Mwanaukweli
JF-Expert Member
- May 18, 2007
- 4,789
- 1,732
Wabunge wa namna hii
1. Kamwe hawawezi kuwa na matatizo na spika.
2. Hawawezi kuitishiwa kikao cha kamati ya nidhamu.
3. Wapiga kura wao hawana shida na nini wanafanya bungeni
Hawapingi juhudi za maendeleo ambao serikali yetu sikivu inafanya.
1. Kamwe hawawezi kuwa na matatizo na spika.
2. Hawawezi kuitishiwa kikao cha kamati ya nidhamu.
3. Wapiga kura wao hawana shida na nini wanafanya bungeni
Hawapingi juhudi za maendeleo ambao serikali yetu sikivu inafanya.
Point ya mchami nadhani iko clear kwa wengi.
Bunge letu limetoka katika mstari wake sahihi, ambao ni kuisimamia serikali, limeiruhusu serikali isimamie bunge, kwa kuweka spika anayeamrishwa na muhimili wa utawala.
Wabunge wote wanaoonekana wanaibana serikali, hao wanaambiwa hawana nidhamu.
Lakini wabunge wanaokosa kuhudhuria, wanaolala bungeni, wanaochelewa, wasiotoa mchango wowote kuisaidia serikali kuendesha shughuli zake, hao ndio wabunge wema. Hawa wanaishi kwa raha bungeni, na posho zao zina uhakika.
Hao hawatasomewa kanuni kamwe.
Hao hawataitishiwa kikao cha kamati ya nidhamu ya bunge.
Hao hawatasimamishwa kuhudhuria vikao vya bunge.
Wananchi ni juu yetu kusema kama pesa yetu tunayokatwa kwenye kodi, inayotumika kuwalipa hawa wabunge mpaka wanakuwa tajiri kupindukia inatumika kihalali pale wabunge wetu wanapolala? Au kutoroka vikao? Au kuchelewa?
Asante mchami kwa kutuwekea tafakari, ambayo umeiweka kwa namna ya mzaha, lakini inazungumza kitu cha msingi.