Wabunge wa CHADEMA wamkaribisha Lowassa


Kuna kitu cha ajaabu kidogo. Wabunge wote wa Kaskazini wako radhi kumpokea fisadi aliyenyimwa uingozi kwao. Amebaki Silinde pekee ndiye kaongea kama Mtanzania, wengine wire ukabika. Ama kweli tutaona mengi safari hii. Makamanda wako tayari kumtisa Kamanda Slaa mradi tu wawe na "mwenzai". Matata kwelikweli. WM.
 
Mkuu, ...Suala muhimu siyo kubadili chama au jina la chama, suala muhimu ni kubadili mfumo wa fikra na mitazamo.
Unachosahau Ng'wamapalala ni kwamba tupo humu ambao tunachukua muda kusoma mtiririko wa thread kabla ya ku comment na wapo ambao wata comment tu post moja bila kuangalia mjadala ulipoanzia, ulipo na unakoelekea. Ndio maana pamoja na kujiunga JF zaidi ya miaka minane iliyopita michango yangu haijafika 6,000 sawa na wastani wa post 2 kila siku tofauti na wengi.

Comment
uliyoitoa hapo juu yathibitisha kabisa ninalolisema kila siku, tuna watu wamejiaminisha kimakosa kwamba wanachosema ni sahihi. Tatizo la mfumo wa fikra na mtizamo hauwezi kupatiwa ufumbuzi na watu wale wale wenye fikra na mawazo yale yale yaliyosababisha fikra hizo hizo na mtizamo huo huo. Kuamini hivyo ni ama kujidanganya katika nafsi zetu au ni matokeo ya fikra zisizo huru zinazosukumwa na unafiki.

Duniani kote panafika pahala ili kuweza kufanikiwa kuleta mabadiliko lazima kutokee mapinduzi na kama nchi imeweza kuongozwa na watu wale wale kwa mfumo ule ule kwa miaka hamsini, mabadiliko hayawezi tena kuwa ya hiari. Binadamu ana tatizo la mazoea na mazoea yanapata nguvu zaidi kadiri siku zinavyosogea na ndio maana ni vigumu kuwatoa madarakani waliokaa muda mrefu kama CCM kwani kumejengeka kiburi cha hatimiliki mioyoni mwao.

Kukaa tukisubiri mabadiliko yaletwe na CCM ni zaidi ya ujuha kwani mtu anatakiwa tu ajiulize ni kitu gani kimezuia hayo mabadiliko yasifanikiwe kwa mihula hiyo yote. Alikuja Mwinyi na ufagio akatuahidi Tanzania mpya na safi, miaka kumi baadaye akaja Mkapa na uwajibikaji akiahidi uwazi na uwajibikaji, miaka ishirini baadaye akaja Kikwete na nguvu mpya, ari mpya na kasi mpya! Wote tu mashahidi kwa matatizo tuliyoyapata.
Siyo wote walioko CCM ni mafisadi na siyo mafisadi wote ni CCM.
Hii ndio hasa ninaiita lugha ya kilaghai ambayo inaweza kutamkwa na mtu anayedanganyika kirahisi, tabia ambayo imekuzwa na mazoea badala hali halisi. Kama kuna fisadi nchi hii, kikatiba ni nani anatakiwa kumshughulikia? Kama kuna wahalifu ndani ya nchi hii ni nani kapewa mamlaka na katiba ya nchi kumwajibisha? Kama tuna utawala unaofuata sheria ni kwa nini kila siku ni kilio kile kile cha wananchi kuhusu kutopata haki na usawa mbele ya sheria?

Mwaka 2010 kuna watu walitajwa kwamba ni mafisadi lakini pamoja na kelele zote, watu hao hao eti walichaguliwa kwa kura nyingi na kupewa uongozi wa nchi! Utawala uliokuwapo ulitumia kila mbinu kuhakikisha unabaki madarakani ikiwa ni pamoja na kuvitumia vyombo vya dola usalama kusimamia uchaguzi usio huru. Nani yuko CCM amewahi kukemea matumizi ya vyombo vya dola kupambana na wananchi wanaodai haki zao? Sana sana tumeshuhudia wale wanaowajeruhi na hata kuwaua wananchi wasio na hatia wakipandishwa vyeo!

Hapana Ng'wamapalala, wewe ni katika watu wanaokesha humu wakitetea hali hii kwa madai ya kijinga kama ulivyoanza hapo juu..eti Siyo wote walioko CCM ni mafisadi na siyo mafisadi wote ni CCM. Wote tumeshuhudia mafisadi ndani ya CCM wakilindwa na hata kuogopwa, je hao mafisadi walio nje ya CCM nao wako juu ya sheria? Mathalani ikithibitika kwa Mh. Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema kaiba, vyombo vya dola vinasubiri nini kumshughulikia au na yeye anaogopwa na serikali kama alivyowahi kutamka Waziri Mkuu Mizengo Pinda?

