Wabunge kimya stahiki za Tundu Lissu

Wabunge kimya stahiki za Tundu Lissu

kisingi

JF-Expert Member
Joined
Apr 9, 2014
Posts
516
Reaction score
377
Wakati bunge likiendelea mjini Dodoma sijasikia swali kuhusu bunge kutekeleza jukumu lake la kulipia matibabu ya mbunge Tundu Lissu anae tibiwa huko Belgium. Hivi ni woga wa wabunge ama ni shindikizo toka mahala fulani kuwa msihoji kuhusu matibabu na haki za Lissu toka bungeni. Tume soma taarifa nyingi zenye majibu ya ubabaishaji toka kwa Spika Ndugai ama Katibu wa bunge zenye kuonyesha nia ya kuto taka kulipa au kumpatia Lissu haki zake za kibunge. Mbona spika ulilipiwa kila kitu kule India. Chonde chonde wabunge simamieni haki za Lissu zipatikane. Hakuna ajuae kesho yake itakuwaje.
 
si alisema baada ya x-mas ataenda, hivi alienda kweli, manake sikusikia
 
Mtoa mada acha kiherehere chako bunge limeanza juzi tu unataka watu waanze kuulizia masuala ya matibabu ya lisu kanakwamba bunge /wabunge hawana majukumu mengine ya msingi ya kuyawakilisha hapo mjengoni, mda ukifika kila kitu kitawekwa wazi wacha papara zako.
 
Back
Top Bottom