Wabunge wa CCM ni wasaliti, Wamenunuliwa na majangili? - Uhuru

masopakyindi

Platinum Member
Jul 5, 2011
17,890
13,190
Katika kuonyesha kutofurahishwa kwa kusitishwa kwa Operation Tokomeza, wananchi wengi sasa wameanza kuamini kuwa ni vigogo, wengine ndani ya CCM na wabunge ndio wanaofadhili au kuneemeka na biashara haramu ya kuua tembo-rasilmali ya nchi.

Kwa mujibu wa gazeti la Uhuru , leo tarehe 6 Nov 2013, limasema,

CHADEMA igeni mfano huu tubadilike kwa kukabiliana na viongozi wabadhilifu wa rasilimali fedha za Chama kwani wanakwamisha. malengo ya Chama
 
Chadema igeni mfano huu tubadilike kwa kukabiliana na viongozi wabadhilifu wa rasilimali fedha za Chama kwani wanakwamisha. malengo ya Chama

Tubadilike..tangu lini wewe ukawa chadema? Ya chadema waachie chadema wenyewe!
 
Ha ha haa mnafiki masopakyindi, hayo yangesemwa na Mh. Msigwa ungetokwa na mapovu ila kwa kuwa ni UHURU poa tu, utaunga mkono...TAIFA LA WANAFIKI waliolewa bendera ya kijani!
 
Last edited by a moderator:
Mmh, hao wabunge wenyewe wanajua hata kama wamenunuliwa? Sidhani.

Huwa nahisi wao kila wanalotetea wameaminishwa ni kutetea chama cha kiendelee kuwepo madarakani (Brain washed), wakikipinga na wao wanakuwa kwenye hati hati ya kupoteza madaraka yao.
 
Chadema igeni mfano huu tubadilike kwa kukabiliana na viongozi wabadhilifu wa rasilimali fedha za Chama kwani wanakwamisha. malengo ya Chama

Unataka Chadema waige nini toka kwa hawa wabunge na mawaziri majangili? Imedhihirika kuwa mtu kama Lukuvi ni jangili wa meno ya Tembo kwani msaidizi wake alikamatwa kwenye operation TOKOMEZA na yeye akawa mstari wa mbele bungeni kutaka operation isimamishwe kwani ingeendelea naye angetiwa mbaroni!!!Serikali inabidi ifanye uamuzi mgumu kuhusu majangili hawa na wala isiwaonee aibu!!!
 
Mmh, hao wabunge wenyewe wanajua hata kama wamenunuliwa? Sidhani.

Huwa nahisi wao kila wanalotetea wameaminishwa ni kutetea chama cha kiendelee kuwepo madarakani (Brain washed), wakikipinga na wao wanakuwa kwenye hati hati ya kupoteza madaraka yao.
Mkuu wabunge hao wala hawaitendei haki CCM ni masilahi yao binafsi.

Kusitisha Operation Tokomeza ni usaliti na tunaona kwenye luninga Wachina wanavyo vuna pembe kama wako kwao.
 
Ha ha haa mnafiki masopakyindi, hayo yangesemwa na Mh. Msigwa ungetokwa na mapovu ila kwa kuwa ni UHURU poa tu, utaunga mkono...TAIFA LA WANAFIKI waliolewa bendera ya kijani!

Mkuu Mag3, huyu jamaa masopakyindi ni mnafiq ajabu.
Mimi hata sijui anasimamiaga wapi.
Kweli ni kundi la Wanafiq waliolewa bendera ya kijani...
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Mag3, huyu jamaa masopakyindi ni mnafiq ajabu.
Mimi hata sijui anasimamiaga wapi.
Yaani anasubiri Mpaka Gazeti la Uhuru ndo limwambie kuwa wabunge wa CCM ni wasaliti plus Brain washed...ajabu sana aisee...
Kweli ni kundi la Wanafiq waliolewa bendera ya kijani...
 
Last edited by a moderator:
Katika kuonyesha kutofurahishwa kwa kusitishwa kwa Operation Tokomeza, wananchi wengi sasa wameanza kuamini kuwa ni vigogo, wengine ndani ya CCM na wabunge ndio wanaofadhili au kuneemeka na biashara haramu ya kuua tembo-rasilmali ya nchi.

Nnyambala, naona sasa unaelekea tunakoelekea wengine. Hii nchi ni ya kila mtu, tunapolalamikia maovu tuwe kitu kimoja. Rushwa na ujangili vinaathiri kila mtu, regardless anatoka chama gani.

OUT OF TOPIC
Hivi wewe na Simiyu yetu mpo chama kimoja?
 
Mkuu wabunge hao wala hawaitendei haki CCM ni masilahi yao binafsi.

