Omutwale
JF-Expert Member
- Feb 4, 2008
- 1,429
- 1,053
Unajua idadi ya wabunge wanaopaswa kuwepo Bungeni au umeona chadema tu? Unakumbuka kuwa saa saba lilitolewa Tangazo kuwa wanakikao? angalia idadi ya wabunge wa ccm na CHADEMAwaliopo kwa asilimia ni akina nani watoro? Njoo na hoja yenye mashiko si kukurupuka
Wachangiaji wa namna hii ndo wanawapofusha Wabunge na viongozi wa CDM. Mwenzetu Mohamedi Mtoi anawachukulia CDM kama muhimili (reference pillar) wa mabadiliko na dola tarajiwa inayotegemewa ilete mageuzi ya kimfumo na kimuundo. Hivyo haitegemewi CDM wafanye kama CCM.
Na kwa muktadha huo ndo maana Mohamedi Mtoi anawashangaa na kuwakanya wajirekebishe. Lakini memba ambao wameifanya CDM na viongozi wa CDM kuwa Malaika hawataki daima chama na viongozi wao wakemewe wala kuguswa kwa makosa wanayofanya. Huku ni kupelekea akili na utashi wetu likizo.
Tunaanza kuzidiwa na wanyama wanaopambanua walau kidogo