Wabunge kataeni hili la TRA kukusanya mapato ya H/shauri mtakuja kujuta

2kimo

JF-Expert Member
Jan 23, 2014
2,029
2,072
Nadhani wabunge wote wanapaswa kuungana kupinga makusanyo ya pesa za halmashauri kufanywa na TRA.

Ni dhahiri kuna halmashauri hazitofaidika na pesa zao, na matokeo yake kuhamishwa kwenda halmashauri zilizoitwa maskini zaidi nchini!

Yaani leo, serikali ikae na kuanza kufikiria kuisadia Mwanza na kuiacha Manyara ijiendeshe?

Wabunge hebu kaeni na kutazama madhara ya mapato ya ndani kukusanywa na mpango! Wote mnalalamikia takwimu zake za juu ya hali ya kipato, sasa mna uhakika gani kama pesa za halmashauri zenu hazitotumika kwenda kusaidia mikoa ya kanda ya ziwa kwa kuwa ni maskini zaidi!
 
babu ubatoka manyara nn
Sitoki Manyara!
Ila vyanzo vya mapato vya ndani ni kwa ajili ya uboreshwaji wa eneo husika!
Mfano kwa hapa DSM, kulimaintain jiji hili si sawa na maintenance ya Manyara!
Sasa na huu mpango wa kusaidia mikoa maskini ndio naona sio kabisa, nazidi kupata hofu ya baadhi ya maeneo kuumia!
 
We ****** nn kama unavizia Tenda umekwama! Pesa zote serikali kuu
Una haja ya kutukana?
Sijui nadhani kama tungekuwa na mitambo ya kuzima akili feki, nadhani humu JF kuna watu kadhaa wangefungiwa vichwa vyao!
 
Sitoki Manyara!
Ila vyanzo vya mapato vya ndani ni kwa ajili ya uboreshwaji wa eneo husika!
Mfano kwa hapa DSM, kulimaintain jiji hili si sawa na maintenance ya Manyara!
Sasa na huu mpango wa kusaidia mikoa maskini ndio naona sio kabisa, nazidi kupata hofu ya baadhi ya maeneo kuumia!

Nchi hii ni moja sioni tatizo kusaidia mikoa maskini inyanyuke.

Migodi ya Mwanza na ndio imeijenga mikoa unayiotetea na wale watu walizuiwa kiyachimba.

Hapa kazi tu
 
Nchi hii ni moja sioni tatizo kusaidia mikoa maskini inyanyuke.

Migodi ya Mwanza na ndio imeijenga mikoa unayiotetea na wale watu walizuiwa kiyachimba.

Hapa kazi tu
Kwa hiyo hiyo mikoa ya Mwanza na Geita ni kuwa maskini au imefilisika?
Yaani sijaelewa!
Mikoa inayojenga mikoa mingine, leo inawezaje kuwa maskini?
Haiingii akilini!
Yaani hata Kojani Pemba ni tajiri kwa Mwanza!
Hakuna anayepinga maendeleo shirikishi, lkn sio hii ya kuanza na kutengeneza takwimu, then upelekeupeleke misaada!
Kama tulitumia takwimu za sensa 2012, sasa ni 4 years down the line data hizo zinaweza zisiwe valid, then tutumie vigezo gani kufanya evaluations?
Ni ngumu kumeza, Ila kuna dalili za maeneo kupata upendeleo!
 
TRA hawana resources za kutosha kufanya hiyo kazi effectively. Ni sawa na kumpa mtoto mchanga wa kulea mwanamke alozaa pacha wanne.
 
Wabunge wa ccm wako busy wao kuzuia wasikatwe asilimia 5 ya makato yao.. Wamependekeza kodi iongezwe kwenye mafuta kufidia hiyo iliyotaka kutolewa kwenye viinua mgongo vyao..

Hilo la manispaa kunyang'anywa uwezo wa kukusanya kodi za majengo ni mkakati maalum ambao wao wanaujua.. Wala usipoteze muda wako..
 
Back
Top Bottom