MKWEPA KODI
JF-Expert Member
- Nov 28, 2015
- 28,700
- 71,119
Jamani eti ccm madiwani 73 ukawa 87 wapi na wapi lakini bado wanalazimisha mamluki
Kwahiyo na wale wa zanzibar.....ni wakazi wa dar je sheria za serekali za mitaa inaruhusu ?? je serekali za mitaa ni miongoni mwa mbo ya muungano??
......bingwa, sheria bila kujali kama inafaa au haifai, haitingishiwi kibiriti....!ukileta mchezo wa siasa kwenye masuala ya sheria, sheria itakuletea kinyume chake!we nae ni kama jipu hunielewi! Inawezekanaje Mimi mbunge wa Kisarawe nishiriki kumchagua mwenyekiti wa halmashauri ya Kisarawe ilikotokea nafasi yangu ya ubunge viti maalum, halafu kwakua naishi Ilala tena nimchague Meya wa Manispaa? Mbone haya miaka yote hayakuwepo? Huu ni upumbavu kila mtu anoshindwa anaibua ujinga.
Hapo unatunga sheria yako sasa...1. hoja ni rahisi huwezi kuwa diwani wa eneo ambalo huishi na ili kuthibitisha ukazi wa eneo njia rahisi siyo chama kusema wala nini bali ni eneo ulilopiga kura ndiko makazi yapo yalipo. kwahiyo hao wabunge wa viti maalum wa zbar ili kuthibitisha ukazi wao ni lazima waseme walipiga kura wapi ?????????
2. kutakuwa na sababu gani za msingi kwa mtu kwenda katika mkoa fulani au zanzibar kuomba nafsi ya kiti maalum kwa kutoa ahadi ya kuwatumikia wakazi hao halafu kupigiwa kura ndani ya chama katika mkoa huo au zbar halafu uwende ukawakilishe watu wa eneo lingine?? huu ni kama utapeli fulani yaani uje hapa
utuombe tukuchague halafu uende ukawawakilishe watu wengine sasa si bora tungemchagua wa kwetu hapa hapa na je wausika hawa waliwaambia wapiga kura wao kuwa wakiwapa kura halafu watakwenda kuamia dsm kuwakilisha kwa udiwani???
3. suala la serikali ya mitaa ni none union issue kwahiyo hawakutakiwa hata kukanyaga jengone kwani ni suala
liko wazi na ndio maana huwezi kusikia mzanzibar anaongoza wizara ya TAMISEMI kwa kuwa si wizara ya muu
ngano.
Huu ni utata. mtu anaweza kujaza fomu hiyo leo lakini baada ya muda akaiuza hiyo nyumba kama ni yake au akahama kama anapanga na kuishi jimbo lingine. je hiyo fomu inakuwa opdated? kwa nini mtu asiwe diwani alikopatia ubunge tu?Something fishy
mimi nashauri wabunge wote wa kuchaguliwa kuanzia leo wote waamie dar alafu kwenye mikoa walikotoka wachaguliwe wabunge wengineMKURUGENZI wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Ramadhan Kailima, amesema wabunge wa Viti Maalumu wanaruhusiwa kuwa madiwani katika maeneo wanakotoka.
Alitoa ufafanuzi huo jana, alipozungumza na gazeti hili kuhusu hatua ya vyama vya siasa, ikiwemo CCM kuongeza idadi ya madiwani wake kutoka kundi la wabunge wa viti maalumu, katika chaguzi za mameya hasa jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Kailima, Sheria ya Serikali za Mitaa inatambua kuwa kila mbunge ni diwani katika eneo anakotoka, hivyo wabunge wa viti maalumu, ni madiwani katika maeneo wanakoishi.
Kwa kuzingatia sheria hiyo, wabunge wa viti maalumu wanapoomba nafasi hiyo ndani ya vyama na kuteuliwa, Kailima alisema, wanatakiwa kujaza fomu namba 8D ya NEC inayoelezea maeneo wanayoishi, ambayo ndiyo inayotumika kuwapa uhalali wa kuwa madiwani katika maeneo hayo.
Maombi ya CCM, Chadema Kailima alisema mwishoni mwa wiki, vyama vya CCM na Chadema waliandikia barua kwenda NEC kuomba uthibitisho wa makazi ya wabunge wake wa viti maalumu, ili utumike kuwaidhinisha kuwa madiwani katika halmashauri za Mkoa wa Dar es Salaam.
Alisema CCM walikwenda na barua ikiwa na orodha ya madiwani inaotaka wathibitishwe ukazi wao na nakala ya fomu namba 8D, ambayo mbunge husika wa viti maalumu alijaza kabla ya kuteuliwa, inayoonesha anuani ya eneo analoishi.
