Hapa tatizo ni mfumo mzima wa uwakilishi hapa Tanzania. La msingi hapa ni ku 'adopt' mfumo ambao wabunge wasiwe mawaziri. Katika mfumo huu mara mbunge anapochaguliwa na wananchi basi kazi yake ni moja tu nayo ni kuwawakilisha bungeni.
Katika mfumo huu, Rais anakuwa na fursa ya kuchagua mawaziri kutokana na watu ambao sio wabunge na watu hawa hufanya kazi kama waajiriwa. Faida kuu ya mfumo huu ni kuwa wanaochaguliwa wanakuwa ni watu wenye ujuzi na uwezo na sivinginevyo.
mfumo huu pia utasaidia kuongeza motisha ya kazi kwa wabunge kwani hivi sasa mbunge akichaguliwa, mawazo yake yote ni kupata uwaziri ili ale nchi. Akikosa basi huvunjika moyo na kuanza fitna kwa wale waliopata. Matokeao yake ni hali ya kupayuka Bungeni au kulala usingizi.
Faida nyingine ni kuwa uwakilishi katika Bunge unakuwa kamili. Katika hali ya sasa ambapo kuna mawaziri na manaibu kama 60, wote hao wanakuwa hawana muda tena wa kuwawakilisha bungeni wale waliowachagua. Hata jambo likiwa baya kwa wananchi wake lakini yeye kama waziri ni lazima aliunge mkono.
Tatizo hapa ni nani atakaye pitisha mabadiliko haya ya Kikatiba? Kwani wanaoweza kupitisha ni wabunge hao hao wanaoutaka uwaziri..