Wabunge na ofisi zao majimboni

kiunzi

JF-Expert Member
Nov 11, 2018
515
364
Nimekuwa na muda wa kutembelea ofisi za wabunge wengi majimboni mwao na kukutana na hali ambayo naomba ufafanuzi,katika baadhi ya ofisi majimboni mwao nimekuta milangoni na madirishani mchwa na mitando ya buibui imejijengea kiasi kwamba inaonesha imeweka makazi ya kudumu.
Baadhi ya ofisi nyasi mpaka milangoni na barazani ,sasa sijuwi hali ya ndani kama hao mende na mijusi wataikuta wao waingiapo.

Wananchi
wanalalamika,madiwani wanalia,viongozi mbalimbali nao hivyo ivyo! kulikoni!, hawa Waheshimiwa,
Baada ya kuchaguliwa tuu hawawaoni majimboni mwao!, siyo makatibu wao wala wao wenyewe.
Wengine wamebandika namba zao milangoni za uwongo! ukijaribu kupiga hata wiki nzima haipatikani.
Nikabaatika kukutana na baadhi ya madiwani mmoja wao kabeba mafaili yana miezi mitatu hajafanikiwa kumuona mbunge wake kuyapitia nakuidhinisha,hamuoni!.
Jamani Wabunge tengeni muda kuwa katika ofisi zenu wananchi wana mengi wanaitaji uwepo wenu na wana mengi ya kuwaambia mkawa wakilishe ,siyo kupoteya jiiiii baada ya tuu kuisha kwa uchaguzi.
Na hili ni wa vyama vyote siyo tawala wala upinzani na kama kuna anayebisha nitampatia majimbo husika yenye hizo ofisi awai kabla ya kusafisha au yeye Mhe. kufika ofisini.
Angalizo; siyo ofisi zote ni kama 45% hawo ndiyo mbaya zaidi.
Ahsante.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom