Wabunge wenye tuhuma wachunguzwe

Lupyeee

JF-Expert Member
Jun 28, 2016
2,683
2,820
Iko wazi kuwa bunge ni mhimili unaojitegemea na ni sehemu ambayo sheria za nchi hutungwa.

Kwa umuhimu huo, si busara kwa wabunge kuwa na hata tone la tuhuma zinazoenda kinyume na maadili ya Tanzania.

Hivi karibuni zimetolewa tuhuma nzito zikielekezwa kwa baadhi ya wabunge wetu tuliowaamini na kuwachagua kuwa wanahusika na mitandao ya wauza madawa ya kulevya!!

Hizi siyo tuhuma za kuachwa zipite hivi hivi, ni lazima zichunguzwe na ikibainika hao wabunge wanahusika kweli na kuuza madawa ya kulevya wafukuzwe bungeni mara moja na ikiwezekana wavuliwe ubunge ili iwe fundisho kwa wengine..
Inasikitisha sana kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani bungeni kuwa na tuhuma nzito kama hizi alafu akaachwa hivihivi tu.
 
Tumalize la vyeti kwanza halafu hili lako lifuate. La vyeti sasa linaanza kuwa ndaza wakati wenzetu wameshapiga hatua ya halichachi.
 
Iko wazi kuwa bunge ni mhimili unaojitegemea na ni sehemu ambayo sheria za nchi hutungwa.

Kwa umuhimu huo, si busara kwa wabunge kuwa na hata tone la tuhuma zinazoenda kinyume na maadili ya Tanzania.

Hivi karibuni zimetolewa tuhuma nzito zikielekezwa kwa baadhi ya wabunge wetu tuliowaamini na kuwachagua kuwa wanahusika na mitandao ya wauza madawa ya kulevya!!

Hizi siyo tuhuma za kuachwa zipite hivi hivi, ni lazima zichunguzwe na ikibainika hao wabunge wanahusika kweli na kuuza madawa ya kulevya wafukuzwe bungeni mara moja na ikiwezekana wavuliwe ubunge ili iwe fundisho kwa wengine..
Inasikitisha sana kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani bungeni kuwa na tuhuma nzito kama hizi alafu akaachwa hivihivi tu.
Waliofoji vyeti tuendelee kuwalinda eeee? kuwa mwana lumumba ina hitaji PhD ya utahira ili kutetea hoja ya kipuuzi
 
Vipi RC mwenye cheti feki? Naona tuanzie hapo kwanza. Wana Dar es Salaam wamechoka kutawaliwa na mhitimu wa darasa la saba.
 
Muuza madawa ya kulevya hawezi kujificha nyuma ya vyeti feki.

Muuza madawa ananyongwa
 
Iko wazi kuwa serikali ni mhimili unaojitegemea

Kwa umuhimu huo, si busara kwa wakuu wa mikoa kuwa na hata tone la tuhuma zinazoenda kinyume na maadili ya Tanzania.

Hivi karibuni zimetolewa tuhuma nzito zikielekezwa kwa mkuu wetu wa mkoa tuliomwaamini na kuwachagua kuwa wanahusika na kughushi vyeti!!

Hizi siyo tuhuma za kuachwa zipite hivi hivi, ni lazima zichunguzwe na ikibainika wanahusika kweli na kufoji vyeti
wafukuzwe kazi mara moja na ikiwezekana wavuliwe nyadhifa zao za ukuu wa mkoa ili iwe fundisho kwa wengine..
Inasikitisha sana kiongozi wa mkoa na jiji kubwa dar es salaam kuwa na tuhuma nzito kama hizi alafu akaachwa hivihivi tu.
 
tz bwana wananchi wake wanapenda kwenda na mipango mingi ndo maana tunashindwa kufikia uchumi wa kati

kwa sasa tunapaswa kumaliza uhakiki wa vyeti kwanza kabla ya tuhuma za kuhisiwa na mtu teana ambae anatumia cheti cha mtu
 
Iko wazi kuwa bunge ni mhimili unaojitegemea na ni sehemu ambayo sheria za nchi hutungwa.

Kwa umuhimu huo, si busara kwa wabunge kuwa na hata tone la tuhuma zinazoenda kinyume na maadili ya Tanzania.

Hivi karibuni zimetolewa tuhuma nzito zikielekezwa kwa baadhi ya wabunge wetu tuliowaamini na kuwachagua kuwa wanahusika na mitandao ya wauza madawa ya kulevya!!

Hizi siyo tuhuma za kuachwa zipite hivi hivi, ni lazima zichunguzwe na ikibainika hao wabunge wanahusika kweli na kuuza madawa ya kulevya wafukuzwe bungeni mara moja na ikiwezekana wavuliwe ubunge ili iwe fundisho kwa wengine..
Inasikitisha sana kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani bungeni kuwa na tuhuma nzito kama hizi alafu akaachwa hivihivi tu.
Tatizo humu tunajibizana na watu tusiojua uwezo wao wa kufikiri. Yaani ile karatasi aliyokuwa nayo bashite imeandikwa kwa mkono na mwandiko wenyewe tatizo ndo unataka waliotajwa wawajibike. Yaani anatoa povu kuwataja akina Wema, Chid, TID, Vannessa na wengineo then mnaona kafanya kazi ya maana. Kuwataja kina Gwajima na hakuna kilichopatikana ndo mnatoa mishipa kusifia upumbavu huo, vita ya madawa ya kulevya inapiganwa kwa mikakati ya kibashite itafika wapi?Kazi ipo ngumu sana kama Wabongo wenyewe ndo wa aina yako. Weka vyeti
 
Muuza madawa ya kulevya hawezi kujificha nyuma ya vyeti feki.

Muuza madawa ananyongwa
Yaani muuza madawa unampa siku 3 aje kituoni hata kama anauza na alikuwa nayo ndani utayapataje?Utampelekaje mahakani bila evidence?Mahakimu wote wanatoa hukumu kwa evidence sio kwa maneno ya mitaani. Dogo anapenda popularity yeye angechukua hiyo orodha akavipatia vyombo vya uchunguzi kimya kimya ili ushahidi upatikane. Au alikuwa anaharibu ushahidi ili wahusika kamili wajipange, hana mikakati na hatofanikiwa.
 
Mbowe alipiga dozi ya colgate na chumvi ili ngada isionekane kwenye mkojo.

Lakini atapatikana tu
 
Wenyewe wangefanya uchunguzi kimya kimya walau wapate japo ushahidi kidogo, sasa inaonekana ni majungu na kusingizia watu. Hii inajenga chuki, uhasama na mpasuko ndani ya jamii. Lakini pia imevuruga maana nzima ya vita dhidi ya madawa ya kulevya, so far hakuna dealer mkubwa hata mmoja aliyekamatwa na watarudi tena kwa kasi ya ajabu
 
Ushahidi ni kupungua kwa mateja pale kinondoni baada ya mwenyekiti kutajwa
 
Back
Top Bottom