Wabunge tafakarini: Je, bado tunahitaji miezi 3 kujadili bajeti ya miezi 12?

Hili ndilo jambo natamani rais wangu alifanyie kazi kupunguza hiyo miezi na mishahara pia warudi kulima kazi ya kutumikia wananchi ibaki kuwa wito tu
 
Hili si jambo dogo kwa mawaziri na wabunge kutumia miezi 3 kujadili bajeti ya miezi 12 ambayo kimsingi ingeweza kujadiliwa na kupitishwa ndani ya wiki 3. Nitoe tu rai kwa wabunge wetu walitafakari hili kama kweli tunataka kuiendea nchi ya viwanda. Ahsante!
Naunga mkono hoja, maana kwa aina ya bunge hili bora hata likafutwa kabisa tukabaki na mihimili miwili tu Serikali na Mahakama, japo nayo Mahakama imeanza kumezwa na Serikali lakini angalau inajikongoja kongoja kuwapa haki kwa raia
 
Huu ni ujinga grade one, kukaa kujadili bajeti isiyotekelezeka hata robo yake.Kwanza yanayojadiliwa kwenye ule ukumbi hakuna kinachofanyiwa kazi hata moja, Bunge linalofanya kazi kwa sasa ni la JPM na Mwanae basi.Hili la JAMHURI YA MUUNGANO WA TZ bora hata lingevunjwa tu kwa sababu, halina kazi tena.
 
Sioni tija yoyote!!! Hata maswali yanayotolewa ufafanuzi sioni tija yake.
Ikiwa kama ni Bunge la Bajeti, iwe bajeti tu! Ndani ya mwezi mmoja inatosha.
Kwa shughuli nyingine kama kutunga sheria, maswali n.k itengwe mwezi mmoja mmoja.
Kwa mfano, June ni bajeti tu!!! November na February kwa masuala mengine.
 
Ilitakiwa kufikia Mei Mosi bajeti iwe imeshapitishwa!
Mkuu aina hii ya bunge kuna haja kweli ya kukaa na kujadili bajeti?! Bajeti zilipaswa kujadiliwa huko huko kwenye baraza la mawaziri na kupitishwa huko huko bila hata kufika ndani ya bunge
tapatalk_1522785797246.jpeg

Hapa wamefanya kama kijiwe cha kupigia stori hawana hata muda wa kumsikiliza Waziri anasema nini halafu akihitimisha wote kwa pamoja wanasema wanaunga mkono hoja bila hata kujua nini kilichomo
 
Hili si jambo dogo kwa mawaziri na wabunge kutumia miezi 3 kujadili bajeti ya miezi 12 ambayo kimsingi ingeweza kujadiliwa na kupitishwa ndani ya wiki 3. Nitoe tu rai kwa wabunge wetu walitafakari hili kama kweli tunataka kuiendea nchi ya viwanda. Ahsante!

Bajeti yenyewe hahiheshimiwi. Sozinje na mtoto wa Dada yake wanajipangia matumizi yasiyopitishwa na Bunge.
 
Bunge la bajeti la kazi gani wkt Rais ndiye anaye amuru pesa kiasi fulani peleka kwenye miradi ambayo haijapitishwa na Bunge?
Bunge la TZ linakaa kutumia tu pesa za watz pasipo kuwa na shughuli yyt ile ya kufanya!!
 
Back
Top Bottom