wabunge wawe na mpangokazi na wauweke hadharani

kirengased

JF-Expert Member
Jan 10, 2016
6,260
6,992
Asalaam, nadhani ni vema wabunge wetu kupitia kwa makatibu wao watakiwe kisheria kutengeneza mpango kazi wa kilamwaka kwa kila mbunge jimboni mwake na kuubandika hadharani.
Kumekuwa na tabia ya wabunge kuahidi mambo mengi wakati wa kampeni,wakisha chaguliwa hawaonekani jimboni wao ni kula raha daslam. Haifai mbunge kukaa tu anatafuta vijembe vya kumpa umaarufu vikao vya bunge vitapoanza. Mwingine unaambiwa eti yukobusy anasoma,kusoma ndo usifanye lolote jimboni?
Ingefaa wabandike mpango kazi katika ofisi zao na kila baada ya miez 4 waeleze walichofanikisha. Hawawatu tunawalipa vizuri sana lakini wamegeuka kuwa wanaahidi vitu wanavyojua hawavimudu mwisho ni blahblah tu.
Tunataka siasa na kazi sio porojo tuu.
 
Kuna tofauti gani kati ya mwakilishi na mtu alieajiriwa kama mtendaji katika majukumu ya serikari za mitaa? Haya ndio mambo wabunge kudhani wanamamlaka ya kuwapa amri wafanya kazi wa serikari wao wenyewe kama Magufuli alivyo na mamlaka hayo kikatiba.

Kazi ya mmbunge ni kuisimamia serikari kwa kuangalia sera zao zinavyofanyika jimboni, kuelezea changamoto zao na pale kwenye mapungufu kama mwakilishi anatakiwa arudi kwa mabosi wao wachukue hatua sio yeye.
 
Mfano Lema wa Arusha aliahidi hospitali lakini mpakaleo hamna hâta kituo cha afya,sio yeye tuu,wapo wengi wenye ahadi hewa. Hii inafanya watu tuone ubunge ni usanii wa kucheza na akili za watu
 
Back
Top Bottom