Wabunge wasiohudhuria vikao wakatwe mishahara na marupurupu yao | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wabunge wasiohudhuria vikao wakatwe mishahara na marupurupu yao

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by BAK, Feb 9, 2009.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Feb 9, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,528
  Likes Received: 81,939
  Trophy Points: 280
  Waungwana

  Kama mnavyofahamu Wabunge wetu wanalipwa mishahara mizuri pamoja na marupurupu manono. Wengi wao hawachangii katika mijadala yoyote inayoendelea bungeni na wengine huwa mahudhurio yao ni madogo sana maana huwa mtaani wakishughulikia shughuli zao binafsi ambazo hazihusiani na wao kuwa wawakilishi wa wale waliowachagua majimboni mwao.

  Mimi nafikiri wakati umefika sasa wale Wabunge wote ambao wanaenda bungeni kuchapa usingizi au hawahudhurii vikao vya bunge bila kuwa na sababu zozote za msingi za kukosekana kwao bungeni waanze kukatwa mishahara na marupurupu yao.

  Kama Mbunge anakosekana Bungeni kwa wiki mbili katika mwezi bila kuwa na sababu zozote za msingi basi mshahara na marupurupu yake ya wiki mbili yaondolewa katika pay slip yake na kurudishwa hazina. Hii itasaidia sana kupambana na wabunge watoro na wale ambao hawachangii katika mijadala mbali mbali ndani ya bunge.

  Kutohudhuria vikao vya bunge bila kuwa na sababu muhimu za kufanya hivyo au kuchapa usingizi ndani ya bunge bila kuchangia mijadala yoyote inayoendelea ndani ya Bunge ni ufisadi. Tunataka kuwa na bunge lenye Wabunge wachapa kazi wanaochangia katika mijadala yote inayoendelea ndani ya Bunge na pia kuhudhuria vikao vyote vya bunge bila kukosa kama hawana sababu za msingi za kufanya hivyo.

  Kuna umuhimu wa kuchukua hatua mbali mbali za kuimarisha bunge letu ikiwemo mahudhurio mazuri na kuchangia katika mijadala mbali mbali ndani ya Bunge.
   
 2. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #2
  Feb 10, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,528
  Likes Received: 81,939
  Trophy Points: 280
  Tuesday Feb 10, 2009
  Local News

  We are sorry for no show, PM says

  PUDENCIANA TEMBA in Dodoma, 10th February 2009 @ 10:15​

  The government today apologized for failure to have representation in the National Assembly on Monday evening, leading to adjournment of the session by the Deputy Speaker to today. Prime Minister Mizengo Pinda apologized on behalf of the government after Speaker Samuel Sitta demanded explanation from him as to why all ministers and their deputies were absent during the session.

  The premier said the ministers and some of the deputies were attending a cabinet meeting that was discussing establishment of a fuel reservoir under the chairmanship of the Vice-President, Dr Mohamed Ali Shein. He said Deputy Minister for Finance Jeremiah Sumari was presenting a paper on behalf of Minister Mustafa Mkulo who was in Dar es Salaam on official duties.

  He said the cabinet meeting started at 5pm and ended at 10pm and that the Minister of State in the Prime Minister's Office (Parliamentary Affairs), Philip Marmo and the Deputy Minister for Finance Omar Yusuf Mzee and other deputy ministers who were not in the cabinet were expected to represent the government in the House.

  "Unfortunately Mr Marmo was sick while Mr Mzee arrived late, and came back and told us that the session had been adjourned for lack of government representation," he said. Before the beginning of the questions and answers session today, Mr Sitta said the business had to be adjourned on Monday evening by Deputy Speaker Anne Makinda because of lack of government representation. The prime minister stressed that it was accidental and was not intentional.
   
 3. t

  tk JF-Expert Member

  #3
  Feb 10, 2009
  Joined: Feb 7, 2009
  Messages: 270
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Hapa tatizo ni mfumo mzima wa uwakilishi hapa Tanzania. La msingi hapa ni ku 'adopt' mfumo ambao wabunge wasiwe mawaziri. Katika mfumo huu mara mbunge anapochaguliwa na wananchi basi kazi yake ni moja tu nayo ni kuwawakilisha bungeni.

  Katika mfumo huu, Rais anakuwa na fursa ya kuchagua mawaziri kutokana na watu ambao sio wabunge na watu hawa hufanya kazi kama waajiriwa. Faida kuu ya mfumo huu ni kuwa wanaochaguliwa wanakuwa ni watu wenye ujuzi na uwezo na sivinginevyo.

  mfumo huu pia utasaidia kuongeza motisha ya kazi kwa wabunge kwani hivi sasa mbunge akichaguliwa, mawazo yake yote ni kupata uwaziri ili ale nchi. Akikosa basi huvunjika moyo na kuanza fitna kwa wale waliopata. Matokeao yake ni hali ya kupayuka Bungeni au kulala usingizi.

  Faida nyingine ni kuwa uwakilishi katika Bunge unakuwa kamili. Katika hali ya sasa ambapo kuna mawaziri na manaibu kama 60, wote hao wanakuwa hawana muda tena wa kuwawakilisha bungeni wale waliowachagua. Hata jambo likiwa baya kwa wananchi wake lakini yeye kama waziri ni lazima aliunge mkono.

  Tatizo hapa ni nani atakaye pitisha mabadiliko haya ya Kikatiba? Kwani wanaoweza kupitisha ni wabunge hao hao wanaoutaka uwaziri..
   
Loading...