Mdau: Wanachojadili Wabunge kwenye group lao, wanataka magari yao yawe na Special number

BigTall

JF-Expert Member
Mar 9, 2022
421
1,048
Wadau salama, leo nimekutana na hili andiko, tusome mtazamo wa mwenzrtu kuhusu kile wanachojadili wabunge...

***************

WANAYOJADILI WABUNGE KWENYE GROUP LAO LEO KUTWA NZIMA

Na Thadei Ole Mushi

Wabunge wa CCM leo kwenye Group lao la kibunge wamejadili na kukusudia kupeleka hoja bungeni wapewe privilege ya magari yao kuwa na Special number.

Sababu kubwa ya kutaka hilo ni kuwa wanasema matrafiki wanawasumbua sana njiani na hawataki usumbufu huo. Kuna mambo kadhaa nayaona hapa:-

1. Tayari wameshajiona kuwa hao ni Raia Special nchini.Yaani wanajiondoa kwenye kuwa mwananchi wa kawaida kuwa VVIP. Wanataka kujitofautisha na wananchi wa kawaida.

2. Trafiki hawezi kukusimamisha kama huna makosa, tafsiri ya maombi haya ni kutaka kuhalalisha kufanya makosa.

3. Kila kundi likiomba Special number hapo barabarani kutakuwa ni vurugu tupu.

4. Nafikiri badala ya kujiombea wao Special number wangetuombea Sisi waalimu na Madaktari ambao huwa wanawahi shughuli nyeti za kijamii. Hebu fikiria Daktari anayemuwahi Mgonjwa asife anasimamishwa halafu mbunge anayekwenda kwa Mchepuko wake hasimamishwi.

5. Wabunge kwenye group siku nzima wanajadili kupewa Plate number Special wanaacha kubangua bongo wanaishauri vipi Serikali kutatua tatizo la mafuta ya kula na ya Petrol nchini ambayo yamepandisha vya kutosha maisha ya wananchi.

Wana Privilege nyingi sana hasa maslahi yao lakini hawajaridhika wanajipigania binafsi kuliko kuwapigania wananchi. Hivi ndivyo wanavyolamba Asali ambayo ni kodi yangu mimi na wewe.

1. Mbunge hulipwa mshahara kwenye scale ya LSS (P) 2 ambayo mshahara wake ni Shilingi 4,600,000.

2. Atalipwa posho ambazo kwa Mwezi hufikia Shilingi 8,292,000 katika mchang'anuo ufuatao.

✓Atalipwa posho Kwa ajili ya mafuta ya gari yake Shilingi 3,750,000.

✓Atalipwa Posho Kwa ajili ya Matengenezo ya Gari yake Shilingi 1,500,000.

✓Atalipwa Posho inayoitwa (Posho ya Mbunge na matumizi mengine jimboni) Shilingi 1,000,000.

✓ Atalipwa Posho ya kujikimu ya siku 10 kama atajisikia kwenda Jimboni Shilingi 450,000.

✓ Atalipwa Posho ya kujikimu kwa Wasaidizi wake watatu Kwa siku kumi atakazokuwa jimboni Shilingi 900,000 hapa kama atajisikia kwenda Jimboni au kwa mchepuko Dar 😂

✓ Atalipwa Posho ya watumishi watatu kama atajisikia kuajiri (Mhudumu wa Ofisi yake, Katibu wake, na Dereva) katika mchang'anuo ufuatao.

3.Katibu wake Shilingi 352,000 Mhudumu 170,000, Dereva 170,000. Jumla Shilingi 692,000. Hapa ni kama atajisikia kuajiri sio lazima.

Jumla ya Fedha zote zinafika Shilingi 12,892,000.Fedha hizi zote zinaingia kwenye account yake Mbunge.

Hii ni nje ya Posho za vikao vya Bunge.

2. Katika vikao vya budget mathalani Mbunge hulipwa Shilingi 240,000 kama sitting allowance, Shilingi 120,000 kama posho ya kujikimu kwa hiyo kwa siku ni Shilingi 360,000.

Bunge la budget pamoja na vikao vya Kamati kwa kalenda ya Bunge la budget la 2021/2020 lilianza na vikao vya Kamati Tarehe 6 march na kuendelea na Bunge lenyewe lililoisha June 30. Jumla ya siku zote ukitoa Jumapili ni siku 97 hizi siku ukizidisha mara 360,000 anazopata kwa siku unapata jumla ya Shilingi 34,920,000. Hii ni Fedha ya Bunge la budget tu. Hapa sijajumlisha na posho za Vikao vya bunge la mwezi wa 11.

