunge na Kamati Zake
Bunge limepewa mamlaka na uwezo wa kutunga sheria yoyote, ila bunge kabla halijaitunga hiyo sheria, sheria hiyo inayopaswa kutungwa lazima kwanza ianzie kwenye "the Executive" na Bunge likiisha itunga hiyo sheria, sheria hiyo haiwi sheria hadi Mkuu wa "the executive" yaani rais, aridhie!, na kuisaini, "accent" asiposaini haiwi sheria!. Hivyo kwenye uwezo wa Bunge kutunga sheria, bunge ni kikaragosi tuu, the real powers lies with the Executive!. Bunge linaelezwa linayo mamlaka ya kumuondoa rais madarakani, "impeachment" na rais anaelezwa kuwa ni sehemu ya Bunge!, ila huyu rais amepewa mamlaka ya kuliunda bunge, kulivunja bunge wakati wowote!. Ingawa Mkuu wa Mhimili wa Bunge ni Spika, ambaye anachaguliwa na wabunge, Mtendaji Mkuu wa `Bunge ni Katibu wa Bunge, rais ndie anayemteua mtendaji Mkuu wa Bunge, tukija kwenye mamlaka na madaraka, kati ya spika na katibu wa Bunge, Spika ana madaraka makubwa tuu ya kupiga kelele bungeni, lakini mamlaka ya kuendesha bunge ni Katibu wa Bunge, Spika lazima anyenyenyekee na kumpigia magoti katibu kumuomba fedha za uendeshaji, kama walivyo mawaziri lazima amnyenyekee Katibu wake Mkuu, where money lies, its where powers lies!.
Bunge Linapaswa Kuwa Independent
Bunge lilipaswa kuwa independent kuisimamia serikali, ikiwemo wabunge wasiwe mawaziri ili kuisimami serikali kikweli kweli kama alivyopendekeza Warioba!, lakini wabunge wetu ambao tuliwachagua wakaisimamie serikali, ndio hao wamepewa uwaziri, "ulaji!", kuna cha usimamizi tena hapo?!, unaweza kumlinganisha Mwakyembe yule wa Kamati ya Richmond na Mwakyembe huyu waziri?!. Msimamizi unapopewa ulaji, unategemea utasimamia nini?!, hivyo hiyo independence of the parliament is also nothing!, just a myth!.

Mahakama ni Huru?.
Mahakama nayo is said to be independent!, uamuzi wake ni wa mwisho!, Mkuu wa Mahakama anateuliwa na rais!, ile tuu kuteuliwa na mkuu wa nchi, tayari ume compromise uhuru wa mahakama dhidi ya serikali, Jaji Mkuu, lazima awe ni mtu wa shukrani kwa rais kumpatia ulaji!. Mahakama haina vote yake separate kwenye budget, bajeti ya mahakama iko chini ya wizara ya sheria!, ili mahakama itekeleze majukumu yake, kila wakati, Jaji Mkuu lazima awe mdogo, kwenda kunyenyekea kwa The Executives kuomba hela za kutoa haki, inapotekea serikali haijatenda haki, kweli unaitegemea mahakama hii as beggars as it is inaweza kuihoji serikali?!. Mahakama ikitoa hukumu ya capital punishment , hukumu hiyo haiwezi kutekelezwa hadi mkuu wa the executive asaini!. Kitu kikubwa na kibaya kuliko vyote kwenye uhuru wa mahakama ni jamaa mmoja kwenye the executive anaitwa DPP!, huyu ana mamlaka ya kuingilia kesi yoyote, mahakama yoyote, na ikiwa katika hatua yoyote kabla hukumu na kuifuta!, "nolle" bila kutoa maelezo yoyote wala sababu zozote, na uamuzi wa DPP ni wa mwisho, hauwezi kuhojiwa na mamlaka yoyote!. Hivyo kitu kinachoitwa uhuru wa mahakama is nothing but a myth!.

