Wabunge wajadili mitambo ya Dowans gizani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wabunge wajadili mitambo ya Dowans gizani

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by fangfangjt, Mar 15, 2011.

 1. fangfangjt

  fangfangjt JF-Expert Member

  #1
  Mar 15, 2011
  Joined: Apr 25, 2008
  Messages: 571
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 33
  Wabunge wajadili mitambo ya Dowans gizani


  Monday, 14 March 2011 21:29
  Leon Bahati


  SIKU ya kwanza ya wabunge kujadili mpango wa kubadilisha sheria ya manunuzi ili serikali iruhusiwe kununua mitambo iliyotumika ilikumbwa na kioja cha aina yake baada ya umeme kukatika ghafla na giza kutanda ukumbini hali iliyowafanya baadhi ya wabunge kupiga kelele; Dowans! Richmond! Dowans! Richmond! Dowans na baadaye CCM! CCM! CCM!

  Ikipitishwa, sheria hiyo itaiwezesha Serikali kununua mitambo ya Dowans ili kutatua tatizo la umeme linalolikabili Taifa.Kelele hizo zilizoandamana na kejeli za kuwasha kurunzi za simu za mikononi na kumtaka mtoa mada kuendelea kwa kutumia mwanga huo hafifu zilisikika katika eneo walilokuwepo wabunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).


  Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti Manunuzi ya Umma (PPRA), Dk Ramadhani Mlinga ndiye aliyekuwa akitoa mada juu ya taratibu za Usimamizi wa Mifumo ya Manunuzi Serikalini.


  "Endelea! Endelea! Endelea!" Walisikika wabunge hao wakisema huku wakiwa wamewasha kurunzi za simu zao ambazo mwanga wake haukuhimili giza lililokuwepo kwenye ukumbi wa Hoteli ya Blue Pearl, Ubungo, Dar es Salaam." Wabunge walibakia gizani kwa takriban dakika 10 kabla ya umeme kurejea.


  Waandishi wa habari nao walitumia fursa hiyo kuwahoji baadhi ya wabunge na wakati wa mahojiano hayo, wabunge hao waliwasaidia wapigapicha za televisheni kwa kuwasha kurunzi za simu zao na kuwamulika usoni wale waliokuwa wakihojiwa ili waonekane vizuri.


  Mbunge wa Iringa Mjini (Chadema), Mchungaji Peter Msigwa alisema hayo ni matokeo ya Serikali ya CCM kukumbatia mikataba mibovu kama walioingia na kampuni ya Richmond Development LLC... "Mkataba huo ndiyo uliorithiwa na Dowans ambayo hukumu imetaka Tanzania iilipe kampuni hiyo Sh 94 bilioni."


  Mbunge wa Viti maalumu (Chadema), Naomi Kihula alilibebesha mzigo wa lawama Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) akisema kuzima kwa umeme huo ni ishara kwamba shirika hilo la umma haliheshimu hata Bunge.


  Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tindu Lissu alisema kitendo ni adhabu kutoka kwa Mungu kwa mjadala huo akidai kwamba Mkuu wa PPRA, Dk Milinga alipinga vikali utoaji wa zabuni kwa Richmond lakini vigogo serikalini wakashikilia msimamo wa kumpinga.


  Alisema hakubaliani na mpango huo wa kubadili sheria hiyo ya manunuzi ili kuwezesha serikali kununua mitambo ya Dowans kama njia ya kutatua tatizo la umeme nchini.


  Baada ya jenereta la hoteli hiyo kuwashwa, Dk Mlinga aliendelea na mada yake na kueleza kwamba kutatua tatizo la umeme nchini kwa kununua mitambo mipya itachukua muda mrefu. Lakini akasema sheria ya PPRA inayotumika sasa hairuhusu kununua mitambo iliyotumika jambo ambalo linaibana serikali kutafuta suluhu ya tatizo la umeme nchini kwa haraka.


  Kwa mujibu wa Mlinga, siyo lazima sheria hiyo iruhusu moja kwa moja ununuzi wa mitambo iliyotumika, bali iwe ni mazingira magumu kama yalivyo nchini sasa na kwamba kutakuwa na vigezo.


  "Taratibu (kwa sheria mpya) zitaandaliwa ili kukabiliana na mazingira ya kusaidia mitambo ikinunuliwa iwe na vigezo vya kitaalamu vinavyoonyesha uwezo wake wa kazi," alisema.


