Ona kwa mfano mnyika hapa:-Niliuliza maswali mawili ya nyongeza; nilihoji ni lini serikali itatekeleza sera husika kwa kuwa upungufu wa ruzuku kwa shule za umma ni kati ya vyanzo vya kuporomoka kwa elimu kutokana na kuathiri uendeshaji wa shule ikiwemo upatikanaji wa vifaa shuleni, na kwa kuwa kwenye vyombo vya habari jana na leo kati walimu na wanafunzi wameeleza kwamba hali hiyo ni kati ya sababu za mgomo unaoendelea hivyo nikata serikali itoe kauli bungeni ya kuutafutia ufumbuzi mgogoro unaoendelea.
Hata hivyo Spika wa Bunge alimkataza Naibu Waziri asijibu swali kuhusu mgogoro kati ya walimu na wanafunzi dhidi ya serikali na kutaka kujibiwa kwa swali ya lini ruzuku itaanza kutolewa kwa kuzingatia viwango vya sera hata hivyo serikali ilitaja kiwango cha fedha ya ruzuku kwa mwaka wa fedha 2012/2013 bila kueleza iwapo viwango kwa mujibu wa sera vitafikiwa kwenye ngazi zote ikiwemo katika shule za msingi.
Sasa kuna haja gani ya bunge kama sio kupoteza kodi zetu tuu.