WABUNGE Vs WASANII

mwanatanu

JF-Expert Member
Jan 22, 2008
851
127
Leo hebu tujikumbushe, kwa wale ambao mlikuwepo enzi hizo za wabunge wakiitwa ndugu.
Hawa wabunge walikuwa wakivaa zile shati za Chuo en Lai ama Kaunda suit.

Wabunge hawa muda mwingi walikuwa majimboni, mara tunakutana nao kwenye vilabu vya kunywa ulazi na mara tunakutana nao bar wakiteremsha bia kusafisha koo baada ya kunywa koomoni.

Wabunge hawa walikuwa wakipanda basi zile za relwe wakitumia warrant kutoka serikalini na wakifika Dar hawa Wabunge walikuwa wakipatikana saa za jioni mitaani uswazini. Kwa kifupi walikuwa ni watu wa watu wanaojua maisha ya kila siku ya sisi watu wa kawaida.

Sasa tumevamiwa na hawa wasanii wanojiita wabunge,ambao lazima uwaite mheshimiwa. Maisha yao ya ubunge hawajui hata bei ya kilo ya maharage.

Hawa wasanii chakula,mavazi yao wanaletewa tu nyumbani.
Wengi wao hawako jimboni wako Dar huwaoni uswazi wala vilabuni wao wako Kempinski wakifanya madeal na wasanii wenzao waitwao wawekezaji.......

..........inaendelea
 
Hawa Wabunge wa sasa ambao mimi nawaita Wasanii wamesoma shule na kutunukiwa mashahada ya kununua ili wakija kuomba kura tuwaheshimu ati ni wasomi.

Hawa wasanii wakishapewa kura hatuwaoni tena majimboni mpaka baada ya miaka mitano na wakija huishia makao makuu ya mkoa wakitafuta viwanja vya kujenga haswa kule wanako ita ati uzunguni.

Hawa wasanii wana wapambe ambao ati wanaitwa washauri....he jamani

inaendelea........
 
Back
Top Bottom