The Myth of "The Doctrine of Separation of Powers and Checks and Balances",
Kiukweli hii doctrine "The Doctrine of Separation of Powers and Checks and Balances", ilikuwa iko supposed kuwepo kiukweli ukweli, ila kiuhalisia, hakuna kitu kama hiki, its just a myth, serikali ndio kila kitu!, hakuna mahali popote bunge na mahakama zina total independence!, serikali ndio mambo yote, hivyo hili bunge letu, ni bunge zuga tuu mbele ya serikali, na hizi mahakama zetu, ni mahakama zuga tuu mbele ya serikali, serikali ndio mambo yote!, sasa inapotokea hivyo vyombo viwili ambavyo vyote ni zuga tuu vinata kupimana ubavu kwa jambo ambalo mtuhumiwa mkuu ni serikali!.
Hili la Bunge Kujipendekeza Kwa Serikali ni Kubwa Kuliko!.
Wengi Kati ya yote niliyowahi kuyashuhudia katika hoja hii ya the separation of powers, na Checks and Balance, kubwa kuliko ni hili la Bunge kujipendekeza kwa serikali, ni kuwa Bunge linawajibu wa kuisimamia serikali, kamati teule za Bunge huundwa pale serikali inapofanya madudu, taarifa ya kamati teule ya Bunge ni taarifa ya mhimili wa Bunge na sio taarifa ya yule yule aliyefanya madudu, yaani serikali, na inapaswa kuwasilishwa Bungeni, na mapendekezo yake, kisha waheshimiwa wabunge waijadili na kuyakubali mapendekezo, kuyapunguza, au kuyaboresha, kisha linatolewa Azimio la Bunge ambalo sasa ndilo linalopaswa kuwasilishwa serikalini kwa utekelezaji wa lazima. Kitendo cha taarifa ya Kamati Teule ya Bunge kuwasilishwa kwa rais Magufuli, ni kituko cha mwaka!.

Kwa mujibu wa Kanuni za Kudumu za Bunge, Taarifa ya Kamati Teule ya Bunge inapaswa kuwasilishwa Bungeni na kujadiliwa
122.-(1) Kamati Teule itatoa taarifa Bungeni kuhusu maoni na uchunguzi wake pamoja na kumbukumbu za ushahidi uliopokelewa na vilevile inaweza kutoa taarifa maalumu juu ya mambo yoyote ambayo itaona yanafaa kuwasilishwa Bungeni. (2) Taarifa ya Kamati Teule itawasilishwa Bungeni na Mwenyekiti. (3) Iwapo baada ya hoja kutolewa, Bunge litaamua kujadili taarifa hiyo, hoja itakayotolewa Bungeni itakuwa ni kwa madhumuni ya kuliomba Bunge likubali mapendekezo yaliyomo katika taarifa hiyo. (4) Bunge linaweza kuamua vinginevyo kwa kutumia utaratibu wa kubadilisha hoja ambao umeelezwa katika Kanuni ya 57 ya Kanuni hizi. (5) Katibu wa Kamati Teule ataweka kumbukumbu zinazoonesha majina ya Wajumbe waliohudhuria mikutano ya Kamati na maamuzi yaliyofanyika.

Kwa kumbukumbu zangu, please correct me if I'm wrong, Taarifa iliwasilishwa kwa mujibu wa kanuni 122 (2), baada ya kuwasilishwa, ilibidi kanuni 122 (3) ifuatwe kwa Bunge kujadili, hapa linazungumzwa Bunge ndilo lililopaswa kuamua kujadili au la na sio spika kuamua!, kumbukeni Spika ni Spika na Bunge ni Bunge, Spika hawezi kujigeuza yeye ndio Bunge na kuzuia taarifa ya kamati teule isijadiliwe Bungeni!. Spika alipaswa kuliuliza Bunge lijadili, na kama kama kuna hoja kuwa taarifa hiyo isijadiliwe, then ingetumika kanuni ya 122(4) ambayo inaliruhusu Bunge kutojadili na kuibadilisha hoja.

Kama Spika ametumia kanuni 122 (4) ya Bunge lisijadili, then uamuzi huu ungefuata kanuni ya 57 ya kubadilisha hoja kwa kuibadili jina isiitwe tena kuwa Taarifa ya Kamati Teule ya Bunge, bali ibadilishwe hoja iitwe Taarifa ya Kamati ya Rais, na itawasilishwa kwa rais, na sio tena Taarifa ya aKamati Teule ya Bunge, kwa sababu taarifa ya Kamati Teule inawasilishwa na kujadiliwa na Bunge, taarifa ya rais ndio inakabidhiwa kwa rais.

