Wabunge wataka ofisi za kisasa

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,789
288,029
Wabunge wataka ofisi za kisasa

na Salehe Mohamed
Tanzania Daima~Sauti ya Watu

WABUNGE wameitaka serikali kuwajengea ofisi zenye hadhi katika majimbo yao pamoja na kuwaweka wataalamu wa fani mbalimbali ambao watawasaidia kuratibu shughuli zao.

Wabunge walitoa kauli hiyo juzi walipokuwa wakihitimisha semina inayohusu mwongozo wa kutayarisha mipango na bajeti ya serikali kwa kipindi cha mwaka 2008/09-2010/2011 iliyoandaliwa na Wizara ya Mipango na Fedha.

Mbunge wa Dole, Juma Selemani N’hunga (CCM), alisema ni aibu kwa wabunge kuendelea kutegemea ofisi za wakuu wa wilaya ambazo hupewa ofisi moja, huku ikiwa haina vifaa vya kufanyia kazi vinavyotakiwa na wabunge.

Alisema wabunge ni watu muhimu na wanapaswa kuwa na ofisi zenye vifaa vya kisasa ambavyo vitawarahisishia utendaji kazi wao tofauti na ilivyo hivi sasa ambapo wanatumia vifaa duni visivyokidhi mabadiliko ya teknolojia ya kisasa.

“Kule Marekani kila jimbo lina ofisi yake na kila mbunge ana wasaidizi na wataalamu wasiopungua 15, sasa angalau na sisi tuwe na wataalamu na wasaidizi hao hata kama hawatafikia kama wale wa Marekani,” alisema N’hunga.

Naye Mbunge wa Iramba Mashariki, Mgana Msindai (CCM), alisema ni vema mazingira ya ufanyaji kazi wabunge yakaangaliwa, kwani gharama za maisha zimepanda huku bajeti kwa ajili ya Bunge ikiwa kidogo.

Alisema endapo wabunge wataboreshewa mazingira ya kufanya kazi itawasaidia kuwafikia kwa urahisi wananchi wao sambamba na kurahisisha mawasiliano na baadhi ya viongozi wa serikali.

“Nina uhakika kama mambo yakiboreshwa tunaweza kufanya kazi vizuri na kuwafikia wapiga kura wetu kwa urahisi zaidi,” alisema Msindai.

Aidha, Mbunge wa Lulindi, Suleiman Kumchaya (CCM), alisema mambo ya uboreshaji wa uchumi wa nchi ni lazima uwashirikishe wananchi na ikiwezekana kuwe na benki ambazo zitakuwa zikitoa mikopo kwa Watanzania pekee.

Alisema kwa muda mrefu serikali imekuwa ikiimba wimbo wa kuwa kilimo ni uti wa mgongo, huku ikiwa haiweki mkazo unaotakiwa, hivyo kuchangia kuchelewa kwa maendeleo katika sekta husika.

“Utaratibu wa kusema kila siku kuwa kilimo ni uti wa mgongo halafu hatuweki mipango thabiti ya kukinyanyua tunapaswa tuachane nao,” alisema Kumchanya.

Aidha, wabunge hao waliitaka serikali kuweka utaratibu maalamu ambao utakuwa ukiratibu mipango ya maendeleo na kutoa tathimini ya mafanikio au kushindwa kwake kila baada ya muda fulani.Maoni ya Wasomaji
Maoni yanayotolewa na wasomaji wa safu hii ni ya kwao na sio maoni ya kampuni ya Freemedia Ltd. Aidha sio maoni ya mtunzi au mwandishi wa habari au makala husika hapo juu. Maoni haya hayajahakikiwa wala kuafikiwa na kampuni ya Freemedia Ltd.
Maoni 15 yameshatolewa. (Nawe toa maoni yako!)
acheni upuuzi kabisa mjengewe ofisi kwa hela kutoka wapi.hapo ni tanzania na siyo marakani .wenzetu ni matajiri.kwanza mi nataka wabunge wote wakopeshe magari ya bei raisi suzuki zinatosha kabisa.mshara wako milioni moja na nusu ,ukienda kutembea dodoma kwa siku laki moja. mwalimu mshara wake laki kwa mwezi.hivi hamumuogepi mungu nyiye watu wa ccm.

