Wabunge wa CCM aibu

Steph Curry

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2012
Posts
5,936
Reaction score
4,713
Huitaji kuwa na degree kutambua upumbavu wa wabunge wa CCM.. Hichi kisa kimetokea muda huu bungeni.

Baada ya Ester Matiko kutoa hoja, sasa Naibu Spika anahoji bunge..

Naibu Spika : Wanaohafiki hoja ya Ester Bulaya (alikosea jina) waseme NDIO..

Wabunge wa CCM: Ndioooooooooooo

Naibu Spika : Samahani sio Ester Bulaya, ngoja nihoji tena "Wanaohafiki hoja ya Ester Matiko wasime ndio"

Wabunge wa CCM : "kimya"

Naibu Spika : wasiohafiki hoja ya Ester Matiko wasime sio.

Wabunge wa CCM : Siooooooooo

Ina maana wao wanapiga kura kwa kusikiliza mijadala au kusikiliza majina?? Ina maana kama jina ni la mpinzani jibu ni sio hata kama hoja hiyo inafaa. Maana mwanzo walipohoji kwa jina la Ester Bulaya waliikubali hoja..




 
Yote haya inaonyesha ni namna gani tunatumia fedha za serikali kwa maaslahi ya ccm na si yataifa. Hainiingii akilini kuwa na kundi la watu bungeni badala ya kuangalia hoja na umhimu wake kwa taifa, wanaangalia watu na umuhimu wao kwa ccm.

Lazima Ccm waondoke!.
 
Hata mimi huu upumbavu wahawa ndungu unanishangaza sana.
 
naona wameamua kufia chama na siyo raia walio watuma ama kweli ccm ni janga kuliko majanga mengine wakazane kuvuga kwenye bvr tu vinginevyo wengi hatutakua nao kwenye bunge lijalo
 
Tubadilishe Serekali October kwenye Sanduku la kura hiyo ndio inayowafa tu

tatizo wanafanya kila hila ili warudi magogoni kwani wakiacha hawajui pakuficha sura zao kwa zulma wanazotufanyia akina siye
 
maccm yamechoka Mkuu wanachostahili ni kutupa kule na kuyasahau kabisa. Jina tu la mbunge linasababisha hoja kukubaliwa au kukataliwa!

 


Kwamba hatma ya nchi hii imekuwa, iko na wako wanaotaka iendelee kuwa mikononi mwa hawa wajinga, wapuuzi na wapumbavu inashangaza, inasikitisha, inaudhi na inakasirisha.
 
Ingawaje Siko Chama Chochote Lakini Nimeona Jinsi Uchama Unatumika Bungeni Hata Kama Kuna Jambo Lenye Maslahi Kwa Taifa Linaweza Kukwamishwa Kwasababu Ya Uchama
 
mkuu angalia tu usijekufa kwa presha na hasira tukapoteza nguvu kazi ya taifa cha msingi tukomae tu awa wapuuzi wasirudi afta oktober

Asante kipngozi kwa ushauri maana inauma mpk inaweza tengeneza sumu
 
maccm yamechoka Mkuu wanachostahili ni kutupa kule na kuyasahau kabisa. Jina tu la mbunge linasababisha hoja kukubaliwa au kukataliwa!

Mkuu hii imenishangaza sana.. Hawa sijui ni wabunge wa aina gani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…