Hivyo CCM kwa mujibu wa Kailima, walithibitisha makazi na anuani ya wabunge wanaoishi Kinondoni, wakajiridhisha kisha wakachukua fomu yenye majina ya wabunge wote wa viti maalumu na kuweka alama ya tiki katika majina ya wabunge wanaostahili kuwa madiwani katika Halmashauri ya Kinondoni.
Alisema baadae Chadema walikwenda NEC na barua, lakini bila nakala ya fomu namba 8D, hata hivyo kwa kutumia fomu hizo zilizopo NEC, wakathibitisha wabunge wa viti maalumu wa chama hicho waliokuwa wakazi na wasio wakazi wa Kinondoni, mbele ya Mwenyekiti wao Freeman Mbowe na ofisa wao mmoja.
Kailima alisema kabla ya Mbowe kuondoka, aliomba kuthibitisha pia wabunge wa viti maalumu ambao ni wakazi wa Ilala bila kuwa na barua, ambapo aliruhusiwa kuthibitisha.
Alisisitiza kuwa kazi hiyo ya kuthibitisha ukaazi wa wabunge wa viti maalumu, ili kutambua wanakoweza kuwa madiwani, inafanywa na NEC kwa kuwa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), hawana uwezo kutoa uthibitisho huo.
Hivi karibuni, wakati wa uchaguzi wa Meya wa Kinondoni, vyama vya upinzani vililalamika kuburuzwa katika uchaguzi huo, kwa madai kuwa CCM ilitaka kuongeza madiwani wa Viti Maalumu tisa, kutoka kundi la wabunge wa viti maalumu.
Vyama hivyo vilidai kuwa, hatua ya wabunge hao wa viti maalumu kuwa madiwani wa viti maalumu Kinondoni, ni uchakachuaji wa wazi wa kura za kumpata Meya wa manispaa hiyo.
Kama umemuelewa, basi utakuwa una akili za hali ya juu kabisa.Kailima kaeleweka, na ufafanuzi wa form 8D, umeeleweka pia......hapa ukweli unaobaki ni labda juu ya sheria isiyofaa, lkn baada ya ufafanuzi, hiyo sheria iko...CCM, tofauti a wengine, waliijua, na walijiandaa kuitumia, na wanaonekana hawatanii ktk hilo...
we nae ni kama jipu hunielewi! Inawezekanaje Mimi mbunge wa Kisarawe nishiriki kumchagua mwenyekiti wa halmashauri ya Kisarawe ilikotokea nafasi yangu ya ubunge viti maalum, halafu kwakua naishi Ilala tena nimchague Meya wa Manispaa? Mbone haya miaka yote hayakuwepo? Huu ni upumbavu kila mtu anoshindwa anaibua ujinga.
.....awali, sheria inapingwa na sheria...na si hisia...labda nikujibu kwa kukuuliza, kuna kipengele cha sheria,ambacho kimetengua sheria na kanuni ya form D8(ambayo kimsingi naona haifai)?....sad truth ni sheria iliyopo, ingawa inaonekana haifai, na kailima kathibitisha hilo...Kama umemuelewa, basi utakuwa una akili za hali ya juu kabisa.
1. Ni diwani sehemu anayotoka, haina maana ni diwani sehemu anayoishi. Hawezi kuwa diwani sehemu mbili tofauti. Kama tunavyojuwa mbunge akiwa Waziri makaazi yake ni Dar! Jee awache kuwakilisha sehemu anayotoka aiwakilishe Dar? Dar itakuwa na madiwani wangapi?
2. Mbunge wa kuteuliwa na raisi anajaza hiyo form 8D? Kama hajajaza sehemu anayotoka itatafsiriwa vipi? Sehemu alopigia kura, au kijijini kwao?
3. Mkurugenzi kqshindwa kutaja ni kifungu gani hicho cha sheria alichokitafsiri. Au kawa Jecha na yeye?
Uliyemfahamu naomba utufafanulie
Unaniuliza mimo kipengele cha sheria kinachopingana na sheria yenye kipengele ya form 8D wakati huyo Mkurugenzi wa NEC hata hiyo sheria inayohalalisha hiyo form 8D yeye hajaitaja? Mimi suala langu la msingi ni kutaka kujuwa ni kifungu gani cha sheria ya uchaguzi kina halalisha hayo, akitaje. Katoa maelezo tu hajakitaja kifungu gani......awali, sheria inapingwa na sheria...na si hisia...labda nikujibu kwa kukuuliza, kuna kipengele cha sheria,ambacho kimetengua sheria na kanuni ya form D8(ambayo kimsingi naona haifai)?....sad truth ni sheria iliyopo, ingawa inaonekana haifai, na kailima kathibitisha hilo...
...mbunge wa viti maalum akijaza hiyo form kisheria, anaonesha anuani ya makazi yake, na kupata wadhifa wa udiwani ktk halmashauri yaliko makazi yake...CCM waliijua hiyo sheria, na walijiandaa kuitumia...