Wabunge kukataa hoja ya Mh Mnyika kuthibiti matumizi holela ya Taasisi za serikali ni sawa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wabunge kukataa hoja ya Mh Mnyika kuthibiti matumizi holela ya Taasisi za serikali ni sawa?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Inanambo, Apr 14, 2012.

 1. Inanambo

  Inanambo JF-Expert Member

  #1
  Apr 14, 2012
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 2,865
  Likes Received: 1,149
  Trophy Points: 280
  Juzi nilikuwa nasilkiliza Bunge wakitunga sheria na kurekebisha sheria. Mh J. Mnyika alikuwa anatoa maoni kuhusu marekebisho ya matumizi ya Bajeti ya taasisi za Serikali. Kwamba kuna makusanyo wanafanya na kutumia hizo pesa wapendavyo bila kuingiliwa na Bunge au serikali. Mnyika akataka sheria itungwe kudhibiti matumizi ya hayo mapato au kodi. Mfano Ewura, THA, TRA, TCCA, TAA na wengineo wana mapato wanakusanya ambayo hutumia wapendavyo bila kuingiliwa na serikali mfano kujilipa posho za vikao, safari na mishahara mikubwa kuliko taasisi zingine za Umma na serikali ambayo imepelekea waTz waone hakuna usawa kwenye keki ya taifa. Taasisi hizi hufanya hivyo kwa sababu sheria inawaruhusu hivyo Mh Mnyika Jembe la Ukweli akataka sheria itenguliwe wapate kudhibitiwa hakuna matumizi nje ya Bajeti. Nilishangaa hakupata Support kwa Wabunge wenzake na sheria ilipita kama ilivyoandikwa. Nauliza tutajenga lini Usawa kwenye taasisi zetu ikiwa tunawakubali pesa zikusanywe na zitumike wengine wapendavyo?
   
 2. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #2
  Apr 14, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  tangia lini ccm ikaunga mkono hoja ya kupinga ubadhilifu na kuleta maendeleo kwa Taifa?
   
 3. Shark

  Shark JF-Expert Member

  #3
  Apr 14, 2012
  Joined: Jan 25, 2010
  Messages: 20,133
  Likes Received: 7,381
  Trophy Points: 280
  Hao wabunge wengine ni member kwenye hizo taasisi/mamlaka.

  Wengine wana "Kamlete" wao wengi tu wamejaa kwenye hizo taasisi pia.
   
 4. KASHOROBANA

  KASHOROBANA JF-Expert Member

  #4
  Apr 14, 2012
  Joined: Jul 30, 2011
  Messages: 3,249
  Likes Received: 406
  Trophy Points: 180
  Kwani hujui kuwa mbunge mmoja 1 wa chadema ni sawa na wabunge 30 wa ccm??? Imagine mapendekezo muhimu kama ayo yalotolewa na john mnyika yanaishia kupingwa na wabunge wa ccm, that is rediculus,
  my take: Nashauri kwa yeyote alomchagua mbunge wa ccm 2010 akatubu na ikibidi hakacheki yawezekana akili yake imeshake kama ya the great ***** may be (alipigwa concession)
   
 5. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #5
  Apr 14, 2012
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,668
  Likes Received: 21,901
  Trophy Points: 280
  Halafu wanajinadi eti ni wawakilishi wa wanamchi!
   
 6. k

  kaudagaa Member

  #6
  Apr 14, 2012
  Joined: Jan 14, 2012
  Messages: 31
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  :frusty:tatizo ni ubinafsi,na kuchumia tumbo.hawafikirii kizazi kijacho ambao ni watoto wao,ndio maana ukienda kwa wenzetu wanathamini sana watoto wao.
  Mfano mzuri ni mamvi ameanza kuiba tangu enzi za nyerere na bado hatosheki...lakini naamini ipo siku yatatokea ya Zambia chini ya Satta
   
 7. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #7
  Apr 14, 2012
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Wabunge hao hao wa CCM waliunga mkono hoja ya manunuzi ya vitu chakavu
   
 8. R

  Rweyemam Member

  #8
  Apr 14, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 55
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Ninatamani Mh Mnyika awasilishe hoja binafsi Bungeni kuhusu kuthibitiwa matumizi ya pesa kwenye taasisi za Serikali ambazo kwa sasa hivi haziingiliwi na Bunge.
   
