Wabunge wanayumbisha nchi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wabunge wanayumbisha nchi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by VUTA-NKUVUTE, Feb 6, 2012.

 1. VUTA-NKUVUTE

  VUTA-NKUVUTE JF-Expert Member

  #1
  Feb 6, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 5,869
  Likes Received: 6,608
  Trophy Points: 280
  Ni wazi kuwa Wabunge,hasa wa Bunge hili la kumi, chini ya Spika Anne Semamba Makinda ndio wanaoiyumbisha nchi.Ni Wabunge wa CCM wachache wa upinzani.Wao ndio viherehere wa kudai kuongezewa posho na mishahara.Wanataka,kwa mfano,posho zao zipande toka shilingi 70,000 hadi 350,000 kwa siku.Hizi ni posho za kufuru.Kada gani itavumilia kufuru hii ya Wabunge? Kwani wao wana nini na sisi tuna nini? Madaktari wametuonyesha njia.Pamoja na kutowaunga mkono Madaktari,TUCTA watalazimika kucheza mpira itakapofika zamu yao.Kwa mtindo huu,kila sekta itagoma.Amini nawaambia,nchi hii haitatulia hadi Bunge la Kumi litakapoacha ulafi...Rais zinduka na tumia madaraka yako kuondoa ulafi wa Wabunge wako wa CCM kuiponya nchi hii.Wakigoma Polisi na Wanajeshi je? Serikali itawapata wapi wengine?
   
Loading...