Sifa kubwa ya kuwa Mbunge ni kujua kusoma na Kuandika. Nisaidie ku share kila mwananchi aone anachojadili mbunge wake leo.

Ole Mushi
0712702602.

*************************
 
Hakika Wabunge wanaupiga mwingi. Nimeamini ndio maaana wakati wa Uchaguzi Njia za Giza, Ubabe na Bao la Mkono hutawala.
 
✓ Atalipwa Posho ya kujikimu kwa Wasaidizi wake watatu Kwa siku kumi atakazokuwa jimboni Shilingi 900,000 hapa kama atajisikia kwenda Jimboni au kwa mchepuko Dar

✓ Atalipwa Posho ya watumishi watatu kama atajisikia kuajiri (Mhudumu wa Ofisi yake, Katibu wake, na Dereva) katika mchang'anuo ufuatao.

3.Katibu wake Shilingi 352,000 Mhudumu 170,000, Dereva 170,000. Jumla Shilingi 692,000. Hapa ni kama atajisikia kuajiri sio lazima.

Jumla ya Fedha zote zinafika Shilingi 12,892,000.Fedha hizi zote zinaingia kwenye account yake Mbunge.

Hii ni nje ya Posho za vikao vya Bunge.

2. Katika vikao vya budget mathalani Mbunge hulipwa Shilingi 240,000 kama sitting allowance, Shilingi 120,000 kama posho ya kujikimu kwa hiyo kwa siku ni Shilingi 360,000.

Bunge la budget pamoja na vikao vya Kamati kwa kalenda ya Bunge la budget la 2021/2020 lilianza na vikao vya Kamati Tarehe 6 march na kuendelea na Bunge lenyewe lililoisha June 30. Jumla ya siku zote ukitoa Jumapili ni siku 97 hizi siku ukizidisha mara 360,000 anazopata kwa siku unapata jumla ya Shilingi 34,920,000. Hii ni Fedha ya Bunge la budget tu. Hapa sijajumlisha na posho za Vikao vya bunge la mwezi wa 11.

Sifa kubwa ya kuwa Mbunge ni kujua kusoma na Kuandika. Nisaidie ku share kila mwananchi aone anachojadili mbunge wake leo.

Ole Mushi
0712702602.

*************************
Ubinaffsi tu ndo umewajaa
 
Mimi siwaamini wanasiasa kamwe. Na kijiwa mwanasiasa, sitakaa niamini hata maneno yangu mwenyewe.
 
Wabunge wawe wanalipwa na halmashauri,baada ya local kutoka bungeni kuwa alihudhuria Bunge,sasa Ndugai analipwa kwa kazi gani.
 
Kwa hiyo wagonga meza na wenyewe wanataka waonekane kama wasiojulikana....
 
Sijaelewa au katibu wa bunge sio watu wa uhasibu ni linguistic .hivi unapewa posho ya sitting allowance na bado unapewa night allowance.
Halafu kama ana wasaidizi hawaajiri na ofisi ya bunge bali vyote hupita mikononi kwa mbunge mwenyewe.Ina maana ni kibarua hawakakatwi kodi wala NSSF, wakimalizana basi.ni watu wa ajabu wasio na nia hata ya kuajiri watu 3.
 
Wabunge siyo watumishi wa kudumu. Wanaitumikia ilani ya miaka mitano tu. Wakimaliza wanatakiwa kuondoka. Anayetaka akubali kuleta mrejesho wa alichofanya na kutoa ahadi mpya.

Uelewa wa wananchi ndicho kigezo kikuu cha kuwapima wabunge. Endapo uelewa upo chini, basi lawama ni kwa wananchi wenyewe. Tusiwalaumu sana wabunge bila kuwageukia wananchi.
 
Waliotunga huo utaratibu wa kujilipa mahela yote hayo kwa ka nchi masikini na omba omba kama tanzania ni nani?
 
Hii nchi itaendelea mwaka ambao watazania tutaamka na kuamua huu upumbavu uishe, kinyume na hapo watatufanya wanavyojisikia hawa kenge. Na wameshaona watz ni mazuzu, wanatubidua bidua tu.
 
Kwa malipo hayo ndo maana tunaona wafanyabiashara wakubwa wanaenda huko,hyo pia ni sehemu ya kuongeza utajiri

Siku zote viongoz wetu wanajifikiria wao na familia zao,ingekuwa tuna umoja tungewapotezea kabsa hata kwenye makampeni tusingekuwa tunatokea
 
Wadau salama, leo nimekutana na hili andiko, tusome mtazamo wa mwenzrtu kuhusu kile wanachojadili wabunge...

