Wabunge wa CCM waelezea sababu ya Magufuli kupendwa zaidi na watu wasio na elimu na masikini

real G

JF-Expert Member
Feb 7, 2013
5,241
2,000
Dodoma. Wabunge wa chama tawala wameunga mkono ripoti ya Taasisi ya Twaweza inayoeleza kushuka kwa ushawishi wa Rais John Magufuli.

Ripoti hiyo iliyotolewa jana na kubainisha kwamba umaarufu wa Rais huyo wa awamu ya tano umeshuka na kwamba anakubalika miongoni mwa maskini, wasio na elimu kubwa pamoja na waishio vijijini.

Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Lucy Mayenga amesema kilichoelezwa na Twaweza ni sahihi kwa sababu Rais amejielekeza kwa makundi hayo ambayo hayana mtetezi.

"Hao ndiyo watu wengi zaidi. Kiuchumi inakubalika," amesema Lucy.

Wakati Lucy akiendelea kutoa hoja zake, Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega alitoa taarifa iliyopokelewa na mtoa hoja.

Uledi amesema: "Kwa muda wa utafiti, Rais alikuwa anapambana na vyeti feki, dawa za kulevya na mafisadi. Hao wote hawawezi kumpenda zaidi ya maskini ambao hawaguswi na mambo hayo."

Lucy ametoa maoni hayo wakati akichangia mjadala wa bajeti ya Serikali unaoendelea bungeni.

Chanzo: Mwananchi
 
mng'ato

JF-Expert Member
Oct 27, 2014
28,589
2,000
Hata watumishi wa umma wanampenda sana sana na ndio maana hata UHAKIKI mwingine wa wafanyakazi unaanza upya soon.
 
Kihava

JF-Expert Member
May 23, 2016
4,300
2,000
CCM rafiki zake ni mbumbumbu, maskini na wanaosumbuliwa na maradhi yakiwemo ya akili. Na ndio mtaji wao. Ndio maana hakuna siku CCM itaandaa mtaala wa kufundisha shuleni kuwafanya watu waewe werevu. Hata siku moja. Nikiwa kidato cha Tano na Sita enzi hizo tulisoma riwaya moja inasema " Usiku utakapokwisha". Kwamba siku ambayo watanzania watapambazuka kiakili watakaa watawala wanaowaonea na kuwanyanyasa. Lakini bila usiku wa akili na ufahamu kwisha tutaendelea kupiga makofi kwa wezi kama wale waliokunywa juisi magogoni juzi.
 
HEKIMA KWANZA

JF-Expert Member
Mar 31, 2015
2,882
2,000
Dodoma. Wabunge wa chama tawala wameunga mkono ripoti ya Taasisi ya Twaweza inayoeleza kushuka kwa ushawishi wa Rais John Magufuli.

Ripoti hiyo iliyotolewa jana na kubainisha kwamba umaarufu wa Rais huyo wa awamu ya tano umeshuka na kwamba anakubalika miongoni mwa maskini, wasio na elimu kubwa pamoja na waishio vijijini.

Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Lucy Mayenga amesema kilichoelezwa na Twaweza ni sahihi kwa sababu Rais amejielekeza kwa makundi hayo ambayo hayana mtetezi.

"Hao ndiyo watu wengi zaidi. Kiuchumi inakubalika," amesema Lucy.

Wakati Lucy akiendelea kutoa hoja zake, Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega alitoa taarifa iliyopokelewa na mtoa hoja.

Uledi amesema: "Kwa muda wa utafiti, Rais alikuwa anapambana na vyeti feki, dawa za kulevya na mafisadi. Hao wote hawawezi kumpenda zaidi ya maskini ambao hawaguswi na mambo hayo."

Lucy ametoa maoni hayo wakati akichangia mjadala wa bajeti ya Serikali unaoendelea bungeni.

Chanzo: Mwananchi

Ni lini wabunge wa CHADEMA wataeleza kwanini wamepoteza mvuto? Asilimia 17 tu ndio wanawakubali, tatizo ni nini? mambo ya kubadilisha gia angani?
 
jingalao

JF-Expert Member
Oct 12, 2011
33,138
2,000
CCM rafiki zake ni mbumbumbu, maskini na wanaosumbuliwa na maradhi yakiwemo ya akili. Na ndio mtaji wao. Ndio maana hakuna siku CCM itaandaa mtaala wa kufundisha shuleni kuwafanya watu waewe werevu. Hata siku moja. Nikiwa kidato cha Tano na Sita enzi hizo tulisoma riwaya moja inasema " Usiku utakapokwisha". Kwamba siku ambayo watanzania watapambazuka kiakili watakaa watawala wanaowaonea na kuwanyanyasa. Lakini bila usiku wa akili na ufahamu kwisha tutaendelea kupiga makofi kwa wezi kama wale waliokunywa juisi magogoni juzi.
werevu wanaokubali kuongozwa na DJ Zero?
 
galindas

JF-Expert Member
Mar 3, 2013
981
1,000
Utambuzi wa mambo huendana na elimu, sasa kama mmewanyima elimu huko vijijini mnategemea uwezo wa kupambanua mambo wanautoa wapi.? Wanachosubiri uchaguzi ufike muwape kofia na kuwadanganya wakichagua chama kingine patatokea vita. Shame on you.
 
bne

JF-Expert Member
Oct 11, 2016
1,618
2,000
Ni lini wabunge wa CHADEMA wataeleza kwanini wamepoteza mvuto? Asilimia 17 tu ndio wanawakubali, tatizo ni nini? mambo ya kubadilisha gia angani?
Mbona jibu rahisi tu.
Kuzuiwa shughuli za kisiasa na kuacha upande mmoja kuendelea propaganda kupitia viongozi wa umma ndio sababu kuu
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom