Wabunge Nigeria waruka ukuta ili kuingia bungeni

Wabunge Nigeria waruka ukuta ili kuingia bungeni

MeinKempf

JF-Expert Member
Joined
Jun 11, 2013
Posts
11,092
Reaction score
7,236
Ukweli ni kwamba kuna story ambayo unaweza ukasimuliwa na rafiki yako ama mtu yoyote halafu ukaona kama ni uzushi na hakuna ukweli wowote.

Pata picha pale ambapo Spika wa Bunge pamoja na Wabunge wanafungiwa geti la kuingia ndani ya Ukumbi Bunge.

Nakupa story kutoka Nigeria, Spika wa Bunge la Nchi hiyo Aminu Tambuwal amelazimika kuingia ndani ya Bunge kupitia mlango mdogo wa dharura baada ya Polisi kufunga milango ya Bunge hilo kwa sababu za kiusalama

Spika huyo alijitambulisha kwa Maafisa Usalama hao ili wamruhusu aingie lakini hakuna aliyeonekana kujali ombi lake wala kumjibu, japo baadaye walimruhusu aingie kupitia mlango mdogo wa dharura huku wabunge wengine wakizuiwa kuingia kitendo kilichowafanya waamue maamuzi magumu ya kuingia ndani ya Bunge kwa kuruka ukuta.

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nigeria, Suleiman Abba amesema walilazimika kuzuia mtu yeyote kuingia ndani ya jengo hilo na kuweka ulinzi wa hali ya juu baada ya kupata taarifa kwamba kuna majambazi walipanga kuvamia Bunge hilo.

Polisi waliwashambulia kwa gesi ya machozi Wabunge waliokaidi amri ya kutokuingia Bungeni, Wabunge wawili walipoteza fahamu katika vurugu hizo.
 

Attachments

  • NIGERIA.jpg
    NIGERIA.jpg
    33.1 KB · Views: 806
  • NIGERIA2.jpg
    NIGERIA2.jpg
    42.6 KB · Views: 760
Nigeria ni kama hakuna serikali au wamegawana utawala na bokoharam.
 
Hata sie hatuna Serikali Mkuu, Tezi dume haijulikani atarudi lini akiwepo au asiwepo hakuna tofauti yeyote, P Pinda ndiye huyo kazomewa Bungeni tena kwa kishindo, hospitali hazina madawa na hazina nyeupe haina hata senti moja. Haya ukiyaangalia kwa kina utaona ni sawa tu kabisa kusema sasa hivi Tanzania haina Serikali.

Nigeria ni kama hakuna serikali au wamegawana utawala na bokoharam.
 
Hahaaaa kuna vitu vinafurahisha sana humu duniani
 
Back
Top Bottom