 9. B

  Bobuk JF-Expert Member

  #9
  Apr 14, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 5,876
  Likes Received: 481
  Trophy Points: 180
  Tatizo ni letu kufikiri kwamba ipo siku Serikali ya CCM na wabunge wake watabadilika na kutetea masilahi ya Taifa. Wabunge wa CCM hawawezi kuunga mkono hiyo hoja ya Mnyika because huko kwenye taasisi hizo ndiyo CCM hufanya ufisadi wa kufa mtu. Nani asiyefahamu kwamba hizo TAASISI kama TANAPA hutoa pesa kusaidia kampeni za CCM. Nani hafahamu taasisi kama NSSF au PPF, CCM ilichota huko pesa kujenga ukumbi wa Chimwaga na kugharamikia mkutano mkuu wa CCM. nani aiyefahamu kwamba baada serikali kufilifisika imekwenda kukopa pesa NSSF, PPF na hata NMB.

  Bottomline hao wabunge wa CCM wako kwenye board za taasisi (pamoja na sheria kukataza mfano Mh. Rosemary kiligini), members wa board hizo huchota mapesa huko kujilipa ma-posho na kujipangia safari za nje. Tumeshuhudua Mizengo Pinda alilipwa 400,000/- @ day kuhudhulia semina ya madini.

  CCM na Ufiasdi ni damu damu, wewe ukitaka ukosane na CCM Jaribu kupinga ufisadi. CCM ni CANCER ambayo inabidi ikatwe kutoka mwilini. Wako wapi wabunge hao VIJANA wa CCM akina Makamba Jnr, Deo Filikunjombe, Dr. Kigwangalaah, Lugola mbona hatukuwasikia wakiinua hata midomo yao, kupinga hiyo sheria inayopalilia UFISADI kwenye taasisi za umma?

  Tukubari UKWELI with CCM nchi hii itaendelea kupiga MARK TIME kama sio kuendelea BACKWARD!
   
 10. e

  evoddy JF-Expert Member

  #10
  Apr 14, 2012
  Joined: Nov 9, 2011
  Messages: 302
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Mnyika katimiza kile tulichomtuma watanzania wao ccm wanaendelea kuliangamiza taifa lakini wananchi tunawajua watetezi wa kweri.CCM NA POSHO NI SAWA NA SIMBA NA NYAMA
   
 11. i pad3

  i pad3 JF-Expert Member

  #11
  Apr 14, 2012
  Joined: Mar 16, 2012
  Messages: 1,520
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  si mliwapigia kura?
   
 12. F

  Froida JF-Expert Member

  #12
  Apr 14, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Yaani ni waajabu sana fikiria watu kama hao unadhani kweli wana nia njema na taifa hili,wamepitisha kwa sababu wameweka mwanya wao na chama chao CCM wazitumie pindi wanapozitaka kwa mfano miaka 35 ya CCM,kuendeshea magazeti kama uhuru,radio uhuru, fedha zote zinatoka huko
   
 13. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #13
  Apr 14, 2012
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,709
  Trophy Points: 280
  Ulishaambiwa kuwa mjengoni vilaza ni wengi wala huhitaji kujiuliza twice, kwanza inawezekana wengi waliokataa hawakuelewa hoja yenyewe, na wengi huwa hawapo au wamechapa usingizi. Wanakataa si kwamba haina uzito bali ni kwasababu ya ile tabia yetu ya kuwa na mtiririko hasi (fallacious argument) na kuongea kutumia hoja ya "wengi wape hata kama ni vilaza" argumentum ad populum" au arguing by appealing to the emotions of the people"

  Hili litaendelea kuifanya Tanganyika izidi kudorora, wengi hasa wabunge wa CCM kusema la kweli, wanazikataa hoja za Wapinzani kwasababu tu ni wapinzani wala si kwababu hazina mantiki, na hii tunaiita "argumentum ad hominem" yaani argument against the personality!!!!
   
