ng'adi lawi
JF-Expert Member
- Sep 27, 2014
- 2,956
- 1,114
Uamuzi wa serikali kuwapa TRA jukumu la kukusanya property tax ni sahihi kwa sababu
1. Makusanyo yataongezeka kwani wataalamu wa halmashauri watashirikiana na TRA na hakutakuwa na mianya ya rushwa iliyoko sasa katika ukadiriaji wa thamani za majengo(valuation).
2. Wenye majengo mengi makubwa hawalipi kodi ya mapato kikamilifu kwa hiyo TRA itawafahamu na kuwakadiria ipasavyo kutokana na vyanzo vya mapato ya kujenga majengo hayo na pia kama wamepangisha kutokana na kodi za pango.
3. Fedha zote zitaingia katika mfuko mkuu wa serikali na halmashauri zitapewa ruzuku kikamilifu kutegemea bajeti zao. Kwa hiyo wanaolalamikia uamuzi huu hawana nia njema au hawaelewi manufaa yake kwa kina.