na jonj perege, kanani, - 29.03.08 @ 10:23 | #3964

Kanani, we angalia ni wabunge wa chama gani wanataka hayo alafu utapapta jibu. Hii mijitu inafikiria anasa tu, eti wawafikie wananchi zaidi. Ni lini waliwafikia hat kwa kidogo? Mtu na akili zake anatoa mfano wa marekani,mbona uwajibishwaji wa mafisadi hamtolei mfano wa marekani? Mbona elimu, kilimo,afya, kima cha chini,haki na uhuru hamtolei mfano wa marekani? Yaani inapokuja kuongezewa marupurupu na kujengewa ofisi ndo mnajifananisha na Marekani? Mnataka kuishi kama wasemavyo vijiweni "Bongo- New York" Ebu acheni upuuzi watumikieni wananchi.

na kukuz, singapore, - 29.03.08 @ 10:36 | #3970

kwa hyo wabunge wa ccm wanataka kutwambia hawawafikii wananchi kwa ukaribu sababu hawana ofisi za kisasa na wasaidizi lukuki,naomba wananchi wa wabunge hao wasiwachague 2010 mana hawana la kutetea kwa wananchi wao zaidi ya kutaka ofisi za kisasa wkt kazi zao haziendani na usasa,mambo yao hufanya kizamani sana,mi ningewaomba wafanye kazi kisasa kwanza,then wananchi wakikubali ndio wajengewe hizo ofisi za kisasa,hivi wabunge hawana hata aibu kufananisha na marekani.

na mstari wa mbele, calif/usa, - 29.03.08 @ 08:04 | #3976

Wabunge kazi yenu ni kuwakilisha wananchi,Ofisi zilizopo zinatosha.Nchi yetu ni masikini,umasikini uliosababishwa na wabunge haohao kwa tabia yao ya kulindana huku wakipitisha nakushabikia mikataba ya ovyo hata ile iliyosainiwa nje ya nchi kwa mamantilie.Mnadai maslahi zaidi, ofisi na watumishi wake,je' zahanati zetu zina majengo yakutosha zikiwemo nyumba za wataalamu wake?Kuna dawa za kutosha?.Shule zetu zina madarasa na nyumba za waalimu za kutosha?Kuna maktaba na vitabu vyake?maabara na vifaa vyake?.Nyie ni sauti ya umma.Daini vitu kwa maslahi ya wananchi wenu kabla umma haujawahama.Watendeeni haki wananchi wenu,siyo kuangalia maslahi binafsi.Bado asubuhi mno kwa wabunge wetu kujilinganisha na wabunge wa Marekani.ONEENI HURUMA NCHI YENU."MTU MWEMA HUACHA JINA".

na Yusuph , Dodoma, - 29.03.08 @ 08:05 | #3977

Waheshimiwa wabunge Watoto wa wakulima wanakaa chini madarsani hawana viti. Mnadai eti ofisi za kisasa. Hata za kizamani hawa watoto wa wakulima hawana. Angalieni wabunge watoto hawa wasije laani nchi. Hivi shule za kata zina waalimu? Na kama wapo wanatosha? Waheshimiwa kama hamfanyi kazi kibinafsi na kujipendelea na hila kwa nini mnapozunguka kwa kampeni msiwe mansema maneno haya? Kwamba pindi mkiingia ofisini mtadai kuongezwa marupurupu kabla hamjaanza hata kufanya kazi, mtadai maofisi ya kisasa na kukopeshwa magari ya kifahari wakati wananchi wanapigika. Oneeni huruma Tanzania. Ni dhahiri wabunge wetu mnalipwa hela nyingi tena hamjawahi kucheleweshewa mafao yenu hata mara moja. Waalimu posho zao kiasi kidogo cha tangu 2005 na kuendelea hawajalipwa. Nyie mnasema mnataka kuongezewa hata mishahara. Hongereni kwa hayo ila hamkuchaguliwa kwa ajili ya hayo. Mmejenga madarasa ndio na hospitali sawa lakini wabunge hospitali sio majengo ni madaktari na madawa, shule ni waalimu wanafunzi na nyenzo za kufundishia, wapeni waalimu ofisi za kisasa na vitendea kazi vy kisasa walete wasomi wa kuikomboa Tanzania kiuchumi. Waliopo sasa wameshindwa kwa kugeuka matapeli na mafisadi

