Wabunge na Elimu ya shahada (Degree)

Sio uongozi wa siasa tu..uongozi wowote ule ulio bora msingi wake ni hekima, lakini ili uongozi huo uendelee kusimama na kutetea haki na usawa kwa unaowatawala, pamoja na hekima lazima pia uwe na uwezo wa kupamba na kupambanua mambo, kujenga na kutengua hoja,kuwa na fikra huru na za kina.....ambavyo hivi vyote vinajengwa na elimu! Ifike mahali serikali iogope kupeleka miswaada na budget za kihuni bungeni, kwasababu tu inaelewa aina ya watu ambao wanaenda kuifanyia maamuzi hiyo miswaada!

Oh yeah, ULIONA BAJETI PINZANI YA ZITTO KABWE ilivyokuwa na kasoro? Alisahau Kitu Muhimu kabisa Wapi pa

Kupata Income ? to relieve the GVT expenditure... wote wakaiona ni bogus... Hakuna anayeiongelea imetupwa

Jalalani; CUF wanataka Waweke yao... Yeye ni Msomi na Mwenye Degree kali ya UCHUMI...
 
I really doubt if that is a solution. Let's think of the number of PhDs and Professors that we have had in that house and what they have done so far.....! Mind you, we also have an economist and a PhD holder in the 'first office'!
But again mind you those Phd holders may use the same loophole of MPs being illiterate to still as they are not able to think outside the box due to lack of critical thinking ability. Look at most CCM MPs.
 
Salaam JF,
Ni hili swala la wabunge wa Jamhuri kuwa na elimu ya at least shahada ya kwanza (undergraduate degree)...juzi MH. John Mnyika alipokuwa anahutubia bunge kwenya mjadala wa bajeti kuu ya serikali alisema "tumefika hapa tulipo(kwenye umaskini wa kutupwa na hali ngumu ya maisha ambayo haijawai kutokea) kwasababu ya udhaifu wa raisi kikwete, uzembe wa bunge na upuuzi wa ccm"...kwenye hili swala la uzembe wa wabunge, naona kuna hoja mbadala zaidi ya uzembe, kuna wabunge wengi tu bungeni wanafanya/support maamuzi bila kujua athari zake kesho na kesho kutwa kwao( watakapotoka hapo mjengoni) na kwa jamii nzima kutokana na ukosefu wa elimu (ukomavu wa fikra), Majirani zetu hapo kenya wameshapitisha hili...kuanzia mwaka kesho hakuna mbunge ataruhusiwa kugombea bila kuwa na at least shahada ya kwanza, tusijipe moyo kwamba...mbona TZ wasomi ndio wanongoza kwa uwizi, ni wanaiba kwasababu wanajua bunge limejaa watu ambao hawajakomaa kiakili, ambao watapitisha hoja yeyote bila kujali uhalisia wake! Elimu kwa watu wanaotuongoza ni muhimu sana....."The function of education is to teach one to think intensively and to think critically. Intelligence plus character - that is the goal of true education." -Martin Luther kng Jr, Naamini hata sisi hatutakuwa tumewahi sana tukilijumuisha hili katika marekebisho ya katiba yanayoendelea.
Nawaisilisha.

Mimi nakuunga mkono 100%. Kuna haja ya kuweka hiki kifungu kwenye katiba. Ubunge husiwe ni kazi ya kuwakilisha tu wapiga kura bali pia uwe ni kazi ya uongozi na utaalam wa kuchambua na kujenga hoja zenye nguvu bungeni. Elimu inasaidia watu kujenga uwezo wa kufanya hivyo. Hivyo basi ili kujua kama mtu anayetaka kuwa mbunge atakuwa na uwezo huo lazima tutumie kiwango cha elimu kama kipimo. Hii itasadia kuondokana na bunge la kupiga muhuri hoja za serikali hata kama hazina tija kwa wananchi.
 
Oh yeah, ULIONA BAJETI PINZANI YA ZITTO KABWE ilivyokuwa na kasoro? Alisahau Kitu Muhimu kabisa Wapi pa

Kupata Income ? to relieve the GVT expenditure... wote wakaiona ni bogus... Hakuna anayeiongelea imetupwa

Jalalani; CUF wanataka Waweke yao... Yeye ni Msomi na Mwenye Degree kali ya UCHUMI...
I'm not pointing fingers at who did what and didnt do what....i just believe its great idea to have the house of parliament filled by intellectuals than the opposite! To have citizen's representatives who can reason and decide freely for the best of the community....to have representatives who will value their "YES" votes!
 
Naunga mkono hoja hii, pia nawashangaa sana wasiouona umuhimu wa kuwa na "intellectuals"
katika bunge letu. Ukweli unabaki palepale upo udhaifu mkubwa sana tunapokuwa na wawakilishi
wasiokuwa na uwezo wa kujenga hoja zenye mashiko, na kuthubutu kusema na kufanya maamuzi
kwa utashi wao kutokana na kile wanachokiamini na kuona kuwa ni sahihi kutokana na uwezo wao
wa kupambanua mambo.

Elimu ya shahada inafaa kabisa kuwa "at least level" ya kuanzia. Wasomi wapo wengi tu.
Tatizo ni kuwa na mawazo ambayo mimi binafsi naona kuwa ni potofu kuwa masuala ya siasa
ni umahiri wa kuongea. Tena naona tunazidi kupotea kabisa eti ukiwa maarufu iwe ni kwa uimbaji,
utangazaji, ukimwaga misaada basi inatosha.

