Wabunge wengi wanasahu majukumu yao

CHIBA One

JF-Expert Member
Nov 16, 2018
560
2,087
Imekuwa ni desturi ya wabunge wengi kuahidi na kufanya mambo ambayo si miongoni mwa majukumu ya msingi kwa mbunge kuyafanya, na kusahau yale ya msingi waliyotumwa kuyafanya kama wawakilishi wa jimbo na wananchi.

Mbunge ananunua baiskeli? Nani aliwaambia hili ni jukumu la mbunge? Kununua baiskeli na kuzigawa kwa baadhi ya wananchi. Unawezaje kupima ubora wa huduma za msingi kwa kugawa baiskeli? Unatumia pesa za jimbo ama za mfukoni kwako?

Kanga, Sukari, viberiti, kama unataka kugawa vitu hivi kama raia yoyote mwingine kama tendo la "kujitolea na upendo kwa wengine" Gawa lakini usije kujinadi eti "niligawa viberiti kijiji kizima. Hapo tunahesabu kama uligawa tu kama raia wa kawaida na sio sifa za kukupa uwakilishi. Mbunge hana jukumu la kugawa pipi shekhe.

Niliwasaidia vijana wawili Wasitapeliwe pesa zao baada ya kufika dar. Unakuta mbunge mzima anaongea ujinga kama huu kwenye mkutano. So what? Unataka ubunge kwa sababu cheap kama hizi? Wewe ni raia mwema tu uliyetimiza majukumu yako.

Nilihudhuria misiba na kugawa baiskeli kwa walemavu, nimesomesha watoto 30 kwa elimu ya sekondari. Tunashukuru kwa kufanya matendo mema. Lakini bado hizi sio sera zinazolenga muktadha wa jamii kunufaika na utumishi wako. Hata makanisa na misikiti yanachangia watoto ada.

JUKUMU LA MSINGI la mbunge ni kuishauri serikali na kuomba utatuzi wa changamoto jimboni kwako. Kama huna maji isumbue sana serikali, pigania sana barabara na huduma za afya, elimu na masoko, umeme na kuleta ahueni kwa kina mama na vijana wajasiriamali kwa kuwatengenezea mazingira rafiki ya biashara.

Sitaki niwape siri za kampeni lakini Mnayojivunia kufanya si Mambo ya kujigamba kwenye mikutano eti "Nilitoa magari ya kubebea wafiwa" Tatizo lenu hampendi hata kujisomea miongozo ya Kazi zenu. Kapigeni tena madawati Mkishangilia kila jambo.

Wenu Hohe Hahe wa Nyasa.
 
Back
Top Bottom