Ili hili liweze kufanyika, ingebidi kanuni hii ifuatwe
57.-(1) Hoja ikishatolewa ili iamuliwe inaweza kubadilishwa kwa:- (a) kuondoa maneno fulani kwa ajili ya kuingiza maneno mengine; (b) kuondoa maneno fulani bila kuongeza mengine; au (c) kuingiza au kuongeza maneno mapya.

Sina kumbukumbu ya hili kufanyika na sikusikia likiripotiwa na media yoyote!. Kwa vileBunge letu linafanya baadhi ya mambo kwa kujifungia, kama hili lilifanyika lakini halikuripotiwa, then taarifa iliyowasilishwa kwa rais, ilipaswa iwe na jina jingine!, Tangulini rais ambaye sio mbunge akapokea taarifa ya Kamati Teule ya Bunge badala ya kupelekewa Azimio la Bunge?.

Wabunge wetu walilikubalije hili la Spika kujigeuza Bunge na kuamua kwa niaba ya Wabunge wote, huku waheshimiwa Wabunge wetu wakiwa wanaangalia tuu, like worshipers waiting for their priest, longed to hear him pray!, play their minds away?!. Kama Spika ndiye mwenye uwezo wa kuwafahamu wabunge wote, their abilities and capabilities, halafu Spika huyo anapiga simu kwa rais Magufuli kumuuliza nimteue nani?, "Mh spika, nakumbuka ulinipigia simu ukaniuliza utachagua nani?, nikakujibu Mungu atakuongoza", then huku ni kujipendekeza gani?, huku ni zaidi ya kujipendekeza!, ni kujikomba!. (rais Magufuli naye huyu bana!, hana siri, ametoa siri ya Spika, kumpigia simu rais, kumuuliza amteue nani kuongoza kamati Teule ya Bunge?!, what sort of speaker do we have?!). Sasa kama Spika anajikomba kwa rais hadi kumpelekea Ripoti ya Kamati Teule badala ya kumpelekea Azimio la Bunge!. Kiukweli nimemkumbuka sana Spika Sitta (RIP), Mungu amuweke mahali pema peponi. Kwa maoni yangu binafsi, napendekeza, Mhe. Job Ndugai ndie awe spika wetu wa mwisho asiye mwanasheria!.

Tukisema Bunge letu ni Bunge la ajabu, tutakuwa tunalionea?, tukisema Wabunge wetu ni wabunge wa ajabu, tutakuwa tunawaonea?!. Nimepitia kanuni za Bunge, sikufanikiwa kuona popote ni kanuni ipi ilitumika kuiwasilisha ripoti ya Kamati Teule ya Bunge kwa Mhe. rais!.

NB. Bunge pia linayo mamlaka ya kutengua kanuni yoyote ili kufanya jambo lolote lililo inje ya kanuni, sikumbuki kama kulifanyika utenguaji wowote wa kanuni, kuruhusu ripoti ya Kamati Teule ya Bunge kuwasilishwa kwa rais bila kujadiliwa na Bunge na kutolewa Azimio la Bunge, kama kuna anayejua kuwa kanuni zilitenguliwa, anijulishe, ili nilifute bandiko hili.

Kama Mhimili wa Bunge letu tukufu linaweza kufanya mambo shaghalabaghala, Mhimili wa Mahakama ndio ndio uko chini ya Kaimu Jaji Mkuu ambaye mpaka leo ni miezi 9 anakaimu na mwisho wa kukaimu ni miezi 9!, Mkuu wa The Executive ndio huyu anayaikanyaga katiba aliyeapa kuilinda, kuitetea na kuitekeleza, tutegemee nini?!.

Mungu Ibariki Tanzania.
Wasalaam

Paskali
Rejea
Wito: Wabunge Badilini Kanuni Kuondoa Udikteta wa Spika/N.Spika ...
Maamuzi ya Serikali ni Shaghala Baghala! No Coordination! We Need ...