Kusitisha Operation Tokomeza ni usaliti na tunaona kwenye luninga Wachina wanavyo vuna pembe kama wako kwao.

Kinachogomba hapo ni namna hiyo operesheni ilivyoendeshwa. mimi siamini kwamba kwa hali ilivyo sasa hivi, serikali hii inao uwezo wa kupambana na majangili, wauza madawa ya kulevya, na wengine kama hao. tatizo ni kwamba kuna wazito ndani ya biashara hizo. na hao ndio wanafanya operesheni ya kweli iwe ndoto. kinachoweza kufanyika ni vurugu tu hasa kuwaumiza watu wasio na uwezo wa kutoa rushwa. hata ukiangalia tatizo la wenye malori, utaona kwamba kisiki ni kwamba kuna vigogo waliojiingiza huko. wamehujumu reli ili wafaidike. na hiyo inafanya iwe ngumu sana kuchukua hatua stahiki. kilichotakiwa ni uongozi wa juu uwe tayari kabisa kupambana na rushwa na ufisadi kwa nguvu zote. lakini kwa kuwa mafisadi na wala rushwa wamejipenyeza katika mfumo mzima wa serikali, tutabakia kupiga kelele na kulalama tu
 
Ha ha haa mnafiki masopakyindi, hayo yangesemwa na Mh. Msigwa ungetokwa na mapovu ila kwa kuwa ni UHURU poa tu, utaunga mkono...TAIFA LA WANAFIKI waliolewa bendera ya kijani!
Mkuu tumia asilimia ndogo tu ya akili yako ya kuzaliwa na utueleze maudhui ya mada, kama inaunga mkono ujangili au la!
Nisingependa kukuingiza kwenye yale makundi ya watu wasio na uwezo wa kuchambua mada, ila wasindikizaji kwa vibwagizo.
 
Sijisumbui kukuita mkuu, maana hustahili!
Maana nyie masalia ya F4F mna taabu sana.

Nakupa changamoto moja na iku keep busy mchana huu, hebu tafuta mada moja humu JF ambayo nimeunga mkono mafisadi, majangili au wezi wa EPA etc.

Tatizo la watu kama ninyi ni kuwa na akili za kuandamana tu kama Lema.
 
Nnyambala, naona sasa unaelekea tunakoelekea wengine. Hii nchi ni ya kila mtu, tunapolalamikia maovu tuwe kitu kimoja. Rushwa na ujangili vinaathiri kila mtu, regardless anatoka chama gani.

OUT OF TOPIC
Hivi wewe na Simiyu yetu mpo chama kimoja?
Tupo pamoja mkuu.
Watu wanachoshindwa kuelewa ni ukweli kuwa hata wana CCM damu damu wanaudhika sana na ufisadi ndani au nje ya chama chao CCM katika hali yoyote ile.
Likini siye wenye ngozi ngumu, tumeamua kubaki ndani ya chama hadi kieleweke.
Hakuna mwana CCM anapenda kuibiwa!

Mii ni mwana CCM damu damu, [MENTION]Simiyi yetu[/MENTION] changamoto hiyo, lakini naamini tupo pamoja.
 
Mkuu na mimi ninao walalamikia ni hao vigogo ndani ya hiyo biashara, lakini kusitisha zoezi kunaleta hisia kuwa kuna wana CCM wanaohusika na ndio wapigaji kelele wakuu.
Cha kufanya ni kwamba kama kuna walioonewa watetezi wao wangewasiliana na wansheria ili sheria ichukue mkondo wake on isolated cases.

Lakini kusimamisha operation hii mimi naichukulia kama uhujumu.
 
CHADEMA igeni mfano huu tubadilike kwa kukabiliana na viongozi wabadhilifu wa rasilimali fedha za Chama kwani wanakwamisha. malengo ya Chama

Usipotawaja chadema utajamba?yaani topic haziendani kabisa du kweli watu ni watupu mbaya,hamsaomi kazi kupost tu uchafu wenu,
GOD BLESS YOU
 
sasa wewe unapoambiwa achana na flan ni mwizi nawe unasema siyo mwizi, na unapomshuhudia anaiba unakubali kweli ni mwiz nimeshuhudia, unaambiwa tena achana naye hutaki inaonyesha na wewe ni mwizi, kama hupendi wizi ungeachana naye na ikibidi toa taarifa polis
 
Mara ngapi nimeshakwambi, Nenda pale Coet UDSM, zamani ilikuwa inajulikana kama Faculty of Electrical and Computer Systems Engineering halafu kaniulizie ndo ujue kama mie ni F4F au vp.
Btw, sihitaji kuitwa Mkuu na mtu mnafiq kama wewe
 
Operation iendelee kuwepo maana inasaidia kulinda maslahi ya wananchi, ikiaachwa hivi hawa Wachaga wataifilisi hii nchi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…