maramia
JF-Expert Member
- Jul 17, 2015
- 2,030
- 1,345
Kuna habari zimeandikwa katika magazeti ya leo kwamba kuna baadhi ya wabunge tena wa CCM wamekamia kumweka kiti moto spika wa bunge pamoja na kuiadabisha serikali ya Rais John Pombe Magufuli eti kwa kitendo chake cha kutoa amri ya kuhojiwa na baadaye kufikishwa mahakamani kwa wabunge wanne wa CCM waliotuhumiwa kwa kuomba rushwa. Kangi Lugora, Mwambalaswa, Murad na Ndassa.
Naamini kama hii ni kweli, wabunge hao wanadanganyana mchana kweupe, hakuna watakachoweza kumfanya Rais kwa hilo, badala yake nao wataporomoshwa na wananchi kama majengo pacha ya Marekani ya World Trade Centre yalivyoporomoshwa na magaidi wa Al Qaeda, wala wasithubutu.
Yaani wabunge wa CCM waungane kuitetea mijitu iliyoomba rushwa ili iharibu taratibu za nchi, No No kwa hilo watakuwa peke yao nasi wananchi tutasimama upande wa Magufuli dhidi yao.
Mimi binafsi nawaomba wabunge hao ambao baadhi tuna majina yao wajiweke wazi katika hili ili tujue wanachokipigania hasa ni nini labda wanaweza kupata wapumbavu wa kuwasapoti badala ya kuendesha usaliti wao kisiri.