 
Wanabodi,
Nchi inaundwa kwa mihimili mitatu rasmi , The Executive, The Legislature na The Judiciary, na pia kuna mhimili wa nne usio rasmi, the 4th Protocal, The Press.

Hii mihimili yote mitatu, kila mmoja una mamlaka yake "powers" ambayo hayapaswi kuingiliwa na mamlaka nyingine, na inafanya kazi kwa uhuru "independent",
Si kwa utawala huu,awamu ya tano ni mhimili mmoja tu sababu ndio "unaotafuta pesa na kulipa mihimili mingine ili ifanye kazi zake" So mahakama,bunge hawawezi kwenda kinyume na mfadhili wao unless they go rogue.
 
Wanabodi,
Nchi inaundwa kwa mihimili mitatu rasmi , The Executive, The Legislature na The Judiciary, na pia kuna mhimili wa nne usio rasmi, the 4th Protocal, The Press.

Hii mihimili yote mitatu, kila mmoja una mamlaka yake "powers" ambayo hayapaswi kuingiliwa na mamlaka nyingine, na inafanya kazi kwa uhuru "independent",
kwa maandiko sawa lakini kihualisia hapana kuna muhimili uko juu ya mingine ule unaotoa bajeti,by Mh

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wanabodi,
Nchi inaundwa kwa mihimili mitatu rasmi , The Executive, The Legislature na The Judiciary, na pia kuna mhimili wa nne usio rasmi, the 4th Protocal, The Press.

Hii mihimili yote mitatu, kila mmoja una mamlaka yake "powers" ambayo hayapaswi kuingiliwa na mamlaka nyingine, na inafanya kazi kwa uhuru "independent",
Pascal usipotoke, mihimili ya dola imejengwa ktk msingi wa utatu mtakatifu na kwa maana hiyo kuna mhimili mmoja ulio mkuu. Hii mihimili miwili inayobaki yote inapigania upili kwa sababu ya maslahi ila kiukweli bunge linapaswa kuwa ' mwana' nayo mahakama ndiyo ' roho takatifu' kwa maana inapaswa kusimama katika haki. Ahsante!
 
Hili swali si ulishaliuliza kipindi kile cha kwanza kwanza kabisa ukaambiwa kuna muhimili umejichimbia zaidi ya mingine mkuu? Unataka risasi wewe.
 
Sorry figure limeteguka kabla chakula hakijaiva hivyo kinarudi jikoni kitapakuliwa tena.
P

Naomba nikupe nukuu hii yaweza kukubadili kidogo.

Ila kwa sasa RC Dar ndiyo kila kitu,hata akisema UA wachagga wote itafanyika chini ya Nataka za mhimili uliojikita zaidi.
 

Attachments

  • DJLZjFSVYAEzgc3.jpg
    DJLZjFSVYAEzgc3.jpg
    41.5 KB · Views: 70
Pascal usipotoke, mihimili ya dola imejengwa ktk msingi wa utatu mtakatifu na kwa maana hiyo kuna mhimili mmoja ulio mkuu. Hii mihimili miwili inayobaki yote inapigania upili kwa sababu ya maslahi ila kiukweli bunge linapaswa kuwa ' mwana' nayo mahakama ndiyo ' roho takatifu' kwa maana inapaswa kusimama katika haki. Ahsante!

Utatu mtakatifu ni nafsi tatu nazo ni sawa ila kazi ni tofauti, kilichokosekana kwetu ni nafsi moja kuwa na power kuliko others.
 
Wanabodi,
Nchi inaundwa kwa mihimili mitatu rasmi , The Executive, The Legislature na The Judiciary, na pia kuna mhimili wa nne usio rasmi, the 4th Protocal, The Press.

Hii mihimili yote mitatu, kila mmoja una mamlaka yake "powers" ambayo hayapaswi kuingiliwa na mamlaka nyingine, na inafanya kazi kwa uhuru "independent",
Sielewi unaandika nini hapa Pasco,
Wewe ulikuwepo live pale ukumbini siku ile mpaka ukaitwa "Njaa" kama tafsiri ya Mayalla,
Pale ndipo dhana mpya ya "Mhimili Chimbifu Zaidi" ilipowekwa wazi,
 
Back
Top Bottom