Mbona ni jambo la kawaida tu kuwakamata viongozi wa upinzani, kuwapiga wabunge wa upinzani na hata kuwasweka ndani kwa mambo ya kipuuzi? Kwa nini kama ni wezi wasikamatwe wakafunguliwa mashtaka? @Ng'wamapala, nachukia sana unafiki lakini nachukia zaidi matapeli wa kisiasa popote walipo. Hebu soma tena mada zote unazozianzisha pole pole na taratibu halafu ujiulize kama kweli una nia njema katika kuzianzisha. Hao wasafi ndani ya CCM wameweza vipi kuishi pamoja na kuwa na mshikamano na mafisadi?
 
Last edited by a moderator:
Asanteni wabunge wa chadema kwa kukiri kumpokea mzee weyu low as a, watanzania baadhi wanaanza kutuonyesha ukabila hasa kwenye kupeana ajira na Leo wanaleta usoni, jeshi no wasukuma wamejaa kisa wakubwa ndio wao, tunawataka viongozi was kutujali site,
 
HABARINI ZA JIONI

MAKAMANDA NAOMBA UFAFANUZI KUHUSU HILI

1. inakuwaje lowasa akiwa nje ya chadema anakuwa fisadi ..ila akiwa ndani ya chadema anakuwa msafi..nasema ivi kutokana na chadema kujiandaa kumpokea lowasa ushahidi ninao na picha ninazo..kuwa soon lowasa anaenda chadema..kama niivyo hata magufuli aki amia chadema nahizi kashfa mnazo mpa atakuwa msafi tena

2.ina kuwaje kwenye pesa ambazo na watu wa chadema zina wahusu huwa hawa ongei chochote..inamaana nanyi pia mna jali maslahi yenu..nasema hivi nikiwa na maanisha pesa za kampeni zilitolewa nyingi sana zaidi ya milion 200 kwa kila mbunge lakini hakuna hata moja alie lalamika kuwa serikali ina ingia hasara na wananchi wana umia..posho za bunge nikubwa sana but hakuna wabunge wanao fight with..

Niliwaza kuconlude kuwa chadema huwa wanakuwa wapole sehemu ambayo na wenyew wana husika...

NAOMBA NIELEWEKE KUWA SIKO UPANDE WA CHAMA CHOCHOTE ILA NAOMBA MAJIBU TOKA KWENU MAKAMANDA..
 
Mapato na matumizi ya chama hazina ipo tengelu, na hapo hakuna anaehoji.
 
Mmeingia woga sana, lakini hamna namna...

Leo mtasema yote, endeleeni kuropokwa...

Teh teh
 
Ametubu, kwani mtu akikosa basi ataendelea kuwa mkosaji mpaka afe??? Fikiria hata wewe dhambi ngapi umefanya hivyo msikitini/kanisani wakufukuze. Ukiona umeenda kanisani/msikitini ina maana umekubaliana na sera za huko. Karibu na wewe tukutubishe, uwe msafi
 
Hakuna jibu, maana unacho uliza ni wazo lako, au hisia zako, sasa unatakka kujibiwa hisia zako? Lowassa yupo CCM si Chadema, kama umeota yuko Chadema pole yako, Elewa hiyo ni ndoto tu kama ndoto zingine
 
Nani ksema Lowsa anatfutwa na CDM? Un ushhidi?
 
petro faustine,

..hivi hujawahi kusikia mhalifu akisaidia polisi ktk upelelezi?

..wakati mwingine mhalifu anaweza hata kusamehewa makosa yake au kupewa kifungo kifupi ikiwa atatoa ushirikiano utakaopelekea kukamatwa wahalifu wengi zaidi.
 
Last edited by a moderator:
Kila chama kinayo misingi yake ambayo ukitaka kwenda huko yakupasa uielewe Na uwe radhi kuifuata. Yy Na wenzie ukiona hivyo ujue wametubu Na kuiamini injili ya cdm. Hongereni cdm kwa usajili, Mimi sina chama ila nitawapigia kura yangu kwa ngazi zooooote.
 
Gamba Ng'wamapalala

Kila Siku lazima uanzishe thread inayomhusu Lowassa na CHADEMA.
Acha wivu wa Kike Mkuu,muacheni Mzee wa watu afanye analoona linamfaa,huku kutapata kwenu Ma agents wa Magamba ni indication kuwa huyo Mzee Mnamgwaya sana.
Mkuu;
Gamba Bramo

Kuanzisha thread ni utashi wa kila mwanaJF.

