Wabunge sita wa Kenya wakamatwa kwa kutoa matamshi ya chuki

real G

JF-Expert Member
Feb 7, 2013
5,227
5,292
160614105930_muthama_512x288_bbc_nocredit.jpg

Wabunge sita nchini Kenya wanatarajiwa kuwasilishwa mahakamani kufuatia madai ya kutoa matamshi ya chuki.

Siku ya Jumapili mbunge mmoja anayegemea upande wa serikali alidaiwa kutaka kuuawa kwa aliyekuwa waziri mkuu na kiongozi wa upinzani nchini humo Raila Odinga.

Wabunge hao ni Moses Kuria, Kimani Ngunjiri na Ferdinand Waititu kutoka kwa upande wa serikali na Junet Mohammed Aisha Jumwa,Johnson Muthama na Timothy Bosire upande wa upinzani.

Bw Kuria anadaiwa kuitisha kuuawa kwa Raila kupitia lugha ya kikikuyu.Hathivyo amekana kutoa matamshi hayo.

Wabunge wa Upinzani walifanya mkutano na wanahabari siku ya Jumatatu na kutoa wito kwa wafuasi wa chama hicho kulinda uongozi wa chama hicho kwa kuwa serikali imeshindwa kufanya hivyo.

Polisi wamesema kuwa tamko hilo ni la chuki.Wanne hao wanatoa ushahidi katika kituo kimoja cha polisi katika mji mkuu Nairobi.Wabunge watatu wa Jubilee walitoa matamshi hayo usiku wa kumia Jumanne.

Mkuu wa idara ya jinai Ndegwa Muhoro amewaambia waandishi kwamba polisi watamkamata mtu yeyote anayeeneza matamshi ya chuki.

Chanzo: BBC
 
Tatizo kenya kila kabila lina chombo cha habari
Unakuta ukabila unakuzwa na vyombo hivyo

Hilo pia jana limewekwa wazi hapa

Vyombo vya habari vya lugha asili vyadaiwa kupalilia ukabila

VUGUVUGU la uhamasisho mashinani (Kengo) Jumanne limesema kuwa vyombo vya habari vinavyotangaza kwa lugha asili ni “vizalishaji vya utengano wa kijamii.”

Mshirikishi wa kundi hilo Mlima Kenya Bi Bernice Wandia akiongea Mjini Thika alisema kuwa “vyombo hivyo vinafaa kumulikwa kwa undani na mikakati iwekwe ya kudhibiti jinsi vituo hivyo husajili msikilizaji na mtazamaji wao katika makundi haramu ya ukabila.”

Bi Wandia alisema kuwa vyombo hivyo huwa na programu za kisiasa ambapo waalikwa huwa ni wa jamii yenye lugha ya kituo hicho “na ambapo katika usiri wa kinyumba huwa wanatoa matamshi hatari kwa utaifa.”

Alisema kuwa “mimi kama wa kutoka Jamii ya Agikuyu najua waziwazi kuhusu baadhi ya watangazaji wa vipindi kadha ambao kila uchao
wanachochea hisia za kikabila, kudunisha makabila mengine na pia vyama vinavyodhaniwa kuwa hasimu kisiasa.”

Alisema kuwa baadhi ya vipindi hivyo hushirikishwa na wanasiasa wabishi ambao “hawaogopi lolote katika usiri wa unyumba kurushia
makabila mengine cheche za matusi, kuwaangazia wapiga kura kutoka jamii zingine kama wasiojielewa na wanaofaa kukaliwa kisiasa kupitia
kukosa kuchagua wagombezi wao wa urais.”

Alisema kuwa jitihada zote za serikali za kuunganisha Wakenya hazitafua dafu iwapo “vyombo ambavyo vinatumika kuwasilisha jumbe hizo
za umoja ni vilevile ambavyo vina vipindi vya kutenganisha taifa.”

Bi Wandia alisema kuwa katika siku za hivi majuzi ambapo mrengo wa Cord umekuwa ukiandamana dhidi ya Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC), kumekuwa na “harakati za kina za kuangazia Cord kama muungano wa wasioaminika kisiasa na ambao hawafai kuwa mamlakani.”
Kudumisha utengano
Alisema kuwa hali ni iyo hiyo katika jamii zingine ambapo kulingana na mrengo ambao watangazaji wa vipindi wanaunga mkono, matamshi ni ya kudunisha na kuwatenganisha Wakenya.

Bi Wandia alisema kuwa “wanasiasa hutumia lugha zao za mama kuwasilisha jumbe za kukera na ambapo Mkenya wa kawaida aliye
mashinani hukumbatia mwongozo huo wa kuchukia jamii zingine na vyama vyao.
“Kuna virusi angani na hilo ni kwa uhakika. Virusi hivyo vya ukabila na utengano vinasambazwa na vyombo vya habari kupitia mitambo kuwa
mikononi mwa wakabila, wasiojumuika katika uzalendo wa umoja na walio na mtazamo kuwa jamii zao zina haki ya kuwa mamlakani kuliko zingine,” akasema.