  Lakini hakuna mbunge aliyechangia kwenye mkutano huo unaongozwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Uchumi na Fedha, Dk Abdallah Kigoda aliyeonyesha wazi kwamba anaunga mkono mpango wa kubadili sheria hiyo ya manunuzi.


  Hali hiyo ilimfanya Dk Kigoda kuwataka wawe makini kwa sababu kamati yake ilijadili kwa undani suala hilo na kubaini kwamba sheria hiyo ina upungufu... "Suala la manunuzi tulifikirie kwa umakini," alisema akieleza kuwa wabunge ndiyo wanaotarajiwa kuokoa jahazi la tatizo la umeme nchini.


  Aliwataka wajaribu kufikiria njia fupi ya kulitatua ili kuokoa uchumi, maana hali inaweza kuwa mbaya zaidi kwa taifa iwapo litadumu kwa siku 100.


  Awali, akifungua mkutano huo, Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai aliwataka wabunge hao kutumia fursa hiyo kuishauri serikali kuhusu utaratibu mzima wa usimamizi na mifumo ya ununuzi wa umma kwani hali ya nchi ni mbaya.


  "Eneo la manunuzi ni changamoto kubwa kwa serikali. Bado kuna udhaifu katika udhibiti na uwajibikaji katika eneo zima la manunuzi," alisema Ndugai na kuwataka wabunge kuwa makini na kutumia mjadala huo kuishauri serikali kwa sababu asilimia 70 ya bajeti yake inatumika kwa manunuzi na asilimia 90 ya bajeti ya maendeleo nayo hutumika katika suala hilo hilo.


  "Fedha nyingi za Serikali zinapotea katika manunuzi. Ni changamoto kwetu sisi wabunge kuishauri ipasavyo Serikali katika eneo hili. Muswada wa Sheria ya Manunuzi ya Umma ya mwaka 2010 unategemewa kujadiliwa na kupitishwa na Bunge lijalo," alisema Ndugai.


  Hata hivyo, alisema kabla ya kupelekwa bungeni, Kamati ya Bunge ya Fedha na Uchumi itawashirikisha wadau mbalimbali kuuboresha.
   
 2. G

  Gurtu JF-Expert Member

  #2
  Mar 15, 2011
  Joined: May 15, 2010
  Messages: 1,202
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Watanzania tunatakiwa kusoma hadi darasa la ngapi ili tuwe na uelewa mpana? Haiingii akilini mwangu kama kuna mantiki kwa serikali kupoteza muda mwingi kushawishi wabunge waridhie kubadilisha sheria ya manunuzi ya umma ili iweze kuruhusu mazingira ya ununuzi wa mitambo chakavu.

  Hoja ya ununuzi wa mitambo chakavu ni mazingira ya kujenga ufisadi bila kujibu maswali ya msingi kama haya:
  1. Siyo kweli kuwa hoja hii ya kubadilisha sheria inalenga kununua mitambo ya Dowans?
  2. Kwanini Serikali ya Tanzania ilijenga mazingira ya kukodi mitambo badala ya kununua ya kwake?
  3. Kwanini unununzi wa Mitambo chakavu uwe kipaumbele wakati kuna uwezekano wa kununua mitambo mipya?
  4. Je, huu utaratibu unaofikiriwa kuingizwa kwenye sheria unatumika katika nchi gani?
  5. Je, waliokuwa wamenunua mitambo ambayo wameyatumia hadi yakawa chakavu wana sababu gani za kuuza mitambo hiyo na ipo katika hali gani?
  6. Je, mitambo chakavu ikinunuliwa na bado ikashindwa kufanya kazi atalaumiwa nani?
  7. Ni nini tatizo la serikali katika kununua mitambo yake wenyewe?Je, ni kutokuwa na fedha au kutokujua soko la mitambo kama hiyo?

  Tuna haja ya kuwa na maswali mengi ya kujiuliza katika mazingira ya utendaji wetu. Tunapaswa kushangaa sana kwani kama mitambo mipya tunashindwa kununua lakini yakiwa chakavu tunayaweza tuna maanisha nini? Haiingii akilini kama serikali yenye ubavu hata wa kukopa fedha hata IMF ishindwe kununua mitambo yake hadi inunuliwe na kampuni binafsi au watu binafsi.