na Godfrey, Dar es Salaam, - 29.03.08 @ 08:31 | #3982

Maslahi yao pamoja na mikopo yao inatosha kabisa kama wanataka ofisi kama za Marekani, Posho si wanazo? na mikopo wanapewa tena first priorit.. basi kama wao wana uchungu WACHANGISHANE WAJIJENGEE OFISI HIZO kama wananchi tunavyo changishana kujenga shule.Nchi ina matatizo kibao, HALI YA UCHUMI IMEKUWA MBAYA VIPATO DUNI KWA WANANCHI WENGI. MIKATABA MIBOVU NA MENGINEYO MENGI, WAO WANADAI WAJENGEWE OFISI, HAMIENI MAREKANI KAMA BALALI HUKO MTAKUTA KILA KITU KIKO SAFI. Si ndi kazi yenu mafisadi TUACHIENI NAFASI TUCHAGUE WABUNGE WANAOTUFAA. BADO KIDOGO TU TENA MTASEMA MISHAHARA NA POSHO HAZIWATOSHI.RUDISHENI PESA MLIZOIBA TUJENGE OFISI....

na William , MBY, - 29.03.08 @ 08:38 | #3983

Tatizo kubwa linaloipata serikali ni la kijitakia.Serikali ilipaswa kuweka ukomo wa mbunge usizidi vipindi viwili kama ilivyo kwa Rais ili kupata wabunge wenye mawazo tofauti.Swala la ubunge ni la kisiasa.Ukiangalia mbunge anateuliwa na chama cha siasa na akishakuwa mbunge anasimamia ilani ya chama chake lakini wakati huo atataka kila kitu afanyiwe na serikali kuu.Serikali imeshajenga ofisi kila kata ambazo yeye amapaswa kuhudumia jimbo lake kwa kushirikiana na watendaji wa serikali za mitaa kuhakikisha utekelezaji wa mipango ya maendeleo iliyopitishwa bungeni intekelezwa ipasavyo. Sasa ofisi anayotaka ni ya kufanyia kazi gani ikiwa yeye anatakiwa kupoke ripoti na malalamiko ya watu wa jimbo lake kutoka kwa watendaji hao?Kama wabunge wanaona kuna umuhimu wa ofisi zao binafsi kwa nini wasijenge wenyewe kama ambapo wanajitokeza kuomba kura wenyewe tena hata kwa kununua kura?Ikfika wakati wa uchaguzi utawaona wengine wanakwenda kulala hata makaburini kuwanga ilimradi tu apate ubunge lakini hatujawahi hata siku moja mgombea ubunge akisema akipata ubunge atalazimisha serikali imwangezee posho wala imjengee ofisi.Sasa iweje leo? Kwa sababu hizo kwanzia sasa nitaendesha kampeni kwa wanahabari ili wawaelimishe wananchi kuhoji mbunge yeyote atakayejitokeza kugombea ubunge awaeleze kwanza alipwa jumla ya sh.ngapi kwa maendeleo ya jimbo na amezifanyia nini ili wananchi wapime na kuona kama kweli hela hizo zilifika jimboni na matumizi yake ni sahihi?Hawa wabunge wanajuwa serikali haina ujanja wa kuwabana maana sio mwaajiri wake hivyo wanataka kuiburuza kila kukicha.Na sisi tutawataka watueleze wakishapata ubunge wasipo tekeleza wanayoahidi tuwafanyie nini maana kama tusipo fanya hivyo tutaendelea kuibiwa tu mpaka yesu asheke tena.!.