On my views katika katiba mpya vigezo vitazamwe na kuboreshwa likiwemo hili la elimu.
Wenzetu wa Kenya wameshaliona hili sie siku zote tunazinduka wakati wenzetu wameshatangulia.
 
Mawazo haya ni mazuri mno, ila kunachangamoto nyingi ambazo zinajumuisha waheshimiwa wataka kura pamoja na watoa kura (jamii) kwa ujumla.Kweli huwezi kuchambua kitu kwa undani kama hukijui, matokeo yake ni kuuza sura mjengoni badala ya kutoa constructive ideas juu ya mada inayoongelewa unaanza kutoa lugha za matusi na kejeli kama inavyofanyika kule mjengoni.Lakini Wananchi pia tunapaswa kulaumiwa kwa namna mojaau nyingine maana kura zetu tunazitoa kwa wenye pesa bila kuzingatia kigezo cha elimu, kuna wasomi wengi wamegombea nafasi za uongozi kwa nyakati mbalimbali katika maeneo mbalimbali lakini tukawapiga chini miongoni mwa sababu ikiwa ni kukosa pesa. Wapiga kura tunahaja ya kuionyesha serikali kwamba tunataka mabadiliko kwa vitendo ili serikali isome alama za nyakati kama ilivyofanyika katika haja ya madailiko ya katiba
 
Mkuu Munyamakwa...tupo pamoja ili nadhani tusisubiri mpaka siku ya kupiga kura, kuna marekebisho ya katiba yanaendelea...tukipata nafasi ya kukutana na hawa akina warioba, tusikike kama tunavyosikika hapa JF!
 
I really doubt if that is a solution. Let's think of the number of PhDs and Professors that we have had in that house and what they have done so far.....! Mind you, we also have an economist and a PhD holder in the 'first office'!

Hata mie pia doubt lakini ukiangalia kwa makini wasomi mara nyingi huwa wanaingia pale ambapo pana opportunities. Ukiangalia historia ya bunge letu, kwa muda mrefu wabunge walikuwa wana shule ya kawaida na wasomi wengi walikuwa nje ya bunge wakifanya kazi nyingi za maendeleo na mambo yanakwenda. Tatizo limekuja pale ambapo posho na mishahara ilipoongezeka ndipo tukaanza kuona watu wengi wasio na sifa kuingia kwenye siasa iwe wasomi, wafanyabiashara na hata ambao sio wasomi. Mie mtazamo wangu hapa wasomi wengi walioingia kwenye bunge nawachukulia kama wanachukulia bunge kama sehemu ya ajira na si vinginevyo. Lakini all in all, wasomi wana mchango wa kuleta mabadiliko katika bunge letu endapo tu watakaoingia wawe na historia nzuri katika vyama vyao vya kisiasa
 
  • Thanks
Reactions: SMU
Degree za kusotea ndio degree si za KUNUNUA mfano.
Degree ya Komba, Anne kilango, Rage, Dr. Kamala, Dr. Nchimbi, Dr. Dhaifu..... Wote hawa na walionunua shahada utaona MATOKEO YAO DHAIFU.... so question hapa kubwa TCU IWE MACHO.... na wakome to legalize vyuo fake abroad most of which are internet Universities....havitoi
proper education zaidi ya biashara tu... i understand kuna LONG DISTANCE LEARNING INSTITUTIONS & VACITIES ILA TCU NDIO ITOE ACCREDITION kwamba zinafaa..... Matokeo tutakuwa na PROFESSIONALS FAKE EVERY WHERE.... utapasuliwa mguu ukiumwa kichwa na vice versa..... Leo nimesoma magazeti ...clinic moja huko Mwanza badala ya kumng'oa jino moja bovu Dr. akang'oa meno 3 mazima kaaahh.... Tz kila kitu kinawezekana... HATA TWIGA KAPANDISHWA NDEGE KWA NGUVU NA KAENEA UTASHANGAA SANA....1.2 bil ni VIJISENTI TU...
Shauri yenu...leo tena tsh 300bil za vigogo 6 zakutwa Swiss bank... Tz POLE Tz
 
Na yeye Zitto pamoja na elimu yake pengine hakuwa makini kuipitia hiyo budget kabla ya kuiwakilisha bungeni kwa kuwa naye pengine aimeishaona udhaifu wa bunge ambalo limekosa watu makini, kama angelifahamu hili basi kabla ya kuiwakilisha angeipitia kwanza kwa umakini. Bunge letu limejaa watu ambao si makini kwa mambo yenye msingi. Wanapewa makabrasha wanayahifadhi kwenye mikoba yao muda mwingi wanautumia sehemu kama chako ni chako nk. asubuhi kikaoni kwenda kupiga kura za ndiyo na hapana bila kufahamu wanachopitisha au kukataa kwa undani.
 
I really doubt if that is a solution. Let's think of the number of PhDs and Professors that we have had in that house and what they have done so far.....! Mind you, we also have an economist and a PhD holder in the 'first office'!

definitely yes problem hapa sio elimu bali ni uadilifu kuna wachumi wanasheria,waganga walio bobea lakini kwa kukosa uadilifu wamejikuta wakimezwa na ujinga wa kupitisha bajet kwa ushabiki sasa hii utasema unahitaji elimu gani kujua kwamba huu ni ujinga?
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom