Wabunge wasahau matatizo ya mimba sekondari za kata | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wabunge wasahau matatizo ya mimba sekondari za kata

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Jun 13, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jun 13, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  BAADHI ya wananchi wilayani Korogwe, Tanga, wamelalamika wabunge wao kwa kile walichokielezea kuwa ni kutoshughulikia ipasavyo, matatizo ya mimba kwa wanafunzi wa shule za sekondari za kata.Wananchi hao pia wamedai kuwa wawakilishi hao pia hawatembelei shule hizo hadi viongozi wa kitaifa, au Mwenge wa Uhuru unapopitishwa katika maeneo hayo.

  Kwa upande wao, baadhi ya wanafunzi katika shule hizo walisema hata wakifika katika maeneo ya shule, viongozi hao hawakutani nao ili kusikiliza matatizo yao na kwamba badala yake, wanaishia katika ofisi za walimu.

  Kwa mujibu wa wanafunzi hao, wakiwa katika ofisi hizo, wabunge hao wanatoa ahadi za kusaidia vifaa vya michezo na vitabu ambavyo hata hivyo baadaye hawavipeleki.

  Baadhi ya wanafunzi katika shule za Wilaya ya Korogwe, walisema wengi wao hawajawahi kumuona mbunge wao akitembelea shule.

  Wanafunzi wengine walidai kuwa hawajui hata jina la mbunge wao.Kwa upande wao wananchi walisema mbunge wao amekuwa akiwatembelea kwa nadra na hasa kukiwa na ziara za viongozi wa kitaifa kama Rais, Makamu wa Rais na Waziri Mkuu.

  Hali kadhalika wakati wa mbio za Mwenge wa Uhuru na kampeni za uchaguzi.
  "Rais akiondoka au mwenge ukipita mbunge naye anaondoka," alisema mkazi mmoja, wa Kata ya Manundu, Korogwe Mjini.

  Kata hiyo iko ndani ya jimbo la Korogwe Mjini linalowakilishwa bungeni na Joel Bendera, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Habari, Michezo na Utamaduni.

  "Ziara nyingi za wabunge wetu zinakuwa wakati huu wa kuelekea katika uchaguzi kwa ajili kampeni ambapo huahidi kutoa misaada mingi ambayo pia huwa hailetwi," alisema mwananchi mwingine.
  Hata hivyo, Madiwani Francis Komba wa Kata ya Mtonga, Neema Isaka(Viti Maalum), Robert Bago (Kata ya Manundu) na Amina Lukwalo wa Kata ya Magunga, mjini Korogwe walimtetea Bendera,kwamba ni mtu anayetembelea jimbo lake mara kwa mara.

  Kwa nyakati tofauti, madiwani hao walisema mara nyingi mbunge anafika jimboni kwa ziara za kuhimiza maendeleo ya shule na kusisitiza na nidhamu kwa wanafunzi.Wakuu wa shule za sekondari za Semkiwa, Willson Mgonja, Chief Kimweri, Anna Mrongo na Ngombezi, Clement Mhanusi, walisema Bendera alitembelea shule hizo mara nne tangu achaguliwe na kuzungumzia ya maenedeleo ya shule na nidhamu kwa ujumla.

  Lakini katika shule walizowahi kutembelea, wanafunzi walidai kuwa alifika mara moja au mbili tangu achaghuliwe.Jitihada za kumpata Bendera kwa njia ya simu kuzungumzia madai hayo hazikufanikiwahttp://www.mwananchi.co.tz/habari/4-habari-za-kitaifa/2444-wabunge-wasahau-matatizo-ya-mimba-sekondari-za-kata
   
Loading...