Wabunge wa namna hii
1. Kamwe hawawezi kuwa na matatizo na spika.
2. Hawawezi kuitishiwa kikao cha kamati ya nidhamu.
3. Wapiga kura wao hawana shida na nini wanafanya bungeni
Hawapingi juhudi za maendeleo ambao serikali yetu sikivu inafanya.
na hiyo glass sijui ni ya changa'aa maana wabunge wa ccm hawaeleweki kabisa.Exactly mkuu,
Hapa akianza kuota kwa sauti, neno la kwanza litakuwa "Chadema..."
Sio ajabu kama unavyofikiria. Unaweza kutazama TV,ukasinzia bila kufahamu.[na ukaiacha TV inaendelea]. Unaweza kusoma,ghafla ukalala. It is caused by concentration on some difficult to understand thing.
Ndio 'nidhamu' yenyewe. Unawezaje ku'concentrate' bila kuwa na 'nidhamu'?Sio ajabu kama unavyofikiria. Unaweza kutazama TV,ukasinzia bila kufahamu.[na ukaiacha TV inaendelea]. Unaweza kusoma,ghafla ukalala. It is caused by concentration on some difficult to understand thing.
Umenipata vizuri mkuu.Point ya mchami nadhani iko clear kwa wengi.
Bunge letu limetoka katika mstari wake sahihi, ambao ni kuisimamia serikali, limeiruhusu serikali isimamie bunge, kwa kuweka spika anayeamrishwa na muhimili wa utawala.
Wabunge wote wanaoonekana wanaibana serikali, hao wanaambiwa hawana nidhamu.
Lakini wabunge wanaokosa kuhudhuria, wanaolala bungeni, wanaochelewa, wasiotoa mchango wowote kuisaidia serikali kuendesha shughuli zake, hao ndio wabunge wema. Hawa wanaishi kwa raha bungeni, na posho zao zina uhakika.
Hao hawatasomewa kanuni kamwe.
Hao hawataitishiwa kikao cha kamati ya nidhamu ya bunge.
Hao hawatasimamishwa kuhudhuria vikao vya bunge.
Wananchi ni juu yetu kusema kama pesa yetu tunayokatwa kwenye kodi, inayotumika kuwalipa hawa wabunge mpaka wanakuwa tajiri kupindukia inatumika kihalali pale wabunge wetu wanapolala? Au kutoroka vikao? Au kuchelewa?
Asante mchami kwa kutuwekea tafakari, ambayo umeiweka kwa namna ya mzaha, lakini inazungumza kitu cha msingi.
Kuwa mbunge wa ccm ni raha sana, unakula posho bila jasho. Halafu sijui maendeleo ya nchi yataletwa na nani. Wakati wao wamelaa wapinzani wako macho kuhakikisha hakuna jambo linalopitishwa kiholela, halafu wanaitwa vinara wa fujo.
Hii ndo bongo bana, lolote waweza fanya popote kama una nafasi ya kufanya hivyo bila kuulizwa
Haha ha haa, walikeshea wapiiii.
Alafu ikifika ile ya nawahoji, wote watasema ndiyoooooo kwa kitu ambacho hawajakisikia hata.
Long way to go