Wabunge wa CCM kupiga kampeni Longido, Tume ya Uchaguzi mna taarifa?

Toosweet

JF-Expert Member
May 27, 2012
2,141
1,982
Heshima Kwenu,

Baadhi ya wabunge wa CCM wameonekana kumpigia kampeni za chinichini aliyekuwa mgombea ubunge kstika jimbo la Longido (CCM),Dr. Steven Kiruswa kwenye Uchaguzi Mkuu wa 2015 mbele ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aliyekwenda kuweka jiwe la msingi kwenye mradi wa maji wa Longido.

Junk 29,2016 Mahakama Kuu Kanda ya Arusha ilitengua ushindi wa mbunge wa Longido, Onesmo Ole Nangole (CHADEMA) na sasa Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC) inasubiriwa kutangaza kuwa jimbo liko wazi na tarehe ya uchaguzi.

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Arusha (CCM),Catherine Magige alitumia nafasi ya kusalimia wananchi aliyopewa na mkuu wa mkoa huo, Mrisho Gambo kumtambulisha Dr. Kiruswa na kusema amekuwa akimtuma Bungeni kuzungumzia matatizo ya Longido.
"Yale ambayo nimekuwa nikiyazungumza bungeni kuiomba serikali, huyu hapa (akimwonyesha) Dr. Kiruswa ndiyo alikuwa ananiambia, kila siku ananisumbua kwenye simu. Yeye hakushinda ubunge lakini anatekeleza ilani ya Chama Cha Mapinduzi kupitia mimi, " alisema Magige.

Mwananchi.

Hoja:Kulikuwa na ulazima wa Mkuu wa Mkoa kualika mbunge asalimie wananchi kikampeni kwenye shughuli ya Serikali?

Kwani Longido haikuwa na mbunge mpaka Magige atumwe bungeni na Kiruswa?

Kiruswa hana mamlaka ya kutuma mtu wa kumwakilisha bungeni wakati yeye si mbunge.

NEC fuatilieni hii habari.
 
Bunge haliko live tutahakikisha vipi kama alipeleka shida bungeni?
Hata kama hakupeleka, ni makosa kuwaambia wananchi walio na mbunge kwamba yeye anatumwa na mtu asiye mbunge kuwawakilisha, sababu, aliwahi kugombea ubunge.

Hii ni tabia mbaya ya kumdharau mbunge aliyekuwepo na ni kinyume cha taratibu. Asubiri uchaguzi, kama atashinda atamaliza hamu yake ya kuwakilisha wananchi.
 
Kule mbeya tulia akson anacheza ngoma na wananchi wasikie upinzani kafanya hivyo polisi wa ccm watavamia mara moja nchi ya hovyo sana hii kuna mijitu haimuogopi Mungu yanamtaja taja tu wakati maongo hayana sifa ya kutaja jina la Mungu.
 
Back
Top Bottom