Huu wivu wa kike ndiyo upi? Wa kiume ndiyo upi?

Kuansisha thread zinazomhusu Lowassa haina maana nina muogopa au simuogopi.

Kitu gani kunafanya udhani ninatapatapa na pia ni ajent wa magamba.

Mimi na Lowassa wapi na wapi.

Nashangaa unaumizwa na thread zinazomhusu Lowassa. Kwani wewe pia ni ajent wa Lowassa?
 
kama ungekuwa na akili ungewauliza ccm ni kwa nini waohawamfukuzi wakati wanasema na mchafu?

vile vile kama ungekuwa na akili ungeiuliza serikali ya ccm kwa nini hawakumpeleka mahakamani kwa sababu bunge lilisema alihusika na richmondi na moja ya mapendekezo ya kamati ya bunge lilikuwa kuwafikisha mahakamani wote waliohusika?

au na wewe wamekubandikia tikiti maji kichwani?
 
Hakuna kitu chanamna hiyo kuwa cdm Kuwa wa
namchukuwa lowasa ccm muendelee naye
 

Mkuu Gamba Ng'wamapalala


Kwnaini tu usifanye uka Complie thread zako zote zinazmhusu Lowassa na CHADEMA ukaja na uzi Mmoja.
Kila Siku Kuanzisha uzi unaomhusu Mtu ni Kushusha hadhi ya Jukwaa Letu Mkuu.
 
Last edited by a moderator:
Mbona unajihami sana kuwa huna chama! Najua hofu yako ni kuwa utajulikana kuwa mwana CCM maana ni wana CCM tu wanaouliza maswali ya hovyo na wivu kiasi hiki. Basi kama huna chama chochote, umetumwa na mwana ccm uulize hili swali yaani unatumika, tena vibaya.
 
Mkuu,
Acha jazba na matusi!

Kila mwananchi ana fikra na mtazamo wake, cha muhimu ni kujenga hoja na kupambana katika hoja.
 
Umesomeka mkuu,,,hata kama yeye lowasa hatakubali kujiunga na CDM hizo kauli na tetesi za viongoz wa cdm kumtaka lowasa ajiunge nao zimekishushia hadhi cdm..mi najiondoa rasmi CDM

Subiri Lowasa akiingia CHADEMA mnabadilishana kadi anakupa ya makufuli unampa ya funguo, kisha unaacha chama.
 

Nakuunga mkono zaid ya 100%,lowasa kuingia CDM nikukiua chama kwa haraka na uhakika mkubwa,mtu ambaye mlisema ni fisadi na ccm wakawasaidia zaid kusema ni kwel ni fisadi,leo kusema mumkaribishe nikujiua kwa uhakika mkubwa sana,
Hakuna taasisi yoyote ambayo imewahi kumsafisha na wala yeye mwenyewe hajawahi sema ni nani alihusika kama siyo yeye zaidi yakusema anauchukia umaskini(ambayo ni porojo)...
Leo bashe amemnyanyua mkono magufuli,ambapo bashe alikuwa ni mtu muhimu katika team ya lowasa,ila leo kamtosa,wale madiwan wa monduli ni kizungumkuti,leo wanasema wapo CDM kesho wamechukua form zakugombea udiwani ccm,kwa hiyo utaona kuwa lowasa hana wafuasi wala watu ambao utasema ni wapo nae popote pale,zaid ya wao kuangalia fursa(na lowasa wakat ule alitumia fedha sana)na hata hawa wanaoshadadia ahamie CDM ni kuwa bado anawapa fedha.
Kitendo cha lowasa kujiunga CDM iwe awe mwanachama wa kawaida au vyovyote ujue CDM itapoteza wanachama wengi ambao ni wafia chama na hata ule uaminifu katika macho ya watu utakuwa umekufa na hiko ndio kifo chake...
Ccm imevua gamba CDM inajifanya inajua kuaminisha watu nyeusi ni nyeupe,katika kosa kubwa lakiufundi watalofanya CDM nikumpokea lowasa,huku kwenye mitandao watu wanapiga kelele kuwa anafaa ila huko field hali ni tofauti...ujumbe huu uwafikie,wasiposikia wataona kwa vitendo...CDM inajitosheleza haihitaji mtu wa namna yake
 
Umesomeka mkuu,,,hata kama yeye lowasa hatakubali kujiunga na CDM hizo kauli na tetesi za viongoz wa cdm kumtaka lowasa ajiunge nao zimekishushia hadhi cdm..mi najiondoa rasmi CDM

Subiri Lowasa akiingia CHADEMA mnabadilishana kadi anakupa ya makufuli unampa ya funguo, kisha unaacha chama.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…