Wabunge wa UKAWA hamieni ACT-Tanzania

Wabunge wa UKAWA hamieni ACT-Tanzania

Mmmh, really!!??..........Ina maana hata ukisimama jukwaani katika mikutano yenu ya uenezi wa chama chenu cha ACT unaweza kujenga hoja kwa uelekeo na mtazamo huu ndugu East African Eagle ili kushawishi wananchi wawaunge mkono na kupata wanachama?

Kwa mtazamo wangu, this is too low na kwa hakika huku ni kushindwa kusonga mbele kwa kiwango cha juu sana kwa sababu safari ya ACT kujijenga na kujiimarisha kisiasa as a futuristic strong political party in Tanganyika/Tanzania, haijafika hata robo and honestly kama chama kina watu kama wewe kinachowategemea anyhow (majukwaani, mitandaoni na hata ONE TO ONE) kukijenga na kukieneza kwa kwa maana ya kueneza sera, itikadi, imani na mipango ya chama, then lazima kiandike maumivu tu!!

And you know what bro? Hata hawa wabunge wa CHADEMA na CUF unaowaalika wajiunge na chama chako kwa mtindo na mbinu hii ya kiwango cha chini sana cha ushawishi, kiukweli watakuwa wamekudharau sana kwa sababu utakuwa umewaweka katika viwango vya daraja la chini sana la "wapumbavu na wajinga!!"

Aidha, tunasikia kuwa ACT ni kama tawi la CCM na kwa maana hiyo kinapata ufadhili wa fedha za kuendeshea shughuli zake za sasa toka huko na kwa maana hiyo wabunge wa CUF na CHADEMA unaowaita "kujiunga" na ACT likely target ni kupata fedha hizo ambazo (labda) zitakuwa zaidi ya mafao watakayopata baada ukomo wa ubunge wao walionao kufika hapo mwakani 2015.

Fine, tu assume wamekubali wito huu na kuzipata fedha hizo ikiwemo kulipia madeni yote waliyonayo kutoka katika taasisi walizokopa mara baada ya kuukwaa ubunge. Ni wazi kuwa watakuwa wamejiunga na chama si kwa sababu wamevutiwa na sera, itikadi na mipango ya chama bali ni kwa sababu ya fedha tu, au siyo? Ni kwa maana hiyo wakitokea wengine wanawapa fedha zaidi na zaidi, watakwenda huko!!

Mwisho, napenda tu kuuliza maswali haya, kwamba, hivi kuna binadamu yeyote amewahi kutosheka na pesa katika ulimwengu huu? Hivi ninyi wenyewe waanzilishi wa ACT pamoja na CCM mfadhili wenu, kuna mtu asiyehitaji pesa na mamlaka na ameridhika na alichonacho kwa sasa?

Kwa maswali haya ambayo kwa kweli majibu yake ni HAPANA; tunafika kwenye hitimisho la kwamba, ni ngumu sana na actually ni uwendawezimu kwa mtu yeyote kuitoa familia yake katika nyumba ambayo tayari anaishi na aliijenga na kuikamilisha kwa gharama kubwa na inapendeza isipokuwa kwa kasoro na mapungufu madogo madogo tu ya kiufundi na eti kwa kushawishiwa ahamie katika nyumba ambayo iko katika fikra tu ya hatua ya kuanza kujenga msingi kwa tumaini na imani kuwa itakuwa nzuri zaidi sana sana kuliko hii anayoishi sasa!!...

Kina Samwel Sitta, Dr Harrison Mwakyembe, Nape Moses Nnauye, James Lembeli and others waliliona hili na kuuona ukweli huu (just before 2010 General Election?) na CCJ yao na kisha kuchukua maamuzi sahihi, ndiyo maana mpaka leo wapo katika ulingo wa siasa za juu za Tanzania lakini CCJ ni kama haijawahi kuishi. I am optimistic that, ACT - Tanzania kwa mtindo na mwendo huu wa kisiasa, uelekeo wake ni huuhuu!

Hii mbinu haifai hata chembe kama kweli chenu ni chama cha kiisiasa. Na kama ni chama cha kisiasa cha kweli chenye malengo ya muda mrefu, basi, build yourselves from grassroots, recruit new and commited party members na na sharti muonje machungu ya kuimarisha vyama vya upinzani katika nchi za dunia ya tatu kama hii ya kwetu. Na ofcoz kama kuna wakongwe kutoka vyama vingine wanaotaka kuhamia kwenu, wafanye hivyo wenyewe kwa kuvutiwa na itikadi, sera na mipango thabiti ya kichama cha kiisiasa, and not anything else kwa sababu itakuwa ni kujilisha upepo tu!
 
Back
Top Bottom