 14. N

  Naytsory JF-Expert Member

  #14
  Apr 14, 2012
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 1,593
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Chadema jipeni moyo mtashinda, hizo hoja zenye maslahi kwa Taifa wenyewe kwa wingi wao bungeni wameikataa ninyi zileteni kwetu wananchi ambao 20 15 tutawauliza hao wabunge wa ccm kwanini hawakujali maslahi ya watanzania walipokuwa bungeni? Hivyo hawatufai.
   
 15. C

  Curriculum Specialist JF-Expert Member

  #15
  Apr 14, 2012
  Joined: Oct 8, 2007
  Messages: 2,736
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Siyo sawa ni kuendeleza wizi!
   
 16. H

  Haika JF-Expert Member

  #16
  Apr 14, 2012
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,318
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Roho iliniuma sana hadi nikabadili channel, yani zile ndiooooooo" nilikuwa nahisi kizunguzungu!!

  Hivi hawa wabunge, ni binadamu kweli? watanzania wenzetu, wenye lengo moja? huwa napata aibu sana kufikiria watu wale wazima na familia wanavyotia aibu, nahisi ni kama mimi.

  KILICHONIFARIJI NI KUWA IMEINGIA KATIKA HANSARD, BASI. HUWEZI JUA HUKO MBELENI. SIE NA MUNGU WETU.
   
 17. N

  Ndinani JF-Expert Member

  #17
  Apr 14, 2012
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 5,413
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Hawakupigiwa kura za kuwachagua bali waliiba kura ili waonekane wamechaguliwa!! Sasa waliiba kwa kuwa kura zilizopigwa hazikulindwa ila sasa tumegundua kuwa kupiga kura peke yake hakutoshi bali kupiga kura na kuzilinda kura ndio dawa peke yake ya kukishinda ya chama cha magamba!!
   
 18. Inanambo

  Inanambo JF-Expert Member

  #18
  Apr 14, 2012
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 2,865
  Likes Received: 1,149
  Trophy Points: 280
  siku hiyo nilimsikia CAG akisimulia jinsi fedha za serikali zinavyofanyiwa ubadhirifu wa hali ya juu bila kujumuisha hizi ambazo huzina uthibiti wa serikali na Bunge. nadhani wakiamua pia kizitafiti watagundua ubadhirifu wa kutisha kuliko huo wa fedha zilizo kwenye Bajeti. Kweli Mheshimiwa Mnyika ni mtafiti na anajua anachoongea Bungeni na yule Mwenyekiti alimwambia maybe hiyo sheria itakuwa 'in Future' nadhani alikuwa anamdhihaki tu siyo kukubaliana naye. Kama waliotoa maoni hapo juu ni vema MH. upeleke hoja binafsi na sisi tutakuunga mkono.
   
 19. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #19
  Apr 14, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 554
  Trophy Points: 280
  Achilia mbali kabisa kukubali hoja, hakuna mbunge wa CCM wala Mwana CCM yeyote anayetaka Ubunge anaweza akakubali kusikiliza mazungumzo ya kupunguza au kubana matumisi katika eneo lolote lile ndani na nje ya Mipaka ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania sababu wanaogopa issue ya POSHO ZA VIKAO KWA WABUNGE ITARUDI. Na ninashangaa Mnyika kajisahau vipi kuiunganisha hii issue kwenye hoja yake au aliishiwa muda.
   
 20. l

  lubaga Member

  #20
  Apr 14, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 65
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tangu lini mtu aliyedumaa akili akawa na uwezo wakufikiri na kupambanua mambo kama makamanda wa chadema ,wabunge wa ccm wamedumaa akili akili zimekumbwa na utapia mlo ndiyo maana kila lilijema hulipinga kwa uwingi wao ,lakini mwisho wa ccm umekaribia hata mtoto wangu mwenye miaka miwili na siku nane ananisalimia kwa vidole viwili akimanisha yeye na chadema mpambanaji kwa hiyo sina shaka kwamba ccm imefika mwisho.
   
Loading...