  Tunahitaji kuelewa mazingira ya dharura ni yepi kwa sababu tukichukua mfano wa tatizo la umeme linaeleweka miaka mingi na msimu wa maji kukauka kwenye mabwawa unaeleweka. Dharura inaanza lini na nani wa kufafanua maana ya dharura.

  Watanzania tunatakiwa kuwa makini kwani sasa ninaona nchi hii hatuna viongozi bali tuna watu wanaotaka kutawala nchi kwa malengo yao na kwa faida yao
   
 3. M

  Mzee Kibiongo JF-Expert Member

  #3
  Mar 15, 2011
  Joined: Jun 18, 2008
  Messages: 241
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Na ni bora walizimikiwa umeme mkutanoni. Wao ndio walishinikiza mkataba uvunjwe, halafu wao hao hao ndiyo wanapigia kelele suala la Dowans halafu wanalalama nchi kuwa gizani. Lakini hawaji na mkakati mbadala wa kututoa gizani. Wa-TZ kwa kujifanya tunajua kuongea na kupiga kelele nyingi ni mafundi. Wanaume wa kweli ni wale waliopeleka suala la Dowans mahakamani. Wabunge na wote wanaopigia kelele suala la Dowans na umeme bila mkakati mbadala ni madebe matupu.
   
 4. kweleakwelea

  kweleakwelea JF-Expert Member

  #4
  Mar 15, 2011
  Joined: Nov 29, 2010
  Messages: 2,419
  Likes Received: 435
  Trophy Points: 180
  kukubali kununua vitu chakavu bina element za ufisadi!
   
 5. kweleakwelea

  kweleakwelea JF-Expert Member

  #5
  Mar 15, 2011
  Joined: Nov 29, 2010
  Messages: 2,419
  Likes Received: 435
  Trophy Points: 180
  kukubali kununua vitu chakavu ina element za ufisadi!
   
 6. Bill

  Bill JF-Expert Member

  #6
  Mar 15, 2011
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 4,158
  Likes Received: 1,246
  Trophy Points: 280
  Kwa nini kila mara umeme ni dharura. Hatutaki kanunueni mitambpo mipya. Suppose hiyo Dowans isingekuwepo mngechukua hatua gani kukabiliana na hii dharura?
   
 7. Mtumishi Wetu

  Mtumishi Wetu JF-Expert Member

  #7
  Mar 16, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 4,982
  Likes Received: 425
  Trophy Points: 180
  [FONT=&quot]WABUNGE WAJADILI DOWANS GIZANI;[/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]Gazeti la Mwananchi la Machi, 15, 2011,na Leon Bahati, liliandika kwamba wabunge wa bunge letu tukufu la Tanzania walijadili ili kubadili sheria ya manunuzi, serikali iweze kununua mitambo ya DOWANS. [/FONT]
  [FONT=&quot]Kisingizio ni kwamba nchi inaingia hasara kubwa kwa kukosa umeme kwa muda mrefu, hivyo basi wabunge wakubali sheria ya kutonunua mitambo iliyo tumika ibadilishwe ili serikali iweze kununua mitambo mitumba ya Dowans. [/FONT]
  [FONT=&quot]Hii project ni kwa faida ya nani tujiulize??????[/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]Lakini nina hakika humu JF kuna watu au wabunge wanaoweza kuwa na maono ya mbali saana ili kuondoa tatizo la umeme Tanzania kabisa. [/FONT]
  [FONT=&quot]Nilishajaribu kuandika humu kuhusu namna ya kuondoa hilo tatizo la umeme for a long term solution. Kununua mitambo ya thermo ya Dowans ni jibu la muda mfupi, maana mahitaji ya umeme Tanzania ni makubwa bado. [/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]Kwanza gharama ya kuendesha mitambo ya mafuta diesel (MFANO IPTL) ni kubwa saana kwa uchumi wa nchi masikini kama yetu. Kwa kukosa huruma kwa watu wanchi hii na kuangalia masrahi binafsi watu watahitaji kununua mitambo ya generator (wapate 10%) inayokula mafuta mengi saana na kuwa mzigo kwa uchumi wa taifa hili.[/FONT]
  [FONT=&quot]Hivyo kuwa na umeme usiotegemewa kunasababisha hata wawekezaji kutukimbia na kwenda kuwekeza kwenye nchi zenye umeme wa uhakika.[/FONT]
  [FONT=&quot]Tuangalie kwenye vyanzo vyetu vya asili vya umeme, mito yetu kama Kagera, Kihansi, Rufiji, Ruvu, hivyo vyote ni vyanzo muhimu vya umeme, tuwe na malengo ya mbali ya maendeleo kwa faida ya taifa letu na vizazi vijavyo.[/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]Tuache uchoyo wa kujifikiria kibinafsi badala ya kupanga kuinua uchumi wanchi yetu. Tutangulize taifa mbele uzalendo kwa maendeleo ya kudumu badala ya mipango ya zima moto inayofilisi nchi yetu tuipendayo Tanzania.[/FONT]
  [FONT=&quot]NIMEWEKA MFANO WA WENZETU WA ECUADOR WALIVYO JIPANGA KUONDOA TATIZO LA UMEME. Soma chini; [/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]15 March 2011 Last updated at 09:37 GMT [/FONT]
  [FONT=&quot]SOURCE BBC NEWS.[/FONT][FONT=&quot][/FONT]
  [FONT=&quot]Ecuador's San Rafael falls: At risk from energy plans?[/FONT]
  [FONT=&quot]By Irene Caselli[/FONT][FONT=&quot] San Rafael, Ecuador [/FONT][FONT=&quot][/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT][FONT=&quot][/FONT]
  [FONT=&quot]A visit to the Coca river and the San Rafael Falls[/FONT]
  [FONT=&quot]Continue reading the main story[/FONT][FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]Related Stories[/FONT]

