Wabunge na mswada wa katiba mpya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wabunge na mswada wa katiba mpya

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kachocho T.K, Nov 21, 2011.

 1. K

  Kachocho T.K Member

  #1
  Nov 21, 2011
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 25
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Wiki iliyopita nilikuwa nafuatalia mjadala wa mswada wa uundwaji wa katiba mpya ya amuhuri ya muungano wa Tanzania, uliojadiliwa bungeni kwa zaidi ya vikao vitatu mfululizo. Baada ya upinzani hasa peeeples na NCCR kuona ni usanii na kuamua kuususia mjadala wabunge wa chama kile pamoja na washirika wao wakaamua kutumia asilimia 95 ya muda kulaani kitendo cha mainteligensia kususia wakasahau majukumu yao ya kuchangia mswada huo. Najiuliza hivi wananchi tuliwatuma kutumia muda kuwajadili watu au kutoa mawazo yao kutetea watanzania walio wachagua? kwa nini posho walizolipwa kwa muda huo watanzania tusizidai zirudishwe kwani hawakuzifanyia kazi sitahiki kwa mujibu wa kifungu no............ cha katiba ile na kifungu no...... cha kanuni za kudumu za bunge km spika anavyotumia vifungu hivi kuwanyima haki ya kuzungumza wenzetu?
   
 2. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #2
  Nov 21, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Kabla hujadai posho za waliobaki bungeni kuujadili mswada na hatimaye kuupigia kura, jiulize yafuatayo.

  1. Hivi wale waliokimbia mjadala tuliwatuma wafanye hivyo?
  2. Hivi posho za siku hiyo wamezirejesha kutokana na kususia kazi waliyopewa na mwajiri wao?
  3. Kususia mijadala ni sehemu ya uwakilishi au ni moja ya hadidu za rejea za majukumu tuliyowatuma?
   
Loading...