Wabunge wanamchimbia Rais Samia shimo!!

Kamundu

Platinum Member
Joined
Nov 22, 2006
Posts
9,293
Reaction score
13,958
Uwekezaji na misaada tuliyopata hivi miaka ya karibuni ikiwa pamoja wa watalii kuongezeka ni kwasababu Raisi Samia alifanya mabadiliko na mwamko 2021-2022. Haya mabadiliko yalitoa mwanga wa siasa mpya na mazingira mazuri ya uwekezaji

Sasa badala ya kuendeleza mazuri kuanzia 2023 Raisi Samia na bunge lake fake. Kuanzia 2023 Raisi Samia ameanza kujali machawa wanao sifia kila kitu hata mabaya. Haya yatafanya tena wawekezaji wajiulize mara mbilimbili kuwekeza Tanzania

Wabunge badala ya kumsaidia Rais na kusaidia nchi wanamchimbia shimo la kumzika kama vilevile walivyokuwa wanafiki kwa Magufuli kwa kusema Tanzania hakuna covid ! Kumbe walikuwa wanamchimbia shimo waje kumzika.

Leo hii walewale wanafiki ndiyo wanamwabia endeleza utekaji, ubakaji, usifuate sheria, kaka kuuwa wauwe tu !! Ukweli ni kwamba shimo la Mama niko futi 5 bado futi moja likamilike. Wanafanya haya sio kwa kumpenda Mama ni kuhakikisha wanaendelea kuwaibia watanzania bila kuulizwa.
 
Mnawasingizia tu shimo alichimba mwenyewe miaka iliyopita.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…