Wabunge jitolee mishahara na posho ya 2020

Bishweko

JF-Expert Member
Joined
Sep 29, 2011
Messages
1,151
Points
2,000

Bishweko

JF-Expert Member
Joined Sep 29, 2011
1,151 2,000
Heshima kwenu wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ( JMT). Nawaomba sana tena kwa heshima yenu kua wasaidieni vijana wetu waliopo Vyuo Vikuu ambao wamekosa mkopo wa Serikali ili waweze kuendelea na masomo yao.

Vyuo mbali mbali apa nchi Tanzania kuna vijana watanzania wakike na kiume ambao wamekosa mikopo kutoka HESLB tangu waingia apo vyuoni.

Wengi wao wanaishi maisha magumu sana,wanabebana,wanakosa chakula na wengine waishia kukata tamaa kabisa.Nyie ni wawakirishi wao na sisi ambao tupo nje ya Bunge ingawa tunajitahidi kuwasaidia ata kwa kulipa kodi ya serikali.

Nawaomba sana tena sana okoeni kizazi hiki,okoeni wadogo zenu,ndugu zenu ata kwa kujitolea posho na mshahara wenu wa msimu mmoja wa Bunge utatosha angalua miaka mitatu. Hata ikishindikana basi ikopesheni Serikali nayo iwakopeshe hao watoto( wanafunzi) wetu ili wasome vizuri na kuja kulijenga ili Taifa.

Ahsante sana ila nawaomba ili lisiwe suala la itikadi za vyama vya Siasa.Nawashukuru sana.

Mungu Ibariki Tanzania
Mungu ibariki Afrika
Mungu bariki Bunge la JMT.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Bishweko

JF-Expert Member
Joined
Sep 29, 2011
Messages
1,151
Points
2,000

Bishweko

JF-Expert Member
Joined Sep 29, 2011
1,151 2,000

Forum statistics

Threads 1,390,281
Members 528,138
Posts 34,048,110
Top