Wabunge kwenda Malaysia kuikagua IRIS

Sooth

JF-Expert Member
Apr 27, 2009
3,928
5,615
IMG_4101.JPG

Ktk picha hii (kwa hisani ya Mjengwa), wabunge wa bunge la JMT wakipata kifungua kinywa leo asubuhi, uwanja wa ndege JKNIA DSM baada ya kutoka Malaysia kuichunguza na kubaini uwezo wa kampuni iliyopewa dhamana ya kutengeneza vitambulisho ya nchini malaysia-IRIS. Wanadai kampuni ina uwezo mzuri na imefanya kazi nchi mbalimbali, kwa hiyo tusiwe na wasiwasi.

Mimi najiuliza maswali mawili: Kwanin ubalozi wetu huko malaysia haukutumika kwa hili mpaka ikalazimu wabunge waende(hapa lengo ni kupunguza gharama)? Pili, kweli wabunge wetu wana 'utaalamu' wa kuchunguza uwezo wa kampuni kwa siku kadhaa na sio 'waambata' waliopo ubalozini? Msingi wa hoja yangu ni kujaribu kupunguza gharama kwa upande wa serikali, ili sekta zenye uhitaji zaidi ziweze kupata fedha za kutosha.
 
Kampuni hiko makini lakini wabunge kwenda kuichunguza ni uzushi, wanachunga nini?
wana taaluma gani ya kuchunguza kampuni kwa siku kadhaa.

mimi nadhani kila wakienda wawe wanawekwa kiti moto kwenye moja ya TV tunawapiga maswali
utagundua mambo wanayofahamu yote yako kwenye internet
 
View attachment 33680

Ktk picha hii (kwa hisani ya Mjengwa), wabunge wa bunge la JMT wakipata kifungua kinywa leo asubuhi, uwanja wa ndege JKNIA DSM baada ya kutoka Malaysia kuichunguza na kubaini uwezo wa kampuni iliyopewa dhamana ya kutengeneza vitambulisho ya nchini malaysia-IRIS. Wanadai kampuni ina uwezo mzuri na imefanya kazi nchi mbalimbali, kwa hiyo tusiwe na wasiwasi.

Mimi najiuliza maswali mawili: Kwanin ubalozi wetu huko malaysia haukutumika kwa hili mpaka ikalazimu wabunge waende(hapa lengo ni kupunguza gharama)? Pili, kweli wabunge wetu wana 'utaalamu' wa kuchunguza uwezo wa kampuni kwa siku kadhaa na sio 'waambata' waliopo ubalozini? Msingi wa hoja yangu ni kujaribu kupunguza gharama kwa upande wa serikali, ili sekta zenye uhitaji zaidi ziweze kupata fedha za kutosha.

Sijui Wabunge hawa wamepata wapi utaalamu wa "kuikagua" kampuni yoyote ile iwe ya ndani au nje ya nchi ili kujua kama ina uwezo wa kuukamilisha mkataba waliopewa na Serikali.
 
Tanzania kila kitu siasa ndio maana hakuna uwajibikaji, ina maana hatuna wataalamu wa kufanya hii kazi, isitoshe walishashinda zabuni wao wanakwenda kufanya nini huko?

waliowapa zabuni ina maana wamelizika nao tunaingia ghalama za nauli kila siku kwa mambo ya kijinga ina maana kila mbunge lazima aende kwenye ziara
 
Sijui Wabunge hawa wamepata wapi utaalamu wa "kuikagua" kampuni yoyote ile iwe ya ndani au nje ya nchi ili kujua kama ina uwezo wa kuukamilisha mkataba waliopewa na Serikali.

Mkuu B.A.K hujui hii serikali ni ya kulipana fadhila? Hao wabunge wamepewa allowance kwenda shopping na kuangalia nafasi za shule kwa ajili ya watotot wao...usione ajabu ndio walewale wanaumga mkono mjengoni mia kwa mia kila muswada unaolletwa mjengoni.
 
ndo tunapoingia mkenge kwa deal kubwa kama hili hakuhitaji Wabungw wala Ubalozi! ila leagal representatives! ina maana TZ inaingia mkataba na kampuni wa zaidi ya $120 mio. bila ya kuwa na wanasheria? btw ikumbukwe Rostam alikuwa anaenda enda sana huko mwishoni mwa mwaka jana na mwanzoni mwa mwaka huu! Yangu mie macho!
 
Na hivi majuzi wabunge si walienda pia Uingereza 'kuichunguza' BAE!

Sijui safari yao hiyo imesaidia kitu gani kingine ambacho Watanzania tulikuwa hatukifahamu kuhusu ufisadi ule wa ununuzi wa rada.
 
Hivi hao wabunge wamechaguliwa kwenda kukaguwa kwani wanautaalam gani?yaani huu ndo wizi wenyewe hamna wataalam husika mi wananiuzi kweli hawajamaa.......halafu jamaa wakiwa michosho wabunge walioenda wote jela miaka 30.
 
Mkuu B.A.K hujui hii serikali ni ya kulipana fadhila? Hao wabunge wamepewa allowance kwenda shopping na kuangalia nafasi za shule kwa ajili ya watotot wao...usione ajabu ndio walewale wanaumga mkono mjengoni mia kwa mia kila muswada unaolletwa mjengoni.

Ndani ya msafara, yupo Shibuda. Huyu jamaa ni mtaalam sana wa kutambua uwezo wa kampuni! lol!
 
Wanautaalam gani kama walienda kuangalia picha na rangi za vitambulisho sawa.
 
View attachment 33680

Ktk picha hii (kwa hisani ya Mjengwa), wabunge wa bunge la JMT wakipata kifungua kinywa leo asubuhi, uwanja wa ndege JKNIA DSM baada ya kutoka Malaysia kuichunguza na kubaini uwezo wa kampuni iliyopewa dhamana ya kutengeneza vitambulisho ya nchini malaysia-IRIS. Wanadai kampuni ina uwezo mzuri na imefanya kazi nchi mbalimbali, kwa hiyo tusiwe na wasiwasi.

Mimi najiuliza maswali mawili: Kwanin ubalozi wetu huko malaysia haukutumika kwa hili mpaka ikalazimu wabunge waende(hapa lengo ni kupunguza gharama)? Pili, kweli wabunge wetu wana 'utaalamu' wa kuchunguza uwezo wa kampuni kwa siku kadhaa na sio 'waambata' waliopo ubalozini? Msingi wa hoja yangu ni kujaribu kupunguza gharama kwa upande wa serikali, ili sekta zenye uhitaji zaidi ziweze kupata fedha za kutosha.
Tena kuna kitu kinaitwa 'diplomasia ya uchumi' sasa sijui hao mabalozi kwanini wasipate usaidizi wa wataalamu kufanya uchunguzi. Wao ni sehemu ya serikali na ni rahisi kuwawajibisha ikitokea vinginevyo.
Wabunge kama mhimili pekee hawana hadhi ya utendaji, hiyo ni kazi ya seikali kazi yao ni kuisimamia serikali itimize majukumu kama yalivyokusudiwa. Ikitokea mazingaombwe kama ya Richmond sijui nani atalihoji bunge au serikali maana kazi zimeshingiliana.
Je wabunge wanawezaje kuwajibika mambo yakienda kombo, nani atawawajisha. Wataalam wanawajibika mahali fulani.

Kazi za kitaalamu zifanywe na wataalamu, sio zifanywe mradi wa kupata posho. Hii nchi inakwenda kwa solar energy , hakuna human input.
 
Back
Top Bottom