Wabunge wajipanga kummaliza Maswi

Wabunge wajipanga kummaliza Maswi

Hata kama ni tetesi Wondolewe tu,pamoja na aliyetuti hasara Warema

Tena hapa ilibidi na Mzee Six aongezwe sababu katuletea KATIBA ya MAFISADI ,wakisaidiana na CHENGE ili wale nchi wakimaliza wasishughulikiwe.I wish tungekuwa kama China tu wanyongwe.
 
Kuna baadhi ya watanzania ni waajabu sana nchini kwetu wakiona mtu au kiongozi mwizi wanampinga na wakiletewa mwingine ambaye ni mzalendo wa kweli na si mla rushwa na hatoi rushwa watamchukia na kumpikia majungu na kumfanyia mizengwe.

Ndugu wadau hoja yangu ya leo ni kuhusu wizara ya nishati na madini ambayo haijawahi kutulia hata mora moja kila siku inavurugu mara mawaziri wezi, mara makatibu wakuu na hata wakurugenzi kama katika shirika la tanesco ambalo lipo chini ya wizara ya nishati na madini.

Kwa sasa wizara hii kusema ukweli imepata viongozi wenye misimamo na wasio yumbishwa na hawana woga wowote na hawaogopi chochote ukianzia na waziri mwenyewe profesa muhongo ambaye bila woga alimwondoa aliyekuwa md tanesco mhando aliyekuwa akiiba, akamuondoa mwanasheria aliyekuwa akichota fedha tanesco nimrod mkono ambaye kwa mwezi alikuwa anachukua bilioni kumi na akahakikisha mgawo wa umeme uliokuwa ukioendelea miaka yote nchini na kudai kwamba mgawo ukiendlea nawafukuza kazi menejiment ya tanesco na bodi yake.

Ukija kwa maswi aliwapangua walaji na wababaishaji katika wizara ya nishati na madini na kuhakikisha wizara inaendeshwa kwa maadili na hakuna ubabaishaji na wizi na uwazi unakuwepo lakini na hakuna wanasiasa kuingilia utendaji wa wizara na taasisi zake kama ilivyokuwa huko nyuma.

Maswi ni muhongo viongozi wenye misimamo na hawaogopo iwapo akitokea mshenzi na mtu ambaye ataka kuleta ubabaishaji kama ilivyotokea kwa akina kafulila na zitto ambao wanatumiwa kwa kupewa fedha kupambana na maswi na muhongo na wao kwa vyovyote hawawezi kukubali.

Kuna jambo ambalo limetokea ambalo baada ya ripoti kutoka na kuonekana kwamba maswi na muhongo hawamo baadhi ya wabunge wamenipanga kutafuta eneo jingine la kupambana na maswi mojawapo ni kutumia sauti ya maswi iliyorekodiwa na kutumwa kwenye simu za watu mbalmbali ili wabunge wadai kwamba alimtukana kafulila.

Na kwa sasa amepangwa mbunge machali atumie sauti hiyo ya maswi kuiweka bungeni na kudai kwamba katibu mkuu maswi ambaye ni kiongozi wa serikali anatukana wabunge. (hivi kwa nini wabunge wao wawe wanatukana na kudhalilisha watu ndani ya bunge lakini wao wakijibiwa wanadai wametukanwa na wana kinga lini na sisi watanzania wengine tutakuwa na kinga hiyo. Mbunge akikutukana akikudhalilisha wewe mtu mwingine huruhusiwi kujibu wakati wabunge wengine ni wajinga na hawajasoma wengine hata uelewa mkubwa hawana kabisa. Hatutaki tumechoka

Tunasubiri kumuona Machali akitekeleza kazi aliyetumwa na Deo Filikunjombe na Zitto kumdhalilisha Maswi.
Aise itakua hujielewi,hivi uko nchi gani? Huyo waziri wako wa nishati kama yuko makini mwambie atoe hiyo mikataba aliogoma kutoa.... Acha siasaaaa
 
Nyoko nyie wote majizi,hakuna mtu mwadirifu na mchapakazi kama maswi,,,amewanyima kula kina zitto na kambi yake na sasa hv mnaimba wimbo wao,nani asiyejua nchi hii ilivyoteswa na uhaba wa umeme,leo hii mambo yametulia mnamwona maswi mwizi,nyoooo,,,,usenge wa zitto na usaliti wake na chuki zao kwa maswi ndo ziturudishe tulikotoka?achen hizo nyie.Nani asyemjua zitto alivyohongwa hela kuidhoofisha chadema,leo hii mnamkubali kwa lipi?hela wapige wengine msalaba wabebe wengine.Nani asyejua hela hizi zilipangwa wakati Maswi akiwa TAMISEMI?mbna hamwongelei chenge aliyepewa 1.6m us dollars?kwasabaabu ni mkakati mmekaa kimya,shame on u

hivi umeumbwa kama binadamu wengine? hata chizi hayuko kama wewe
 
Maswi na Mujongo ni visiki vya mpingo, majungu hayawezi kuwaondoa madarakani

Muziki haujawashwa we waanza kucheza,kiherehere cha nini? Subiri ripoti ijadiliwe ndiyo utauona ukweli!
 
acha kutetea uovu ndugu. Je ripoti ya cag inawaonea? Watanzania acheni kutumika kama dambala la dekio. Kipimo cha uaminifu hakipo hivyo mtu akipewa mamlaka tupo tunajua uaminifu wake. Tukiwa na watu kumi kama wewe katika level ya maamuzi basi taifa litaangamia. Usituhamishe kwenye agenda.