***************

WANAYOJADILI WABUNGE KWENYE GROUP LAO LEO KUTWA NZIMA

Na Thadei Ole Mushi

Wabunge wa CCM leo kwenye Group lao la kibunge wamejadili na kukusudia kupeleka hoja bungeni wapewe privilege ya magari yao kuwa na Special number.

Sababu kubwa ya kutaka hilo ni kuwa wanasema matrafiki wanawasumbua sana njiani na hawataki usumbufu huo. Kuna mambo kadhaa nayaona hapa:-

1. Tayari wameshajiona kuwa hao ni Raia Special nchini.Yaani wanajiondoa kwenye kuwa mwananchi wa kawaida kuwa VVIP. Wanataka kujitofautisha na wananchi wa kawaida.

2. Trafiki hawezi kukusimamisha kama huna makosa, tafsiri ya maombi haya ni kutaka kuhalalisha kufanya makosa.

3. Kila kundi likiomba Special number hapo barabarani kutakuwa ni vurugu tupu.

4. Nafikiri badala ya kujiombea wao Special number wangetuombea Sisi waalimu na Madaktari ambao huwa wanawahi shughuli nyeti za kijamii. Hebu fikiria Daktari anayemuwahi Mgonjwa asife anasimamishwa halafu mbunge anayekwenda kwa Mchepuko wake hasimamishwi.

5. Wabunge kwenye group siku nzima wanajadili kupewa Plate number Special wanaacha kubangua bongo wanaishauri vipi Serikali kutatua tatizo la mafuta ya kula na ya Petrol nchini ambayo yamepandisha vya kutosha maisha ya wananchi.

Wana Privilege nyingi sana hasa maslahi yao lakini hawajaridhika wanajipigania binafsi kuliko kuwapigania wananchi. Hivi ndivyo wanavyolamba Asali ambayo ni kodi yangu mimi na wewe.

1. Mbunge hulipwa mshahara kwenye scale ya LSS (P) 2 ambayo mshahara wake ni Shilingi 4,600,000.

2. Atalipwa posho ambazo kwa Mwezi hufikia Shilingi 8,292,000 katika mchang'anuo ufuatao.

✓Atalipwa posho Kwa ajili ya mafuta ya gari yake Shilingi 3,750,000.

✓Atalipwa Posho Kwa ajili ya Matengenezo ya Gari yake Shilingi 1,500,000.

✓Atalipwa Posho inayoitwa (Posho ya Mbunge na matumizi mengine jimboni) Shilingi 1,000,000.

✓ Atalipwa Posho ya kujikimu ya siku 10 kama atajisikia kwenda Jimboni Shilingi 450,000.

✓ Atalipwa Posho ya kujikimu kwa Wasaidizi wake watatu Kwa siku kumi atakazokuwa jimboni Shilingi 900,000 hapa kama atajisikia kwenda Jimboni au kwa mchepuko Dar 😂

✓ Atalipwa Posho ya watumishi watatu kama atajisikia kuajiri (Mhudumu wa Ofisi yake, Katibu wake, na Dereva) katika mchang'anuo ufuatao.

3.Katibu wake Shilingi 352,000 Mhudumu 170,000, Dereva 170,000. Jumla Shilingi 692,000. Hapa ni kama atajisikia kuajiri sio lazima.

Jumla ya Fedha zote zinafika Shilingi 12,892,000.Fedha hizi zote zinaingia kwenye account yake Mbunge.

Hii ni nje ya Posho za vikao vya Bunge.

2. Katika vikao vya budget mathalani Mbunge hulipwa Shilingi 240,000 kama sitting allowance, Shilingi 120,000 kama posho ya kujikimu kwa hiyo kwa siku ni Shilingi 360,000.

Bunge la budget pamoja na vikao vya Kamati kwa kalenda ya Bunge la budget la 2021/2020 lilianza na vikao vya Kamati Tarehe 6 march na kuendelea na Bunge lenyewe lililoisha June 30. Jumla ya siku zote ukitoa Jumapili ni siku 97 hizi siku ukizidisha mara 360,000 anazopata kwa siku unapata jumla ya Shilingi 34,920,000. Hii ni Fedha ya Bunge la budget tu. Hapa sijajumlisha na posho za Vikao vya bunge la mwezi wa 11.

Sifa kubwa ya kuwa Mbunge ni kujua kusoma na Kuandika. Nisaidie ku share kila mwananchi aone anachojadili mbunge wake leo.

Ole Mushi
0712702602.

*************************
jamani vyoo vya shule za misingi tanzania vimezidi kunuka na kuwa vichafu. wabunge wangenyimwa posho zao hizo kwanza ili kuimarisha vyoo vya shule za msingi nchini. jamani mtu ni afya ianzie shule za misingi!
 
Back
Top Bottom