Wabunge tusaidieni: Sheria ya kustaafu miaka 55 kwa hiari na 60 kwa lazima imepitwa na wakati

sirluta

JF-Expert Member
Nov 28, 2012
6,325
2,487
Sheria hii ya watumishi wa Umma ya kustaafu ukiwa na miaka 55 kwa hiari na miaka 60 kwa lazima, sijui ni ya mwaka gani ila naiona imepitwa na wakati kwani ukifanya mahesabu utakuta ni 1/3 hufikia umri huo, na wale wanaofikia umri huo wakistaafu, kati ya hiyo theluthi moja, nusu yake ndo hulipwa kiinua mgongo chao bila usumbufu. Na baada ya hapo mafao hawapati zaidi ya miaka kumi, wanakuwa wameshatangulia mbele za haki lakini pesa zinafyekwa.

Kwa kuwa life span ya Mtanzania inazidi kushuka kutokana na sababu mbalimbali, umri wa kustaafu uvutwe hadi miaka 50 kwa hiari na 55 iwe ni lazima. Hii itamsaidia mstaafu kufaidi japo kidogo maisha ya uzeeni na pia kutoa fursa za ajira kwa vijana.

Japo jingine katika umri wa kustaafu kwa hiari, mtumishi ambaye ana cheo, aondolewe cheo kile ili ajiandae kustaafu maana 80% ya watumishi wanaotakiwa kustaafu kwa hiari, wenye vyeo mbali mbali wamekuwa vyanzo vya matatizo maofisini kwakuwa wanajua wataondoka hivi karibuni. Wapo pia ambao wamekuwa ni wazembe sana pengine ni kutokana na uzee na hivyo kufanya kazi haziendi.

Wabunge ambao kazi yenu ni kutunga na kurekebisha sheria twawaomba mfanye kazi hizo na siyo kuvurugana kila mara huku mkiacha mambo ya msingi.

Nawasilisha
cc: Waziri wa Katiba na Sheria
 
LABDA MPELEKEENI Mbunge Wa Jimbo Lako Aipeleke Kama HOJA Binafsi!!! ANGALIZO Kama Mbunge Wenu Ni Kutoka UKAWA, Bora Muahirishe Kwanza!!! MAANA Kwa BUNGE Hili La 11, Lilivyo Na Uvyama Na Ubaguzi, WABUNGE Wa CCM HAWATAKUBALI HOJA Hiyo KUTOLEWA Na MBUNGE Toka UKAWA!! HATA Kama Ina Maslahi Kwa WATANZANIA Walio Ktk Mpango Huo!!! Watapinga Na JOB NDUGAI, DKT TULIA Au MZEE WA VIJISENTI Wataitupa PEMBENI!!!! LABDA Awe Mwenzao, Otherwise BORA Kuacha Tu!!! Au Mtafute Yule Wa Upande Wao!!!
 
Back
Top Bottom