Wabunge wananunuliwa ili wadhoofishe wizara tunalifahamu sana hilo hili na inaonekana kabisa, siku ya jumapuili walikuwa na kikao nyumbani kwa Machali hapa mjini pembezoni wakiayajadili haya ili kuyawamaliza , naamini Tanzania haitaendelea kuendekeza majungu na fitina ili wizi uendelee.

Tatizo kubwa ni Misimamo ya Waziri muhongo na Maswi .Ipo siku adhabu yao tutawapa na iwe zaidi ya jehanamu wabunge wa kununuliwa, pamoja na yote wasidhani wao ni Mungu, Mungu yupo na anaona maovu yao na hakika atawapa adhabu yao stahili muda si mrefu.
 
.....baadhi ya wabunge wamenipanga kutafuta eneo jingine la kupambana na maswi.......

IPTL uneonekana huwezi kujipanga ndo maana wamekupanga.

Kwa maelezo haya una sound akili ya CCM. Kama ni kiongozi napata shida sana uwezo wa akili yako kuongoza hata vichaa! Poleni CCM.
 
Last edited by a moderator:
Wabunge wananunuliwa ili wadhoofishe wizara tunalifahamu sana hilo hili na inaonekana kabisa, siku ya jumapuili walikuwa na kikao nyumbani kwa Machali hapa mjini pembezoni wakiayajadili haya ili kuyawamaliza , naamini Tanzania haitaendelea kuendekeza majungu na fitina ili wizi uendelee.

Tatizo kubwa ni Misimamo ya Waziri muhongo na Maswi .Ipo siku adhabu yao tutawapa na iwe zaidi ya jehanamu wabunge wa kununuliwa, pamoja na yote wasidhani wao ni Mungu, Mungu yupo na anaona maovu yao na hakika atawapa adhabu yao stahili muda si mrefu.

Naweza kukuamini

Ukizingatia wabunge wapiga deal kutoka upinzani..inawezekana aisee..never trust wabunge 100%
 
Haka kasheria ka kinga na madaraka ya Bunge nadhani kanatumiwa vibaya. Katika kuhakikisha ya kwamba watu wote wapo sawa mbele ya sheria ni vyema haka kasheria kakafutiliwa mbali. Haiingii akilini kwamba Mbunge anasimama Bungeni anatumia kipaza sauti na kumtukana mtu ama mtendaji wa serikali na anasikika kwenye vyombo vya habari lakini huyu anayetukanwa hapewi nafasi ya kujitetea. Hii ni kimyume na natural justice. Haka kasheria kawe na kikomo ili wabunge wasitumie bunge kuwafanyia wenzao defamation.

Hapa ndipo Maswi, kijana wa Kikurya,( sijui Mkira, Mtimbaru ama Mwirege) anapopandisha mori na kusema huyo anayetumia Bunge kama kichaka kuwatukana watu ajitokeze hadharani aongee nje ya Bunge ili naye aonyeshwe kwamba ukiwa nje ya Bunge mambo yanakuwa haya!!

Hii vita ni kubwa, ni vita ya kimaslahi zaidi. Watu wamenyang'anywa matonge vinywani, watu wamenyimwa pa kuchukua rushwa, watu wamenyimwa pa kuuza miti toka Mufindi wakisema imetoka Kenya, watu wamenyimwa kuuza ma Jenerator, watu wamenyimwa kuwauzia TANESCO mafuta ya generator kwa bei za kuruka, migawo ya umeme ya kutengeneza imeisha, watu wamenyimwa udalali wa vitalu vya gesi, watu wamenyimwa kunyakua maeneo ya kutafuta mafuta na kujihodhia; watu hawataki kuyaona haya wanaangalia tu maslahi yao.

Hakina nasema hata kama wataonekana wana makosa ya kiutendaji lakini wamewatendea watanzania mazuri ya kukumbukwa. Prof. Muhongo na Eliakim Chacha Maswi nitawakumbuka kama watendaji mahiri katika Wizara ya Nishati na Madini.




.....watu wamenyang'anywa tenda ya uanasheria..
 
endeleeni kuwaficha ukweli na kutetea wafu wenzako
 
Back
Top Bottom