Emma.
JF-Expert Member
- Jun 25, 2012
- 19,932
- 5,560
Heshima kwenu Wana JF.
Wabunge wa CCM leo bungeni wameicharukia serikali kuhusu mpango wa serikali wa kutaka kukata mafao yao
Wabunge wa chama cha mapinduzi CCM wamezungumza kwa hisia kali walipokuwa wakipinga hatua ya serikali kutaka kuwakata kodi kwenye yao watapokamaliza kazi ya ubunge mwaka 2020.
Wabunge hao wamesema hawatakubali kuona wanakatwa kodi ya mafao yao na serikali walipokuwa wakichangia mjadala bungeni wa kupitisha Bajeti kuu ya serikali kwa mwaka wa fedha 2016-2017 ,mjini dodoma .
Mbunge wa Mwibara Kangi anasema -Kila mwenzi tunakatwa kodi ya mapato alafu mafao yetu na yenywe yakakatwe kodi?mnataka turudi mtaani alafu muanze tena kutucheka .Lazima wabunge tulinde maslahi yetu hatuwezi kukubali .
Hawa ndo wabunge wamechaguliwa na wananchi wanakwenda bungeni kutetea maslahi yao?