na kimalando, tz, - 29.03.08 @ 08:56 | #3987

Ule msemo kwamba dalili ya mvua ni mawingu bado una maana. kama mnakumbuka mara tu baada ya uchaguzi, wabunge wetu waliomba wongezewe mishahara ili wafanye kazi vizuri na serikali iliwaongezea kufikia zaidi ya milioni moja,zaidi ya mara kumi ya mshahara wa mwalimu anayefanyakazi saa 8 kwa siku na hana posho. Tanzania kuwa mbunge haina maana kwamba unaenda kuwatumikia wananchi ila inamaanisha ni kupata ajira nzuri zaidi kifedha na pia pia kwenda kulinda maslahi ya yako kibiashara. Mfano mzuri ni wimbi la wasomi, hasa walimu wa vyuo vikuu kuomba likizo bila malipo ili kwenda kutafuta ubunge wakati wa uchaguzi baada ya kuona kipato wakipatacho kama walimu hakilingani na miaka yao waliopoteza shuleni na pia na ugumu wa kazi yao. Wabunge wetu hawana miongozo binafsi kwa ajili ya shughuli za maendeleo ya wananchi na ndiyo maana utakuta wanaropoka hovyo kila siku, mara mishahara haitoshi, mara hatuna ofisi, mara tupatiwe wataalam, why? kwanini? ofisi haziwezi kutembea kwenda kuhamasisha maendeleo kwa wananchi, mmepewa magari ya kifahari ili yawafikishe kwa wanachi badala yake hamuendi na mnatafuta visingizio!!! Acheni uzembe, tanzania siyo kama kenya, siyo kama marekani. Fanyeni kazi kulingana na uwezo wa nchi kifedha ili mkuze uchumi na siyo visingizio. Wabunge mnalidhalilisha bunge, lakini hii hainishangazi sana kwani bunge limejaa mambumbu wengi sana. Wabunge hamna uzalendo na nchi na naomba hiyo tabia yenu ya kutoa visingizio miaka nenda rudi huku mnanua kura ili muendelee kiitia hasara nchiikome. 2008 nadhani wengi wenu mtaibika sana kwani wanachi tumeeanza kukusanya vielelezo vya ufanyaji kazi wenu ili msije kutudanganya. Spika nae unaonekana huna uzalendo wa kutosha kwa nchi, jaingalie nini umewafanyia wananchi wako kama mbunge na nini umeifanyia nchi yako kama spika

na Patrick, Tanzania, - 29.03.08 @ 09:34 | #3995

wamejisahau hawa wana2ona sisi wajinga sana kazi ya mbunge ni kushirikiana na watendaji wa jimbo ili kuleta maendeleo leo wakianza wabunge kesho watafuata madiwani mbunge hana ofisi ofisi yeyote iwe kwa mtendaji, kwa katibu tarafa kwa mwenyekiti wa kitongoji ni ofisi yake inabidi aziboreshe kwa fedha anazopata bungeni ili aweze kuwa karibu na wananchi. eti nao wanajifananisha na marekani wakati hata kenya awagusi

na john, tz, - 29.03.08 @ 09:37 | #3997

jamani waacheni hawa ilikila mtu aone, msiwakatishe tamaa, maana wote wamejisahau, kesho watataka tuwape na ulinzi wa king'ora ili wapatiwe nafasi maalum wapitapo. hawa ni wabunge malimbukeni wasiojali wananchi, zaidi ni maslahi yao, na sio wao tu hata kile kichekeso cha wale wahuni wa znz waliosema wanatak un iwakopeshe magari ,hivi hamuoni miujiza wajumbe wa baraza la wawakilishi hawajui hata un ina kazi gani ,au wanadhani un ni world bank, masikini wa tz tumerogwa na makubwa, hawa jamaa tuwafundishe mwaka 2010 kwa kuongoza ni kuonyesha njia siyo kujikweza. na watu ndio wenye mamalaka ya kuamua nakuweka viongozi na si vynenginevyo

na ikram, tz, - 29.03.08 @ 10:04 | #4006

Mnataka mjengewe ofisi Majimboni huku wengiwenu mnaishi Makoa Makuu ya Mikoa na Jijini Dar.Ofisi za Majimboni atakaa nani au mnataka kudai muwe na makam?
Narejea usemi wa Maisha ya Mwanadam;Huzaliwa analia,huishi akilalamika na hufa hajaridhika,ndo nyie hamuachi kulalamika na mtakufa bila kuridhika.

na Mlali A Mlali, Kahama,Tanzania, - 29.03.08 @ 10:41 | #4016

1 ubunge siyo fani bali ni 'chaguzi' Ya hiyari ya wananchi na kwa hivyo wanawajibika kutokana na mahitaji na uwezo wa wananchi wanaowahudumia.

2 Kwanza walipaswa kulipwa kutokana na mapata yanayotokana na majimbo yao ya chaguzi na siyo na serikali, kwani wao siyo waajiriwa wa serikali bali.Mwajiri wao ni majimbo yao ya uchguzi.

3 Kwa sababu hiyo basi wanalipwa kwa makosa na serikali. na ndiyo maana wakisha chaguliwa hawarudi tena majimboni mwao kuchochea maendeleo.sababu mashahara ,mashangingi nk hayategemei walala hoi waliyo wachagua!!????

4 kwa sababu hiyo basi, wanatetea maslai yao binafsi zaidi kulikoni hali halisi ya walalahoi waliyowachaguo ambao ni!!

5 chanagamoto ni hii:WASILIPWE NA SERIKALI ILA NA PATO LA MJIMBO YA CHAGUZI.PATO LA JIMBO LA CHAGUZI NDIYO IWE KIGEZO HALISI CHA MARUPURUPU YA MBUNGE NA SIYO VINGINEVYO
* MWENYE MACHO HAAMBIWI TAZAMA*

na rk, tanzania, - 29.03.08 @ 10:51 | #4019

MLOLONGO WA UONGOZI KATIKA NCHI NDIYO SABABU KUBWA YA UOZO: WABUNGE NI WATU TULIYO WACHAGUWA WENYEWE.NAFIKIRI WATU HAWA NI MUHIMU HATA KUPITA WAKUU WA WILAYA:HIVYO WATU HAWA WANGEPEWA MADARAKA YA JUU KULIKO WATENDAJI WOWOTE KATIKA MAJIMBO YAO.HIVI WAKUU WA WILAYA/MWENYEVITI WA HALMASHAURI/WAKURUGERENZI WA HALMASHAURI ZA WILAYA/DAO.HUU UTITIRI WA UONGOZI WA NINI? HAPA WANAINCHI KIONGOZI WETU NI MBUNGE .HIVYO BORA HUYU APEWE MADARAKA YA JUU KWA KULIKO WATENDAJI WENGINE WOWOTE

na K:, TZ, - 29.03.08 @ 11:30 | #4026

MLOLONGO WA UONGOZI KATIKA NCHI NDIYO SABABU KUBWA YA UOZO: WABUNGE NI WATU TULIYO WACHAGUWA WENYEWE.NAFIKIRI WATU HAWA NI MUHIMU HATA KUPITA WAKUU WA WILAYA:HIVYO WATU HAWA WANGEPEWA MADARAKA YA JUU KULIKO WATENDAJI WOWOTE KATIKA MAJIMBO YAO.HIVI WAKUU WA WILAYA/MWENYEVITI WA HALMASHAURI/WAKURUGERENZI WA HALMASHAURI ZA WILAYA/DAO.HUU UTITIRI WA UONGOZI WA NINI? HAPA WANAINCHI KIONGOZI WETU NI MBUNGE .HIVYO BORA HUYU APEWE MADARAKA YA JUU KWA KULIKO WATENDAJI WENGINE WOWOTE

na K:, TZ, - 29.03.08 @ 11:30 | #4027


Kuwa na ofisi ni sawa lakini kudai ofisi za kisasa "kama za Marekani" katika hali hii waliyonayo wananchi ni matusi yasiyovumilika.