Alionya kuwa ikiwa hatari hiyo haitatafutiwa dawa yake kama suala la dharura, wanasiasa watachoma taifa hili mitamboni ya redio, Wakenya
watabakia kugawanyishwa kwa misingi ya kidini, kisiasa na kikabila na hatimaye harakati zote za kusaka umoja wa Wakenya vibakie kuwa ndoto tu.

Bi Wandia alisema kuwa mitambo iyo hiyo ya redio inatumiwa kwa kiwango kikuu katika kupendekeza wanasiasa ambao hawafai Wakenya kwa vigezo vya huduma bora.

“Wengine wa wanahabari hao ndio wanajipigia debe kuwa wanawania nyadhifa fulani na wanatumia fursa hiyo ya kuwa wamiliki wa mitambo ya matangazo kujipia debe huku wakidunisha wapinzani wao kinyume cha sheria. Wengine wanachapia kampeni wale wanasiasa ambao wamepoteza umaarufu ili wapiga kura waanze kuwaona kwa ufaafu,” akasema.

Alisema vyombo vya habari vikiwa havitawajibila pakuu katika kuwaleta Wakenya pamoja, kutekeleza la haki kwa wote bila ubaguzi na kuzingatia maelekezo ya kitaaluma, basgi vitabakia kuwa adui wa ustawi wa taifa.
 
Siasa za kenya nizavituko

Sonko fights with Nairobi Governor Evans Kidero

Senate Public Accounts Committee meeting wass violently disrupted as Nairobi Senator Mike Sonko engages in physical fight with Nairobi Governor Evans Kidero.

The sitting was violently disrupted Wednesday morning as the senator and governor engaged in a physical fight.

Sonko started a verbal exchange which worsened into a physical exchange, forcing the committee to adjourn indefinitely.
 
160614105930_muthama_512x288_bbc_nocredit.jpg

Wabunge sita nchini Kenya wanatarajiwa kuwasilishwa mahakamani kufuatia madai ya kutoa matamshi ya chuki.

Siku ya Jumapili mbunge mmoja anayegemea upande wa serikali alidaiwa kutaka kuuawa kwa aliyekuwa waziri mkuu na kiongozi wa upinzani nchini humo Raila Odinga.

Wabunge hao ni Moses Kuria, Kimani Ngunjiri na Ferdinand Waititu kutoka kwa upande wa serikali na Junet Mohammed Aisha Jumwa,Johnson Muthama na Timothy Bosire upande wa upinzani.

Bw Kuria anadaiwa kuitisha kuuawa kwa Raila kupitia lugha ya kikikuyu.Hathivyo amekana kutoa matamshi hayo.

Wabunge wa Upinzani walifanya mkutano na wanahabari siku ya Jumatatu na kutoa wito kwa wafuasi wa chama hicho kulinda uongozi wa chama hicho kwa kuwa serikali imeshindwa kufanya hivyo.

Polisi wamesema kuwa tamko hilo ni la chuki.Wanne hao wanatoa ushahidi katika kituo kimoja cha polisi katika mji mkuu Nairobi.Wabunge watatu wa Jubilee walitoa matamshi hayo usiku wa kumia Jumanne.

Mkuu wa idara ya jinai Ndegwa Muhoro amewaambia waandishi kwamba polisi watamkamata mtu yeyote anayeeneza matamshi ya chuki.

Chanzo: BBC

Hahaha nilifikiri kuna freedom of expression au uhuru wa kuongea utakalo sasa iweje mnawakamata tena, wana demokrasia? Waacheni tu waendelee kuongea watakavyo ninyi si wazungu bhana kama USA mna freedom of speech, Kenya siyo kama Tanzania bhana, ni demokrasia full, hapa TZ ukitukana raisi unashitakiwa, blah blah...
 
Hilo lakuiga wazungu litawatokea puani

Wazungu hawashauri mpinzani auawe kama ilivyo kenya

Ndio maana naamini Bwana Juma aliuliwa na serikali
a83570dadb396a0610eee3fc7a55a5c6.jpg
 
Hahaha nilifikiri kuna freedom of expression au uhuru wa kuongea utakalo sasa iweje mnawakamata tena, wana demokrasia? Waacheni tu waendelee kuongea watakavyo ninyi si wazungu bhana kama USA mna freedom of speech, Kenya siyo kama Tanzania bhana, ni demokrasia full, hapa TZ ukitukana raisi unashitakiwa, blah blah...
we vipi?kenya kuna freedom of speech but sio freedom ya uchochezi......acha kutwist hoja ili ujipatie mti wa kuegemea.uchochezi sio mambo ya freedom of speech.nkt
 
Back
Top Bottom