East African Eagle
JF-Expert Member
- Jul 26, 2013
- 3,759
- 2,209
Vyama vinavyounda UKAWA havina sura ya kitaifa.Mfano vyama vikubwa kama CUF na CHADEMA vina sura ya kikanda,kikabila na kidini zaidi.Mfano CUF ina nguvu zanzibar na kinaonekana mbele ya macho ya wengi zaidi kama chama cha wapemba na waislamu wenye msimamo mkali.Tanzania bara hakina nguvu.
CHADEMA pia ni chama kinachoonekana mbele za watu kama chama cha watu wa kilimanjanjaro na wakristo na kina nguvu bara wakati kule zanzibnbar hakina nguvu.
Niliwahi zungumza na Kingunge ngombare Mwiru kuwa ni kwa nini upinzani hauchukui utawala kama kenya,zambia,malawi n.k Akajibu kuwa vyama vya upinzani Tanzania ni vyama vya majimbo kingine kiko jimbo la Tanzania Kingine jimbo la Zanzibar.Akasema kutawala nchi unahitaji chama cha kitaifa siyo cha majimbo kama CUF na CHADEMA.
Chama cha ACT kinaonyesha kuwa kina sura ya kitaifa na kinaweza kuwa chama cha upinzani chenye nguvu kote Tanzania bara na Zanzibar hivyo Wabunge wa UKAWA hamieni huko .Pia CHADEMA na CUF vimejionyesha kuwa vyama vya kidikiteta kwa kuwaburuza wabunge kwa lazima wasiamue kwa utashi wao kuhudhuria au kutohudhuria bunge la katiba hivyo kuvifanya vyama hivyo viwe vya kidikiteta ambavyo ni tishio kwa hao wabunge na ustawi wao wa kisiasa tofauti na chama Cha ACT.
Ni ushauri wangu.Kama hamtaki si neno