Wakati Chama Cha Democrasia na Maendeleo (CHADEMA) kikivuna maelfu ya wanachama wa chama tawala CCM, uku hali siyo shwari ndani ya NCCR - MAGEUZI chama ambacho kinaunda muungano wa UKAWA.
Ni jana tu aliyekuwa mbunge wa Kasulu mjini Moses Machali na Naibu katibu mkuu bara pamoja na aliyekuwa M/kiti wa Vijana Taifa Deo Meck walijiunga na ACT.
Leo imesemekana kuwa vigogo wengine wa chama hicho watakiama na kutimkia ACT vigogo hao ni mbunge wa Kigoma kusini David Kafulila, Mkosamali Mbunge wa Muhambwe na Nicolas Clinton M/kiti wa vijana jimbo la Nyamagana Mwanza.
Kwa mujibu wa naibu katibu mkuu wa ACT akiongea na Clauds Fm Amesema wabunge hao hatawataja kwa majina mpaka atakapo pokelewa katika majimbo yao.
pia naibu katibu mkuu huyo amesema Kuhusu Moses Machali aliyekuwa mbunge NCCR tayari amejiunga rasmi na chama hicho.
Hawa ACT wawaache tu, sisi tuko busy kugombea nafasi ya urais tu, mbowe kishatuzunguka kavuta mpunga kwa lowassa amuuzie chama, kweli siasa za kibongo hazina maana kabisa
Walisema 60, siyo 50. Pia wakasema Lowassa anajiunga nao. Namsikitikia Moses Machali kama amejiunga na wasaliti ACT, amechagua garasa. Bora Shibuda kaenda tawi lingine la CCM, yaani TADEA, kawaepuka ACT na Ayatollaak wao Zitto.Wabunge wanne? Majina? Siyo 50 tena? Wasaliti bana.
Hawa ACT wawaache tu, sisi tuko busy kugombea nafasi ya urais tu, mbowe kishatuzunguka kavuta mpunga kwa lowassa amuuzie chama, kweli siasa za kibongo hazina maana kabisa
Duh! Ni wabunge 4 tena sio 50?
Hii imekaaje, ACT wakiwachukua wabunge kutoka vyama vya upinzani mnashangilia, ati ACT waache tu, lakini UKAWA wakitaka kumchukua Lowassa inakuwa Mbowe keshatuzunguka na kuchukua mpunga. Ama kweli kutawaliwa na akili ndogo ni shida. Lowassa ana watu wanaomuunga mkono si chini ya milioni mbili na wabunge wa CCM zaidi ya mia na hamsini. Unamkataaje mtu mwenye mtaji wa wapiga kura zaidi ya milioni mbili na wabunge zaidi ya mia na hamsini. Ukimkataa mtu wa jinsi hiyo utakuwa kichaa.
Walisema 60, siyo 50. Pia wakasema Lowassa anajiunga nao. Namsikitikia Moses Machali kama amejiunga na wasaliti ACT, amechagua garasa. Bora Shibuda kaenda tawi lingine la CCM, yaani TADEA, kawaepuka ACT na Ayatollaak wao Zitto.