  [FONT=&quot]The image of the San Rafael waterfall is ubiquitous in Ecuador's Amazon region, appearing on everything from tourist brochures to the backs of buses, alongside the Virgin Mary meant to protect drivers.[/FONT]
  [FONT=&quot]The waterfall, the country's largest, is in the Sumaco Biosphere Reserve, a lush site protected by the United Nations for its unique flora and fauna, a result of the wet climate that originates from the meeting of the Andean and Amazon regions.[/FONT]
  [FONT=&quot]But environmentalists say this natural wonder and its delicate ecosystem will be destroyed by what is set to be the country's largest hydroelectric power plant, which is being built on the river that feeds the San Rafael Falls. [/FONT]
  [FONT=&quot]The state-owned company that is managing the Coca Codo Sinclair project says such worries are unfounded. [/FONT]
  [FONT=&quot]They say hydrological studies have established the optimal ecological flow needed for the waterfall to keep flowing with the same intensity, and the project is designed to ensure that this flow is met.[/FONT]
  [FONT=&quot]Chinese funding[/FONT][FONT=&quot][/FONT]
  [FONT=&quot]Promoters and critics agree that Ecuador needs to renew its energy model, and that hydroelectric power will play an important role; where they disagree is over how sustainable Coca Codo Sinclair will be. [/FONT]
  [FONT=&quot]The idea for the project was born in the 1970s, but it was not until President Rafael Correa came to power in 2007 that Coca Codo Sinclair became a priority. [/FONT]
  [FONT=&quot]The project was stalled for a few years while the government looked for funds to finance its construction. Last June, after long negotiations the government secured a $1.7bn (£1bn) loan from the Export-Import Bank of China.[/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT][FONT=&quot][/FONT]
  [FONT=&quot]Matt Terry, of the Ecuadorian Rivers Institute, says studies on the waterfall are out of date [/FONT]
  [FONT=&quot]Chinese contractor Sinohydro officially started operations soon after but, several months on, the construction site seems eerily empty - hardly what one would expect from the government's flagship project.[/FONT]
  [FONT=&quot]Signs in Chinese and bright lights - which locals say have forced away the area's endemic butterflies - are the main indications of the changes to come.[/FONT]
  [FONT=&quot]The dam will be built some 20km (12 miles) upstream of the fall to divert the Coca river, one of the main watercourses in Ecuador's Amazon region. [/FONT]
  [FONT=&quot]The project is supposed to generate 1,500 MW of electricity using 222 cubic metres (7,840 cu ft) of water per second from the river. [/FONT]
  [FONT=&quot]According to Matt Terry, director of the Ecuadorian Rivers Institute, a non-governmental organisation, the hydrological studies are out of date.[/FONT]
  [FONT=&quot]You can see plans in the acquisition of funds for the project. The long term process for implementation of this project, aimed for the development of this nation. [/FONT]
  [FONT=&quot]Wakuu nawasilisha; Tuijadili.[/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
   
Loading...