Wabunge wanaoongoza kwa kulalamika hawalisaidii taifa

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,034
Kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ibara ya 63 (2) moja ya majukumu ya Bunge la JMT (Mbunge) ni KUISHAURI NA KUISIMAMIA SERIKALI ya Jamhuri ya Muungano na vyombo vyake vyote katika utekelezaji wa majukumu yake

Katiba ambayo ndiyo sheria Mama, inaeleza wazi kuwa wabunge wanapaswa kuwa sehemu ya KUSHAURI pale ambapo mambo hayaendi sawa ili kuwezesha maisha ya Wananchi wanaowawakilisha kuwa bora kwa hali na mali.

Bunge la Tanzania lililoanza vikao vyake Jumanne 31/01/2023 limekuja na mtindo mpya wa baadhi ya wabunge KULALAMIKA na KUILALAMIKIA SERIKALI hasa kutokana na mfumuko wa bei na kupanda kwa gharama za maisha nchini. Kwa baadhi ya watu hawa wanaonekana kuwa wamefanya kazi yao vyema lakini kwa wale wanaofahamu kazi za wabunge basi wanaona wazi kuwa WABUNGE hawa ni mizigo

Kila mmoja anafahamu kuwa bei ya vyakula haishikiki huko masokoni LAKINI MBUNGE KWENDA KULALAMIKA BUNGENI BADALA YA KUSHAURI NINI KIFANYIKE NI KAZI YA UJUHA. Wabunge hawa ndio mategemeo yetu sisi wananchi na tunategemea wao ndio waiambie SERIKALI KUWA KWA SASA HALI NI MBAYA HUKO MITAANI HIVYO MNAPASWA KUCHUKUA HATUA HIZI NA HIZI ILI KUONDOA TATIZO HILI.

LAKINI HILI LA WAO KULALAMIKA TU BILA KUTOA MAWAZO NINI KIFANYIKA NI KUTUKOSEA ADABU, SASA KAMA WAO WANALALAMIKA TU, JE WATU WA VIJIWE VYA KAHAWA AU BODABODA WAFANYE NINI.

Pengine wabunge kama Gambo na Mpina hutegemei wakushauri lolote la maana katika kutatua matatizo ya uchumi zaidi ya wao kulalamika lakini UNAPOMSIKILIZA MSOMI KABISA KAMA Dkt BASHIRU, naye anapiga tu porojo unagundua tuna wabunge mizigo wengi sana WENYE KAZI YA KULALAMIKA TU ILI WAPATE UMAARUFU KWA WANANCHI LAKINI KAZI YAO KUBWA YA KUISHAURI SERIKALI HAWAIFANYI HATA KIDOGO.


BAshir.jpeg
 
Bunge linaharibiwa na wabunge ambao wanaongea kwa hisia zao na kufuata rumors/porojo ili kujionesha kwa watu kuwa wanahoja zenye mashiko kumbe pumba tu
 
Bunge linaharibiwa na wabunge ambao wanaongea kwa hisia zao na kufuata rumors/porojo ili kujionesha kwa watu kuwa wanahoja zenye mashiko kumbe pumba tu
Sahihi kabisa na bahati mbaya wanadhani kwa sababu wanatrend kwenye mitandao ya kijamii basi wana msaada kumbe ni kazi bure wanafanya
 
Mbona hata wewe hujashauri?

Kazi yako ni kushambulia na mikelele tu isiyosaidia
 
Ndio hulka ya Watzn hiyo Sasa ,unachokiona ndio jamii yetu ilivyo , watakwambia serikali itoe majibu..

Ikija na majibu wanaanza tena kulalamika 😁😁
 
Ndio hulka ya Watzn hiyo Sasa ,unachokiona ndio jamii yetu ilivyo , watakwambia serikali itoe majibu..

Ikija na majibu wanaanza tena kulalamika 😁😁
Wanasahau kuwa Serikali iliyopo madarakani ni ya chama chao na ni wajibu wao kushauri nini kifanyike
 
Back
Top Bottom