Wabunge wa Upinzani Waingia na Mabomu ya Machozi Bungeni...Wavaa Gas Mask na Kuyalipua...

kibogo

JF-Expert Member
Apr 1, 2012
9,739
4,734

Hili ni bunge la Kosovo, nchi iliyojipatia uhuru mwaka 2008 baada ya Yugoslavia kusambaratika. Bunge la Kosovo ni bunge linaloongoza kwa vituko barani Ulaya.

Kwa muda mrefu kumekuwa na mvutano mkali bungeni kati ya Serikali na wabunge wa upinzani. Hoja kuu ya upinzani ni Serikali itoe ufafanuzi kwanini nchi yao ya Kosovo imekithiri kwa rushwa, ubadhirifu, ukosefu wa ajira na umasikini.

Tarehe 19 Februari mwaka huu bila kutarajiwa wabunge wa upinzani waliamua kuingia bungeni huku wakiwa wamejihami kwa kuvaa vifaa vya kuzuia gesi (gas mask) na kuanza kuwarushia wabunge wa chama tawala mabomu ya machozi.
 
Wamenifurahisha sana hizo ndio zinaitwa siasa za kisayansi nadhani kwa kupitia hilo serikali yao itaelewa upinzani wanamaanisha nini Na lazima akili itawakaa sawa.
 
Hehehe!, siasa iz vere intateining sam taimz!

When conversing don't work, actions like this do :)

Cc Dodoma
 
Hiyo inaitwa #ShikaAdabuYako#
Huu ni mfano mzuri sana inabidi ukawa waige maana mi CCM inaboa sana
Na hayo matatizo ndo yaleyale yanayoikumba tz.
Siku hizi wabunge wa UKAWA ni wachovu sana, hawezi kutamka neno "fisadi"
 
Hivi hawa ni wale wanao zipigaga bungeni?!
Jamaa wana uchungu na nchi yao!, wana impose policies mpaka kwa makofi, mpaka kieleweke :)
 
Imenikumbusha nchi moja jina nimelisahau, ila ni nchi iliyojitenga toka USSR,mbunge mmoja alichangia hoja bungeni kwa Kirusi(Lugha ) alipokea kichapo cha hatari toka kwa wabunge mwenzake
 
Back
Top Bottom