Wabunge kumbuka kwamba kwenye majimbo yenu mnakotaka ofisi za kisasa watoto wanasomea chini ya miti, walio na vyumba haba hawana madawati, shule hazina walimu, n.k. Sasa kipi ni kipaumbele kwenu?

Msisahau vilevile kwamba Wabunge wote (hasa wa CCM) mnaishi Dar es Salaam, hizo ofisi zitatumika lini na zitatumiwa na nani? Hatujafika mahali pa kufikiria jambo kama hilo.

Tafutia watanzania maendeleo kwanza, hizo ofisi zitapatikana tu. Acha ufisadi, watumikie wananchi ili mpate heshima ya kupewa ofisi hizo.

Mwisho, ni makosa kwa wabunge kuidai serikali ofisi. Nyie mlichaguliwa kwa tiketi ya vyama vyenu sio serikali. Bunge ni nguzo tofauti na serikali.

na Kam, Dar, - 29.03.08 @ 17:46 | #4067
 
Kwa wabunge wa aina hii, tusahau maendeleo bora kwa wote. Hata wakipewa pesa na ofisi kubwa kubwa, hakuna watakachofanya zaidi ya kuwahonga mashabiki zao.

Wataalamu wapo wilayani kama vile wa kilimo, mifugo, walimu, madaktari nk. Lakini hawatumiwi kabisa na wabunge katika kupanga mipango ya maendeleo ya wilaya. Hata wakipewa wasaidizi 15, bado haitasaidia kitu.
 
Kwa wabunge wa aina hii, tusahau maendeleo bora kwa wote. Hata wakipewa pesa na ofisi kubwa kubwa, hakuna watakachofanya zaidi ya kuwahonga mashabiki zao.

Wataalamu wapo wilayani kama vile wa kilimo, mifugo, walimu, madaktari nk. Lakini hawatumiwi kabisa na wabunge katika kupanga mipango ya maendeleo ya wilaya. Hata wakipewa wasaidizi 15, bado haitasaidia kitu.

Hawa jamaa wanapenda sana Dar ama Dodoma .Na zaidi Dar .niliwahi kumkuta Mbunge mmoja kule Mbagala anacheza karata , huyu ni yule wa Geita ambaye hatakiwi kwao nikamuuliza maswali akataka kurusha ngumi .Ana duka na ana angalia mapato.Hata kurudi kijiji hawarudi leo ofisi ndiyo zitafanya nini ? Ulevi wa madaraka huu .
 
Ndugu wabunge ni ukweli ambao haufichiki kwamba mnahitaji ofisi bora na wasaidizi ili muweze kufanya kazi zenu vizuri, lakini kinachonisikitisha ni kwamba hamuelewi ni kwa nini hamna hayo yote mnayoyataka. Pesa zote mumewaachia akina JK, Membe, Karamagi, Richimonduli, RA, IPTL na wawekezaji feki ambao ndio wanakula marupurupu yenu. Hebu washughulikieni ili na nyinyi muwe kama wabunge wa marekani kwa kurudisha haki zenu.

Tunaomba muanze na hili la Arusha ambako vijana wetu wengi wamepoteza maisha halafu Buzwagi, IPTL, EPA bila kusahau Uvundo na harufu inayotoka ATC kwenye mikataba hewa etc.
 
Wabunge wetu ni wasanii tu...wanataka ofisi wakati kai hawafanyi ya kutosha? Ofisi haimfanyi mbunge afanye kazi aidi au pungufu, ni moyo wake na ualendo wake ndo unafanya kazi. Wanaweza kujengewa ofisi halafu wakadai kingine....maybe bigger cars? or maybe more money (kama kawaida yao). Usanii mtupu!!

Wabunge fanyeni kazi zenu!!!!!
 
Back
Top Bottom