Tetesi: Wabunge kadhaa waanza kuwasiliana kwa ajili ya wao pia kuchukua maamuzi magumu

Chizi Maarifa

JF-Expert Member
Jul 29, 2013
10,859
24,647
Kama tu tungekuwa na BUNGE IMARA nchi hii ingeweza kusimamiwa kikamilifu kuweza kuyashinda mabaya inayoyakabili miaka nenda rudi.

Wabunge kadhaa wenye uchungu na nchi hii inasemekana wamenza kuwasiliana kwa njia mbali mbali wakitaka liitishwe bunge la dharura kuendana na kile kinachoonekana kama ni hali mbaya katika taifa hili.

Kumekuwa na hali ya mazonge mazonge kwa kipindi kirefu katika mambo mengi yanayoendelea hapa nchini kiasi kwamba taifa limekuwa siku zote likizidi kuelekea jioni na kupoteza nuru.

Inasemekana kuwa bunge ambalo nalo limejeruhiwa kwa kiasi kikubwa na milipuko hii ya magonjwa ana kusababisha wabunge wengi kuwa dhoofu na wengine kulazwa kwa sababu ya hali ya kisiasa nchi kuzidi kukaa tenge kwenye mhimili wake.

Wabunge kadhaa wameamua kuwasiliana na kuanza vikao iwezekanavyo wengine kujiuzulu nafasi zao ili mwenye uwezo wa kiuungu aziendeleze na pia wengine wapo tayari kutoa matamko bila kujali nafasi walizo nazo. haya yanaendelea kusemwa na watu mbalimbali wenye connections na watu wakubwa.

Kiuhalisia hali ni tete...tusubiri maana wanasema "kuti la mazoea lilimwangusha mgema" na pia katika hili kuna ahaja sana ya kufanya maombi maana wabunge kadhaa wenye vyeo vikubwa wamejipanga kufanya matamko makubwa zaidi.
 
Wafanye tu wanaloona ni SAHIHI na pia hao wanaotaka kufanya wanachoona ni sahihi na wao wanatakiwa WAWE NI WASAFI KWELI KWELI hili mwisho wa siku wakimunyooshea KIDOLE mwenzao kiwe na IMPACT......NA MWISHO WA SIKU RAIS atabaki kuwa RAIS tu na tena SI RAIS TU BALI RAIS mwenye MSIMAMO.....na ndio maana hata hao WALIOJIUZULU kwenye kamati ya BUNGE YA VIWANDA NA BIASHARA. kama kweli wanamaanisha wanachokisimamia basi wajiuzulu mpaka huo UBUNGE WAO.....hatutaki UNAFIKI
 
kama tu tungekuwa na BUNGE IMARA nchi hii ingeweza kusimamiwa kikamilifu kuweza kuyashinda mabaya inayoyakabili miaka nenda rudi.

wabunge kadhaa wenye uchungu na nchi hii inasemekana wamenza kuwasiliana kwa njia mbali mbali wakitaka liitishwe bunge la dharura kuendana na kile kinachoonekana kama ni hali mbaya katika taifa hili. kumekuwa na hali ya mazonge mazonge kwa kipindi kirefu katika mambo mengi yanayoendelea hapa nchini kiasi kwamba taifa limekuwa siku zote likizidi kuelekea jioni na kupoteza nuru.

inasemekana kuwa bunge ambalo nalo limejeruhiwa kwa kiasi kikubwa na milipuko hii ya magonjwa ana kusababisha wabunge wengi kuwa dhoofu na wengine kulazwa kwa sababu ya hali ya kisiasa nchi kuzidi kukaa tenge kwenye mhimili wake. wabunge kadhaa wameamua kuwasiliana na kuanza vikao iwezekanavyo wengine kujiuzulu nafasi zao ili mwenye uwezo wa kiuungu aziendeleze na pia wengine wapo tayari kutoa matamko bila kujali nafasi walizo nazo. haya yanaendelea kusemwa na watu mbalimbali wenye connections na watu wakubwa.

kiuhalisia hali ni tete...tusubiri maana wanasema "kuti la mazoea lilimwangusha mgema" na pia katika hili kuna ahaja sana ya kufanya maombi maana wabunge kadhaa wenye vyeo vikubwa wamejipanga kufanya matamko makubwa zaidi
Umejuaje, acha habari isiyo na mashiko! Wabunge wapi? Wa CCM? No Nothing!!
 
Bunge Imara ni utashi na Utayari wa Rais kwa hapa Bongo!

Jakaya aliua kamati ya Wabunge wa CCM ( kuifanya inactive ) kwa makusudi
Kabisa ili Wabunge wawe huru kujadili na kufikia Muafaka Bungeni bila ya kuingiliwa na Chama lakini Wapuuzi wakaona ule ni idhaifu!

Sasa hivi Kamati ya Wabunge wa CCM ipo active sana hivyo Bunge imara itabaki kuwa kwny karatasi
 
Shughuli aliyoifanya Mh rais pale Ubungo ni kubwa sana kwa maendeleo ya taifa hili......na hayo ndio maendeleo tuyatakayo na sio umbea na fitna za ajabu ajabu ambazo kimsingi hazitufikishi popote....u need to grow up
 
Wafanye tu wanaloona ni SAHIHI na pia hao wanaotaka kufanya wanachoona ni sahihi na wao wanatakiwa WAWE NI WASAFI KWELI KWELI hili mwisho wa siku wakimunyooshea KIDOLE mwenzao kiwe na IMPACT......NA MWISHO WA SIKU RAIS atabaki kuwa RAIS tu.....
TULIFUNDISHWA KATIKA SOMO KA URAIA KUWA BUNGE LINA UWEZO WA KUMTOA RAIS MADARAKANI KWA KUPIGA KURA YA KUTOKUWA NA IMANI NAE.
 
Msije mkamjalibu JPM alisshasena, yupotayari kulivunja bunge Mrudi kwenye Sanduku la kura, mimi nina imani JPM atarudi kwenye nafasiyake lakini kunawabunge hawatarudia.
 
Sio ccm au chadema au cuf wenye maamuzi magumu kwa malsahi ya taifa labda lissu wengine wote ni njaa tupu hakuna wakijuuzulu au kuchukua hatua mahususi maana njaa zimezidi uwezo wao wa kufikiri
 
Back
Top Bottom